Waziri Mkuu, kwanini umeficha ripoti ya kuungua kwa soko la Kariakoo? Nini umeficha au unafikiri tumesahau?

Nafikiri uanzishwe uzi wa matamko ya Waziri Mkuu na Matamko na maagizo ya mkuu wa nchi. Hii itatusaidia kufuatilia maamuzi kwa manufaa ya wananchi.

Itakuwa hatari sana maana wataonekana waongo!
 
Soko la Karume nalo limeungua..

Wameunda Tume ya masaa 72 kuchunguza moto wa Karume
 
Baada ya kuungua kwa Soko la kariakooo yalisemwa mambo mengi ikiwemo hujuma au kuunguzwa kwa makusudi kwa soko husika. Lakini Waziri Mkuu aliunda Tume ya Uchunguzi na akawapa maagizo ya kumletea report ndani ya wiki mbili.

Kama ilivyo ada report iliwasilishwa ndani ya wiki mbili => Waziri Mkuu apokea taarifa ya Uchunguzi wa Moto soko la Kariakoo

Lakini baada ya kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu, matarajio ya wengi kama alivyoahidi ni kutoa report hiyo kwa Umma kuhusu kilichosababisha soko kuungua.

Pamoja na hayo yote ikumbukwe Waziri mkuu alishatoa tuhuma kwa watu kuhujumu soko hilo wakiwemo waliokuwa viongozi wa soko la Kariakoo waliofukuzwa na Rais Samia Suluhu kabla ya soko kuungua.

Watanzania walikuwa na hamu sana kujua nini kilisababisha soko hili kuungua. Kwanini Waziri mkuu ameficha hii report? Haina majibu aliyoyatarajia? Amezuiwa kuisoma?
Wahenga walisema, mficha uchi hazai na mficha maradhi kifo humuumbua. Sasa kuungua kwa soko la Karume leo wameumbuka.

Tunataka ripoti ya Tume iliyoundwa kuchunguza kuungua soko la Kariakoo otherwise hii Time iliyoundwa ya soko la Karume haina maana.
 
Kuyachoma moto masoko pia huwa ni mbinu ya kishetani Ili kuwalazimisha wafanyabiashara kupisha ujenzi bila kupenda
 
Wahenga walisema, mficha uchi hazai na mficha maradhi kifo humuumbua. Sasa kuungua kwa soko la Karume leo wameumbuka.

Tunataka ripoti ya Tume iliyoundwa kuchunguza kuungua soko la Kariakoo otherwise hii Time iliyoundwa ya soko la Karume haina maana.

Walisha watuhumu watu wameunguza sasa report naona ilisema kinyume na matatajio ya Rais na waziri mkuu...
 
Back
Top Bottom