Waziri Mkuu Tanzania - Mtu wa sita kwa hadhi nyuma ya wazanzibari wanne

Inaongezaje pato la Taifa? Tukivunja Muungano au tukigawana majukumu kila mtu akawa na serikali yake tutapunguza mzigo wa gharama:

Tutapunguza gharama za kuwa na ma vice presidents na ma retired presidents kibao toka Zanzibar ambao wanahudumiwa na bajeti ya Muungano ambayo Zanzibar hawana cha kuchangia. Tutapunguza gharama za kuwalipa wabunge wa Zanzibar ambao hawahusiki katika mijadala mingi ya mambo yasiyo ya Muungano.

Tutapunguza gharama za umeme wa bure tunaowapa Zanzibar kwa maana serikali ya Mapinduzi imetangaza hawawalipi TANESCO! Tutapunguza mzigo wa kuwasomesha Wazanzibar vyuo vikuu vya bara.

Tutapunguza gharama za kuwatunza viongozi wa Zanzibar waliohamia Dar baada ya kustaafu, Salim Ahmed Salim, Ally Hassan Mwinyi, Abood Jumbe na wengine kibao. Tutaongeza ajira za Wabara ambazo tunalazimika kuwapa Wazanzibar serikalini kwa affirmative action.

Kimsingi, tutapunguza gharama kwa kutua mzigo wa kui finance Zanzibar, ambao hawana shukrani anyway. Na hapo bado hatujaongelea inherent injustices za sheria za Zanzibar zinazo declare wazi wazi kwamba Mtanzania Bara haruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar. Ndio maana wengine tunalilia kwa machungu kuvunja Muungano.

Hukijui hata unachosema. Just unabwabwaja tu. CRAP. Bora ungelikaa kimya.
 
Tuna marais watano, watau kwa watu m1 na wawili kwa watu m40, ndo maana PM anakuwa wa sita, esp huko visiwani japo kwa bara ni watatu.
 
Nami nashangaa...........WAJITOE TUU...................... WAZANZIBAR WOTE HAWAUTAKI LAKINI WAMEJAA KIBAO HUKU BARA KULIKO HATA IDADI YA WABARA WALIOKO KULE

Kwani mnashindwa nini kuitafuta TANGANYIKA YENU? Mpaka waanze Wazanzibari. ZANZIBAR Wameshasema tena sio mara moja hawataki MUUNGANO WA KIINI MACHO. Mnasubiri nini Wadanganyika? Au mnaogopa kivuli chenu.
 
Muungano wa Tanzania haupo sehemu yoyote duniani, si Union, si federation/confederation, huwezi kuupata muungano kama huu sehemu yoyote duniani.

Huwezi kunitajia hata nchi moja dunia hii ambayo inaundwa na muungano kama wa Tanzania.

Kwa hiyo hata protokali zake ziko evasive kama "wave/particle" like duality ya photon.
 
Kitu ambacho sielewi ni kuwa kwanini Wazanzibari wasiamue tu kutoka kwenye muungano mambo mengine yangekuwa rahisi kweli. Nadhani ni rahisi zaidi kuwa na uhusiano wa wa kinchi kuliko tulivyonao sasa ambao tumeukomplicate kwa mambo mengi tu. Labda miye itabidi nisaidie kuchochea hizi hisia za utaifa ili Zanzibar itoke kwenye muungano na tuwe na nchi huru mbili - sijui kama itakuwa ni pre revolution after independence au after revolution. Lakini wakati umefika kwa Wazanzibar siyo kukosoa waanze tu wazi kabisa kutaka kutoka kwenye muungano ili tuwe na nchi mbili nadhani mahusiano yatakuwa rahisi na more organized.

Wenye uwezo na mamlaka kisheria wa kuamua kuutaka au kuuukataa huo Muungano ni Bunge la Muungano na wala si baraza la wawakilishi. Kwa sababu Hati ya makubaliano ya muungano aliridhiwa na Bunge pekee na wala haikupelekwa kwenye baraza mpaka leo kwa ajili ya kurudhiwa.

Inaonekana wazi JMT haipo tayari kutoa hati hiyo ili ilidhiwe na baraza la wawakilishi. Kwa maneno machache na kwa mujibu wa Sheria za Zanzibar Muungano huo wa TNG na ZNZ ni BATILI.

Sasa wenye mamlaka ya kuujadili na hata kuuvunja ni Bunge la Makinda ambapo more than 75% ya member wake ni watu wa Bara.

Sasa kazi kwenu wa Bara kuvunja huo muungano au iambieni JMT ipeleke hiyo hati kule barazani ikachanwe chanwe kabisaaaaaaa
.
 
Pinda hana sifa ya kuwa PM
Pinda ni kiongozi wa Tanganyika hana nafasi yoyote akikanyaga ardhi ya NCHI ZANZIBAR
Viongozi Wa serikili ya Tanzania ni Rais na makamo wake.Pinda ni kiongozi Wa Tanganyika.
 
