Mgeni rasmi kwenye hafla ile alikuwa Rais wa Zanzibar. JK alipokaribishwa kuongea alisisitiza hili kwa kusema huyu ni Rais wa Zanzibar na sio Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na akataka huku bara tulielewe hili. Itifaki hii huwa inatumika pia kwenye sherehe za kila mwaka za siku ya Mapinduzi ya Zanzibar. Haishangazi sasa Waziri Mkuu wetu kuwa namba nne au chini ya hapo siku ile.
Tatizo lililopo ni mabadiliko yale ya Katiba ya Zanzibar kushindwa kuhuishwa ndani ya Katiba ya JMT na hivyo kuonekana ni batili. Hili litaleta taabu sana hata kwenye kuandika upya katiba yetu ijayo.
Tatizo lililopo ni mabadiliko yale ya Katiba ya Zanzibar kushindwa kuhuishwa ndani ya Katiba ya JMT na hivyo kuonekana ni batili. Hili litaleta taabu sana hata kwenye kuandika upya katiba yetu ijayo.