Crucifix
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 1,654
- 590
Siku ya jana kulifanyika ibada kubwa pale Zanzibar, na viongozi wakuu wa kitaifa walikuwepo. Nilishangazwa kwa jinsi protokali ya nchi hii ilivyomuweka Pinda nyuma ya JK, Bilal, Shein, Hamad na Idd. Kama ni waziri mkuu wa serikali ya muungano, basi hata rais wa Zanzibar anapaswa kuwa chini yake kwa maana Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.
Hii imenifanya nimwone PM kama kiranja wa 'Bara'. Mtu wa sita kwa hadhi Tanzania atasema nini Zanzibar ilhali juu yake kuna wazanzibari wanne? Najua katiba za Zanzibar ilifanyiwa marekebisho kwa kupeana vyeo lukuki, lakini ni lini katiba yetu imerekebishwa na kumshusha hadhi PM kwa kiasi hiki. Kwangu mimi jaji mkuu chande hata mama Makinda wana hadhi kubwa zaidi ya rais wa Zanzibar kwa sababu wanaweza kurithi urais wa Tanzania.
kuna baadhi ya wachangiaji wanahoji ati thread hii inasaidia nini kupunguza umaskini Tz........
Watu wenye hadhi ya juu ndio wenye ushawishi wa maamuzi yote. Ndio maana mataifa makubwa huya yanahangaika kutafuta "who are the most influencial" na hao ndio waamuzi wa mambo ya dunia likiwemo hilo la umaskini. Kuwa na "top layer" ya wazanzibari wanne ni kuweka mustakabali wa nchi yetu kwenye mikono yao, sawa na kuweka rehani 'utajiri' wetu kwa minajili ya kukubaliana kisiasa. "Our progress depends much on who rules and what shall happen if we are ruled by zanzibaris?