Hii inshu ya muungano kila nikiisikia huwa napata hasira sana.Nyerere katujengea uoga wa ajabu sana sisi watanganyika.Kafanikiwa kutuaminisha kuwa tusipoyafuata mawazo yake basi hatutakuwa na amani tena,tutauana tu yaani sisi kama hatuna akili vile ya kujua uovu na wema.

Hili dude muungano aliloliasisi limechangia sana sisi watanganyika kuwa masikini.Imagine,tungekuwa na serikali yetu ndogo tu ya Tanganyika ikiwa na Rais/Waziri Mkuu au Rais/Makamo wa Rais on top.Ningekuwa na uwezo hata sasa hivi ninavyoandika ningevunja huu muungano na kila mtu aanze kimpango wak.
 
Ijapokuwa kikatiba PM yupo juu, lakini kuna uwezekano katika sherehe ndani ya znz ni sawa kukaa baada ya hawa viongozi wa znz. Ukiangalia kwa ndani utaona PM yupo kibunge na kutekeleza kazi za serikali.

52.-(1) Waziri Mkuu atakuwa na madaraka juu ya udhibiti,

usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuli za
Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Waziri Mkuu atakuwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali
Bungeni.
(3) Katika utekelezaji wa madaraka yake, Waziri Mkuu
atatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au
mambo yoyote ambayo Rais ataagiza kwamba yatekelezwe.

Hasa ukiangalia 52(1) utaona kuwa kwa muda mwingi yeye anahusika na mambo ya Bara au Muungano. Kwa maoni yangu, akitua ZNZ, yeye yupo nyuma ya Rais wa ZNZ, na hivyo makamu wa rais pia. Lakini nashangaa hichi cheo cha makamu wa rais ZNZ kimeingizwa kinyemela!
 
Binadamu wakikupandisha juu, Mungu anakushusha. Pinda umeshushwa na wanadamu, Mungu wako atakupandisha...
 
Kwa hii miaka 47 nadhani muungano umeshafanya kazi vya kutosha. Sasa muda umefika wa kuingia ukarasa mpya. Either serikali moja au tatu. vingenevyo tuanzishe ujirani mwema.
 
Jamani hakuna cheo cha "rais wa Zanzibar". __

na hichi unaita nini?
103.-(1) Kutakuwa na Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar ambaye ndiye atakuwa Rais wa Zanzibar na Mkuu wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na vile vile Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi la Zanzibar.
 
Mwenzenu niliachwa hoi na kitu kingine kabisaaaaaaaaaaaaaaa!
.....................ALHAJI DOKTA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE! Halafu wakafululiza ma-alhaji kadhaa kabla ya Mzee wa kulialia!!

kwani naye ni Alhaj lini aliupata au nao ni honorary!!!! Wanazuoni mtuambie
 
Wacha uongo wewe! JK sio kitu znz? PM sio kitu znz? Wacha kutudanganya!
FYI, JK ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania. Yeye ndio big dog, waznz wapende wasipende.
Tusome katiba kwa makini:
1. Katiba ya Jamhuri Ya Muungano Tanzania
Ibara 1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano
Ibara 2. Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la
Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni
pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania
inapakana nayo.
Ibara 4 (3) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za umma
katika Jamhuri ya Muungano, na kwa ajili ya mgawanyo wa
madaraka juu ya shughuli hizo baina ya vyombo vilivyotajwa
katika ibara hii, kutakuwa na Mambo ya Muungano kama
yalivyoorodheshwa katika Nyongeza ya Kwanza iliyoko
mwishoni mwa Katiba hii, na pia kutakuwa na Mambo yasiyo
ya Muungano
ambayo ni mambo mengine yote yasiyo Mambo
ya Muungano.
Twende kwa Rais na Serikali:
Ibara 33.-(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na
Amiri Jeshi Mkuu.
Ibara 34.-(1) Kutakuwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano
katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengine yote
yahusuyo
Tanzania Bara.

Hivi mkuu baada ya kuisoma hiyo katiba umeifahamu?

Tanzania ni nchi ngapi? moja, mbili?
ok.. Tanzania ni Muungano
Muungano wa nchi ngapi?

Katiba imezaliwa na makubaliano ya Muungano(The Articles of Union between Tanganyika and Zanzibar).
Rudi kwenye hiyo document kama utakuta huko imetajwa Tanzania, au Tanzania bara na Tanzania Zanzibar.

Tumejitafutia matatizo na sasa tunakosa ujasiri wa kuyatatua.
Hapo mwanzoni wa thread , nilichangia na kusema ni lazima tulijue tatizo ili tuweze kulitatua.

Tatizo ni Muungano na muundo wake. Ni lazima tulishughulike hili halafu tuandike katiba ambayo inaendana na makubaliano juu ya Muungano na muundo wake. vyenginevyo tutasoma katiba sana na tutajihisi tunaifahamu na kuielewa..lakini ,tumeshasema kuwa hii katiba iliyopo ni bomu tayari.

Hivyo vijisehemu vyenye rangi nyekundu na buluu visome vizuri uone kama unavifahamu na kuvielewa kweli.
 
