Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,977
- 10,075
Suala la kuwa wapi siku zote atalijibu Alhamisi moja. Lakini sasa kuna suala la kuwataka madaktari wakutane naye lakini naona kama madaktari wanaanza kurukaruka: Mara hatuendi Karimjee mara tutakutana naye Jumatatu; aaaah. Kama waziri mkuu alichelewa kukutana nao (aliwatumia ujumbe wa.mawaziri) na wao ndio sasa wanatak kuchelewesha mchakato!Na yeye PM alikuwa wapi siku zote??
Wasipoangalia watakosa hata hako ka support walikokuwa wakikacommand toka kwa baadhi ya watu. Busara inahitajika hapa kuliko wakati mwingine wowote; wakiamua kutumia mtulinga matokeo yake hayatakuwa mazuri kwao.