Waziri Mkuu apokea ripoti ya Wafanyabiasha wa Kariakoo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,789
218,420
Taarifa ya leo inaonyesha kwamba Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa amepokea ripoti ya majadiliano kati ya serikali na Wafanyabiashara wa Kariakoo kutoka kwa Tume iliyoundwa ili kutatua mgogoro ulioanzishwa na TRA.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu amsaidie Waziri Mkuu ili safari hii ripoti hiyo iwekwe hadharani angalau na sisi wananchi tujue yaliyomo.
---

1687373508535.png

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Jumatano, Juni 21, 2023, Jijini Dodoma amepokea taarifa ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kupitia, kuchambua na kutoa mapendekezo ya kutatua changamoto za Wafanyabiashara nchini.

Taarifa hiyo imekabidhiwa na Mwenyekiti wa kamati, Dkt. John Jingu ambaye pia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.

Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, Waziri Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Ashatu Kijaji, Waziri wa Nchi OR – TAMISEMI, Angellah Kairuki, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ahmad Chande, Makatibu Wakuu, Makamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wanakamati na Wataalamu kutoka sekta mbalimbali za masuala ya kodi, biashara na uwekezaji.

Akiongea baada ya kupokea taarifa hiyo, Majaliwa amesema Kamati hiyo imefanya kazi kubwa na imeleta majibu ambayo yatatatua changamoto za Wafanyabiashara nchini na ameahidi kuwa Serikali imepokea taarifa hiyo na itayafanyia kazi mapendekezo na ushauri uliotolewa na Kamati hiyo.

Kamati hiyo ambayo ilipewa siku 14, imefanya mapitio katika maeneo mbalimbali ya kikodi, bandari na maeneo ya Wafanyabiashara kwenye Mikoa mbalimbali nchini.
 
.....na ile ripoti ya moto pale kariakooo sokoni waliitoa kwa public?,na pls my PM hujachelewa na usione utakua dhaifu ukiliomba taifa msamaha kwa kulipotosha wakati President Magufuli alipokua ana fight for his life na wewe ukaniongopea kuwa yupo salama na anaendelea na kazi ,huu ulikua ni uongo
 
hakika usimwamini mwanasiasa ,hapo hakuna lolote la maana porojo wafanyabiashara mjiandae kisaikolojia wembe ni ule ule
walifanya hvyo ili kupunguza joto lililokuwepo wakati ule
 
Back
Top Bottom