Katika hali ya kawaida, Muungano unakuwa na wanachama.
Muungano wa Tanzania una wanachama wangapi?

Wanachama hawa wanaitwaje?

Au muungano wa Tanzania hauna wanachama? au walikufa baada ya muungano? Kama walikufa kwa makubaliano yepi? Nani alitoa hukumu ya vifo vya wanachama wa muungano? Na alitoa wapi mamlaka ya kutoa hukumu ya vifo?

Kuna mambo ya Muungano na mambo ambayo si ya muungano....Je tunaposema ni one sovereign state...je mambo ambayo si ya muungano yataongozwa kwa uwezo upi? au mamlaka ipi?

Kwa nilivyoelewa mimi mambo yasiyo ya muungano yapo kwa kila mwanachama wa muungano huu, pia kuna mambo ya muungano ambayo wanachama wanayashughulikia kwa pamoja.

Kama kuna mtaalamu wa katiba ambaye anaweza kutusaidia kutufafanulia mkorogo huu, tafadhali ajaribu kutusaidia.
 
Hivi mkuu baada ya kuisoma hiyo katiba umeifahamu?

Tanzania ni nchi ngapi? moja, mbili?
ok.. Tanzania ni Muungano
Muungano wa nchi ngapi?

Katiba imezaliwa na makubaliano ya Muungano(The Articles of Union between Tanganyika and Zanzibar).
Rudi kwenye hiyo document kama utakuta huko imetajwa Tanzania, au Tanzania bara na Tanzania Zanzibar.

Tumejitafutia matatizo na sasa tunakosa ujasiri wa kuyatatua.
Hapo mwanzoni wa thread , nilichangia na kusema ni lazima tulijue tatizo ili tuweze kulitatua.

Tatizo ni Muungano na muundo wake. Ni lazima tulishughulike hili halafu tuandike katiba ambayo inaendana na makubaliano juu ya Muungano na muundo wake. vyenginevyo tutasoma katiba sana na tutajihisi tunaifahamu na kuielewa..lakini ,tumeshasema kuwa hii katiba iliyopo ni bomu tayari.

Hivyo vijisehemu vyenye rangi nyekundu na buluu visome vizuri uone kama unavifahamu na kuvielewa kweli.

Mbona unauliza maswali ambayo majibu unayo?
Tanzania ni nchi moja. Jina lake ni Jamhuri ya Muungano Tanzania. Katafute sehemu yeyote utaona hilo ndio official name.

Muungano ni kati ya bara na visiwani. Hapo pagumu ni lipi?
Kuna serikali mbili: Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Znz
Kuna vitu vinavyoangukia kwenye Muungano - articles of the union. Vipo 22.

Serikali ya Znz inaangalia vitu visivyoangukia kwenye Muungano kwa upande wa huko Znz.
Serikali ya Muungano inaangalia vitu vya Muungano na vitu visivyo vya Muungano kwa upande wa Bara.
Sasa ugumu ni upi jamani?

Hayo mengine yote ni upepo tu unavuma na nyakati. For me, the Union is clear cut!
Ivi mbona UK nayo ni a Union. Kuna Scotland, England, Wales na Northern Ireland. Kwenye michezo kuna timu ya England, Scotland, Wales na Northern Ireland. Lakini nenda UN utakuta hakuna hizo nchi, ipo UK tu!
Kuna bunge la UK, bunge la Scotland, nk. Lakini hakuna bunge la England. Unaelewa hapo?

We have a similar situation. Overtime, Znz wanaweza kudai bendera, national anthem, timu yao ya mpira, nk, lakini that does not mean kuwa hakuna a UNION GOVERNMENT! Soma historia ya UK mkuu. Unaweza kufumbuka macho kidogo.
We could be having a similar kind of Union.
 
Watu kama Tundu Lissu wenye muono wa mbali wakitahadharisha juu ya athari za baadaye endapo "vijitatizo" kama hivi havitatafutiwa dawa mapema wanaishia kuzomewa na kuzodolewa Bungeni na hao ambao mwisho wao wa kuona ni usawa wa pua zao.

Frankly speaking, hili la Muungano wa Tn na Zn lisipotafutiwa dawa ya kudumu, regardless itakuwa chungu namna gani, ni bomu baya kuliko hatari nyingine yoyote itakayoukabili ukanda huu wa Afrika Mashariki muda si mrefu ujao. Bomu hili lina sura zote chafu na za hatari zaidi kwa wakati huu - UTAIFA (sisi, wao; chetu chetu, chao chetu), UDINI (dini yetu tuko wengi, dini, dini, dini, ...), na UGAIDI. Inahitajika busara, umakini, na uthubutu wa hali ya juu kukabiliana na dude hili liitwalo muungano.

Umenena vema. Mficha maradhi kilio kitamuumbua. Litakalolipuka bomu kama la 'atomic' hapo ndipo kutakuwa kilio na kusaga meno.
 
Umenena vema. Mficha maradhi kilio kitamuumbua. Litakalolipuka bomu kama la 'atomic' hapo ndipo kutakuwa kilio na kusaga meno.
 
Back
Top Bottom