Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda Na Makongoro Nyerere Wateuliwa NEC ya CCM

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
IMG-20180525-WA0027.jpg


======
Makongoro afunguka:

Saa chache baada ya kuteuliwa kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Makongoro Nyerere amesema yupo tayari kwa kazi huku akiwaomba radhi wote aliowahi kuwakosea.

Taarifa za uteuzi wa Makongoro pamoja na Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda kuwa wajumbe wa NEC CCM, ilitumwa na mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa kwa vyombo vya habari saa nane usiku wa kuamkia jana na kuzua mjadala baadhi ya wanasiasa wakihoji sababu za kutotolewa na ofisi ya katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho.

Taarifa ya hiyo ya Ikulu imeeleza kuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli amefanya uteuzi huo kwa kutumia mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Katiba ya CCM toleo la mwaka 2017.

Akizungumzia uteuzi wake, Makongoro alisema awali alikuwa hajui lolote, lakini yuko tayari kwa majukumu mapya ya kazi aliyopangiwa huku akimshukuru kipekee Rais Magufuli kufanikisha uteuzi huo.

Alisema, “Nilikuwa benchi la wachezaji wa akiba kwa muda mrefu na nikawa ‘na troti’ kwa muda mrefu nikisubiri, lakini sasa ameamua niingie uwanjani,” alisema.

Mwanasiasa huyo alisema anachomuahidi mwenyekiti wake huyo ni kufanya kazi kwa bidii na kuwatumikia wananchi kwa unyenyekevu kama kaulimbiu yake ya ‘Hapa Kazi Tu’ inavyosema.

“Nimeshangaa sana, nilikuwa sijui (utezi wake), lakini mimi sio malaika wa mtume,” alisema mtoto huyo wa tano wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na kuongeza:

“Nimewahi kufanya makosa kadha wa kadha (huku akicheka kwa sauti) huenda huko nyuma niliwakwaza watu, ingawa binadamu tuna tabia ya kuangalia mema tu.”

Alipoulizwa anafikiri ni makosa gani aliyowahi kufanya siku za nyuma, Makongoro alisema: “Mimi ni mwanadamu wa kawaida na unapofanya siasa unafanya kwa moyo mweupe na mkunjufu. Naamini kuna watu niliwahi kuwakwaza sana tena sana tu, kwa hiyo kwa kuwa namwamini Mungu ninapogundua nimefanya hivyo lazima niombe radhi.

“Namshukuru mwenyekiti, nimejisikia heshima kubwa sana kwa kuniteua.”

Alipoulizwa ni watu gani aliowakwaza, Makongoro alisema, “Juzi nilikwenda kuomba kura za ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) na nilitumia nafasi hiyo kuwaomba radhi. Sasa suala la kukubali au kutokukubali huwezi kujua kama yameisha. Sina kipimo cha kujua kama yameisha au vipi, ingawa pia kura hazikutosha (akaendelea kucheka kwa sauti).

Makongoro alisema hata hotuba yake ilionyesha dhamira yake ya kuomba radhi.

Mjadala wa taarifa za uteuzi

Kuhusu mjadala kuhusu utolewaji wa taarifa hizo, Ikulu na CCM kwa nyakati tofauti walijibu wakisema Magufuli ni Rais wa wote na Msigwa ndiye msemaji wa Ikulu.

Msigwa alisema alisema Rais Magufuli hauvui urais wake muda wote na yeye ndiye msemaji wake.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Uhusiano wa Kimataifa, Ngemela Lubinga alisema chama hicho hakiwezi kuwazuia watu kulalamika.

“Hata mtu ukimpa chakula akala akavimbiwa bado atalalamika. Wanachotakiwa kufahamu watu ni kuwa, mwenyekiti wa CCM ndio Rais. Kwa mfano, anaweza kuwa katika safari ya kichama na akapata matatizo na kukawa hakuna watu wa mawasiliano Ikulu, kwa hiyo utatukataza tusitoe taarifa kama Rais amepata matatizo?” alihoji Lubinga.

Alisema Magufuli ni Rais na ni mwenyekiti wa chama hicho kwa hiyo Ikulu kutoa taarifa kama mwenyekiti amezungumza haina tofauti kwa kuwa watu ni walewale.

Miongoni mwa wanasiasa waliohoji sababu za Ikulu kutangaza uteuzi hui badala ya idara ya uenezi ya CCM ni mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF, Julius Mtatiro ambaye alisema msemaji wa Ikulu ni mtumishi wa Serikali na hakustahili kufanya kazi hiyo.

“Watanzania wanalazimishwa kukubali kuwa watumishi wa Serikali ni watumishi wa CCM. CCM ina msemaji wake, lakini mambo ya CCM yanatangazwa na Ikulu,” alihoji.

Kwa hisani ya Gazeti la Mwananchi
 
Huenda Makongoro Nyerere anaandaliwa kuwa katibu mkuu

Katibu mkuuu au Makamu alikuwa anatajwa cheo kikubwa tu hasa kutokana alivyozunguka nchi nzima kumpigia kampeni.

Wakati wa kampeni kulikuwa na Timu Tatu ya Rais akiwa na Bulembo
Makamu akiwa na wasaniii.

Na Timu ya Makongoro Nyerere
So it was all expected kuwa aidha angeweza kupewa ubunge na uwaziri muhimu au nafasi kubwa kwenye chama

Hasa kutokana na kuwa dhana nzima ya “turudishieni chama chetu” aliibeba yeye dhidi ya kuuondoa mtandao kama “senior agent “, na dhana nzima ya kuondoa “cartels “ kwenye uchumi ni yeye aliyeanza kuisemea.. ile hotuba yake ya kwanza ya kampeni zake ndio hasa inabeba dira ya haya yanayoendelea hadi leo ikiwa pia ni kazi nzuri ya TISS kuweka dira ya nchi , everything was well planned

Kassoro pekee inayotajwa kuchelewesha ni Tabia yake ya “kutonyenyekea” ila kuelekea 2019/20 JPM anahitaji tena kujenga Timu ya kampeni

Pinda sio mzuri Sana majukwaani ila ni mwanamkakati mzuri na mwanamfumo
 
Ni mambo ya kugawana KEKI ya TAIFA tu. Kuhusu maendeleo ya nchi tusubiri siku Mungu akitumbukuka
 
Back
Top Bottom