Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda Na Makongoro Nyerere Wateuliwa NEC ya CCM

Kama ni hivyo basi ungeanza kwanza kuwashauri chadema watenganishe KUB na Uwenyekiti wa chama, na hata pia waweke ukomo wa Uongozi ili wasije kung'ang'ania madarakani!

Niambie lini ofisi ya KUB imetoa tamko la uteuzi wa wajumbe wa kamati kuu CHADEMA?

Naona umeanza kwenda tenge..... ukomo wa uongozi CHADEMA una mahusiano gani na hii mada?
 
Huu ni ujinga mwingine tena, siyo Watanzania wote tunaohusika na ccm, by the way wanachama halisi wa ccm nchi nzima hawazidi millioni 2.

Hivyo basi mwenyekiti wa ccm ana haki ya kumteuwa mtu au watu anaowataka yeye.

Isitoshe huko ccm kati ya vijana na wazee, nakuhakikishia wazee ndio wenye akili za ujana ña vijana wenyewe walishazeeka akili siku nyingi tu, ujana wao umebaki katika makasha ya mwili tu.


Okay, kuna wana CCM milioni 2, sio lazima kuwa na Pinda, Pinda, Pinda miaka nenda miaka rudi
 
Ili wasigombee urais 2020.

Poor hao wanaolubali teuzi hizo yaani unatoka urais unakuwa balozi
 
Sio rais
Mwenyekiti wa chama
Pumabavu huyu mtoa taarifa! Yaani uteuzi wa chama lazima utolewe taarifa na kurugenzi ya mawasiliano ya Rais? Huu ni ujinga,, ameshindwa nini kumwachia Pole pole? Matumizi mabaya ya raslimali za walipa kodi!
 
Ninamuona mzee Pinda akivaa viatu vya Mangula huku Makongoro akivaa viatu vya Polepole
 
Atanyenyekea tu. Nafasi yenyewe kapewa kwa vile katika ziara yake ya wili tatu zilizopita mkoani Makongoro alipewa nafasi ya kusalimu akamfananisha Magu na Baba yake. Magu was tickled by that.

Mako sio mtu wa kunyenyekea

Jk alimpaaa ubunge na ujumbe wa NEC lakini uliza nani alianza kumshambulia jk na mtandao wake wa Lowassa,rostam na Membe Ndani ya chama.

Huyu ni mtu asiyeweza unafiki atakusifu ila ukiharibu anakuponda haogopi kuwa kijiweni ,yote kwake maisha tu
 
Wamechemka wote wawili mtoa taarifa na mteuzi (ndiye anayeidhinisha yaandikwe)
Msigwa rekebisha barua yako
Ikulu sio mali ya ccm
Unatumika kichama zaidi kuliko kulitumikia Taifa
Ukifika wakati wa kurudi mtaani utajutia baadhi ya maandishi yako
 
Hili halipaswi kuwa hivyo; shughuli za CCM zisemwe na CCM; shughuli za serikali zisemwe na serikali. Mwesiga anatoa taarifa kama nani? Yeye siyo msemaji wa Mwenyekiti wa CCM...
Watu wanahaki kabisa kusema weledi wa Msigwa ni wa kutilia shaka kabisa.
 
Hivi Grayson ni msemaji wa CCM?
Asiee huenda wafanya kazi wa serikali ni waccm
 
Nadhani dhana ya chama kushika hatamu na zama tulizopo haijaeleweka

Shughuli za serikali na za chama ni tofauti kwa mujibu wa mfumo wa siasa uliopo

Sina uhakika kama kutumia nembo ya barua za serikali kwa mambo ya chama ni sahihi!
Mimi nimeangalia nikasikitika sana.

Halafu nikawa naangalia kama kuna mtu mwingine ataona, isiwe nalalamika kwa sababu sijui mambo ya realpolitik Tanzania yakoje.

Shukurani mkuu kwa kuliona hili.
 
Back
Top Bottom