Waziri Mkuu kukutana na madaktari kesho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mkuu kukutana na madaktari kesho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Jan 28, 2012.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Jan 28, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda kesho (Jumapili, Januari 29, 2012) atakutana na madaktari waliofanya mgomo kwenye ukumbi wa Karimjee kuanzia saa 4:00 asubuhi.

  Madaktari hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wanaomba kuonana na Waziri Mkuu na mara zote Waziri Mkuu amekubali kuonana nao lakini hawakutokea. Pamoja na kukubali huko kwa Waziri Mkuu, tarehe 25 Januari 2012 katika Mkutano wake na Wahariri wa Vyombo vya Habari aliwaomba Madaktari kuwa alikuwa tayari kuonana nao lakini hawakutokea.

  Ili kuendeleza jitihada za kutaka kuonana na madaktari hao, Waziri Mkuu alituma Uongozi wa Serikali ukiongozwa na Mawaziri wa Afya na Ustawi wa Jamii; na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kuonana na Madaktari kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Starlight tarehe 27 Januari 2012. Kwenye Mkutano huo madaktari waliwasilisha malalamiko yao na kuomba kuonana na Waziri Mkuu. Kufuatia maombi hayo, Waziri Mkuu amewaandikia madaktari hao barua ya kuwataka kuonana nao Kesho, tarehe 29 Januari 2012 kwenye Ukumbi wa Karimjee, saa 4:00 asubuhi.

  Kabla ya kufikia uamuzi huo, kulikuwa na mawasiliano kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Uongozi wa Medical Association of Tanzania (MAT) na baadaye Mwenyekiti wa Muda wa Kamati ya Madaktari kuhusu mgomo wa Madaktari unaoendelea.

  Aidha, Viongozi mbalimbali wa Serikali wamefanya mazungumzo na Wawakilishi wa Madaktari na Madaktari wenyewe kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Starlight ili kuweza kupata ufumbuzi wa matatizo yaliyowasilishwa Ofisi ya Waziri Mkuu.

  Waziri Mkuu anawasihi Madaktari wote kuhudhuria mkutano.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YAWAZIRI MKUU
  SLP 3021,
  DAR ES SALAAM
  JUMAMOSI, JANUARI 28, 2012
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  sasa siku zote hizo alikua anajivutavuta nini mpaka ndugu zetu na watanzania wenzetu wamepoteza maisha?
   
 3. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,187
  Likes Received: 1,189
  Trophy Points: 280
  Anaenda kuwalilia!
   
 4. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Kwa kauli aliyotoa kuhusu posho za wabunge tar 25, huyu naye ni sehemu ya tatizo la madaktari. Sioni ni vipi anaweza kuja na suluhisho.
   
 5. yegella

  yegella JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Baada ya kutikisa kiberiti na kukuta kimejaa ameamua kuwafata....hahaha au alifikili akina Mgaya
   
 6. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  dah! Ndugu zangu habari hizi vp tena? Makubaliano kwenye kikao leo ni kukutana j3, walikuwa wapi muda wote?
   
 7. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #7
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Shukrani kwa taarifa kiongozi.
   
 8. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Madaktari wasikubali porojo zozote ambazo hazitalenga kutatua matatizo yao na ya jamii in general! Azungumze vitu black an white bila kumung'unya maneno. Wala asithubutu kulia pale ukumbini
   
 9. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2012
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,219
  Trophy Points: 280
  Mimi linaloniuma ni wagonjwa kulala chini,tusubiri kesho PM atatoa majibu gani
   
 10. Atukilia

  Atukilia JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 643
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kesho msipotokea watasema mmeingia mitini tena.
   
 11. k

  kuzou JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  inaonekana hutaki muafaka na unaomba waziri mkuu asifanikiwe mgomo uendelee,kuna watu na viatu duniani
   
 12. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  asante kwa taarifa tulidhani serikali haipo hadi Rais arudi
   
 13. P

  Pax JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Wasipokubali unafikiri ni nini kitafuata? amini usiamini, PM atawaambia serikali itayafanyia kazi madai yao, sioni jibu la tofauti. Madai mengi ni ya kisera zaidi na yanahusu na watumishi wengine pia. Huwezi kuongeza mishahara kiholela bila kuamsha madai kwingine. Mimi ningewashauri wakubaliane naye kuwa baada ya miezi 4-6 wanatarajia kuona utofauti katika yale wanayodai. Migomo ni migumu kuisustain kwa sababu ya tofauti nyingi zilizopo kati ya wagomaji, kuna wengine kati ya madaktari wameshachoka sasa wanatamani tu kurudi kazini, kuna wengine bado ari iko juu. Subiri uone baada ya kesho watakavyogawanyika.

  Wakimkatalia PM tu wataambiwa wanaokubaliana na serikali warudi kazini wasiokubali waendelee kugoma. Waziri mkuu ndio serikali yenyewe na wanatakiwa walitambue hilo. Wakipewa option hizo mbili mgomo ndio umekwisha hivyo. Wawe wastaarabu na kukubaliana deal fulani na PM then waendelee kufuatilia kwa ukaribu, kama Ulimboka unasoma hii msg nafikiri utanielewa what to do. PM hawezi kumfukuza waziri au secretary wa wizara kienyeji enyeji, lazima wamlinde na kumuondoa ili kuondoa taswira ya kushinikizwa. Ni hilo tu.
   
 14. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Ataishia kumwanga chozi tu!
  Maana kuongeza mafao kwa ss ni ngumu, mishahara ya January imelipwa nusunusu!
   
 15. S

  SirBonge JF-Expert Member

  #15
  Jan 28, 2012
  Joined: Jul 18, 2010
  Messages: 349
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 60
   
 16. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #16
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  pinda ana nini huyo....?ni mmoja wa watu walioshidhwa kutekeleza wajibu wake.yupo yupo tu......
   
 17. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Pax, maelezo yako yana hisia ndiyo, lakini hayo unayoyasema ndiyo siasa halisi za Tanzania na Afrika ambazo matokeo yake ndiyo nchi ipo hapa ilipo. Haya madai ya madaktari ambayo mengi yanalenga kuboresha mazingira ya wagonjwa hayajaanza juzi, serikali inajua fika wajibu wake lakini inapuuzia kwa makusudi. Huwezi kuharibu halafu ukatatua tatizo kwa mabavu.
   
 18. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #18
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,595
  Likes Received: 5,775
  Trophy Points: 280
  Mi nawaambia subirini kesho jamani mtashangaa
   
 19. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  wizara ya afya ifumuliwe hilo ni dai la kwanza na dai muhimu
   
 20. P

  Pax JF-Expert Member

  #20
  Jan 28, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Massenberg sisi tuna viongozi wabovu kupita hata watu wanavyoelewa, kuboresha mazingira ya kazi ni vitu basic kabisa vinavyotakiwa vifanywe kila mwaka na serikali. Haingii akilini ati mtu akeshe usiku kucha umlipe buku 10, huu ni usanii uliopitiliza mipaka. Nategemea jambo hili PM kama atatumia hekima alitolee uamuzi wa papo kwa papo, angalau kiasi cha chini kabisa kisipungue nusu ya per diem = 40,000. Hayo mengine nafikiri wangekubaliana kuwe na team ya kuyafanyia kazi, baada ya miezi kama 4 hivi kuwe na mkutano wa madktari wapewe feedback, kama kuna usanii unaendelea wanagoma tena.
   
Loading...