Waziri Mkuu, kwanini umeficha ripoti ya kuungua kwa soko la Kariakoo? Nini umeficha au unafikiri tumesahau?

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,763
2,000
Baada ya kuungua kwa Soko la kariakooo yalisemwa mambo mengi ikiwemo hujuma au kuunguzwa kwa makusudi kwa soko husika. Lakini Waziri Mkuu aliunda Tume ya Uchunguzi na akawapa maagizo ya kumletea report ndani ya wiki mbili.

Kama ilivyo ada report iliwasilishwa ndani ya wiki mbili => Waziri Mkuu apokea taarifa ya Uchunguzi wa Moto soko la Kariakoo

Lakini baada ya kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu, matarajio ya wengi kama alivyoahidi ni kutoa report hiyo kwa Umma kuhusu kilichosababisha soko kuungua.

Pamoja na hayo yote ikumbukwe Waziri mkuu alishatoa tuhuma kwa watu kuhujumu soko hilo wakiwemo waliokuwa viongozi wa soko la Kariakoo waliofukuzwa na Rais Samia Suluhu kabla ya soko kuungua.

Watanzania walikuwa na hamu sana kujua nini kilisababisha soko hili kuungua. Kwanini Waziri mkuu ameficha hii report? Haina majibu aliyoyatarajia? Amezuiwa kuisoma?
 
Ndalilo

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
2,154
2,000
Ni nani mwenye mamlaka ya mwisho kuruhusu ripoti iende public au ikae kifichoni? Yeye anasemaje?
 
Coaster2015

JF-Expert Member
Aug 21, 2018
2,535
2,000
Mkuu nami nilisema siku ile alipotoa taarifa kwamba ameunda tume ya kuchunguza, nilijua haitakuja kutoa majibu, serikali ikifahamu kwa watanzania huwa wasahaulifu saana, ni wachache kama wewe huwa wanafuatailia mambo, hapa watu wengi wanawaza matokeo ya yanga juzi, wameshasahau kwamba soko liliungua moto
 
Ngisibara

JF-Expert Member
Jan 2, 2009
3,107

Kudanganya Ni mazoea yao, Kuna mwingine alisema atatoa ripoti ya jengo la nasaco lilivyoungua mpaka wa leo Ni jii
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
18,791
2,000
Kocha hana utamaduni wa kufuatilia haya mambo!

Kwani ile ya BOT uliiona?
 
Mbekenga

JF-Expert Member
Jun 14, 2010
1,828
2,000
Nafikiri uanzishwe uzi wa matamko ya Waziri Mkuu na Matamko na maagizo ya mkuu wa nchi. Hii itatusaidia kufuatilia maamuzi kwa manufaa ya wananchi.
 
Coaster2015

JF-Expert Member
Aug 21, 2018
2,535
2,000
Nafikiri uanzishwe uzi wa matamko ya Waziri Mkuu na Matamko na maagizo ya mkuu wa nchi. Hii itatusaidia kufuatilia maamuzi kwa manufaa ya wananchi.
Uko sawa, tufike sehemu tuwalazimishe hawa jamaa kuwa wanatimiza ahadi wanazotoa, sio kuanzisha tume kuchunguza jambo, tume inakula hela za kodi zetu halafu ripoti inakuwa hiari yao kuitoa
 
Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,763
2,000
Mkuu nami nilisema siku ile alipotoa taarifa kwamba ameunda tume ya kuchunguza, nilijua haitakuja kutoa majibu, serikali ikifahamu kwa watanzania huwa wasahaulifu saana, ni wachache kama wewe huwa wanafuatailia mambo, hapa watu wengi wanawaza matokeo ya yanga juzi, wameshasahau kwamba soko liliungua moto
Mbaya zaidi aliwatuhumu watu nikajua kabisa ile report ndio itamaliza kazi lakini naona kimya
 
Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,763
2,000
Uko sawa, tufike sehemu tuwalazimishe hawa jamaa kuwa wanatimiza ahadi wanazotoa, sio kuanzisha tume kuchunguza jambo, tume inakula hela za kodi zetu halafu ripoti inakuwa hiari yao kuitoa
Hakika.....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom