Waziri Mkuu hana mamlaka juu ya shughuli za Ofisi ya DPP

Pulchra Animo

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
2,391
2,000
Katika gazeti la Raia Mwema la leo, Jumatano, August 18, 2021, kuna habari kwamba Waziri Mkuu, Majaliwa, amewapa TAKUKURU na DPP siku nne kuwafikisha mahakamani watuhumiwa fulani wa ufisadi. Haya maagizo sio tu ni ya kushangaza, lakini pia ni ushahidi kwamba nchi yetu ina viongozi ambao hawajui mipaka ya kazi zao.

Ofisi ya DPP ipo kikatiba na ni ofisi ambayo inapaswa kufanya kazi zake bila kushinikizwa na kinyamkera yeyote yule. Charging decision ni prosecutorial discretion ya DPP. Akijiridhisha kwamba kuna ushahidi wa kutosha dhidi ya mtuhumiwa, DPP atapeleka kesi mahakamani. Vinginevyo hapeleki. Hapapaswi kuwa na mtu yeyote wa kumuagiza kufanya hiki au kutokufanya kile. Not even the President.

Wanasiasa, tafadhali sana fahamuni mipaka ya authorities zenu. Mnatia aibu
 
Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
13,071
2,000
Ana uwezo wa kuagiza lakini wao wakafuata taratibu zote.

Lakini haimaanishi akisema basi hapohapo wanakamata watu.

Hivyo TAKUKURU watachunguza na DPP ataangalia kama kuna ushahidi na kama upo hao wezi watashughulikiwa.

Kama hakuna basi ndo sie huona ukimya na case closed.
 
Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
4,340
2,000
Waziri mkuu anawajibika kwa raisi tu ndani ya Tanzania watendaji wote serikalini yeye ndio boss wao kila taasisi ya serikali unayoijua wewe Majaliwa ndio boss wao; anaweza kumpa amri hata IGP Sirro akiamua.

Waziri yoyote anamwakilisha raisi moja kwa moja kwenye sector aliyokabidhiwa, kauli yake ndio ya raisi; unless raisi mwenyewe aikane.

Unashangaa kuona watu kama hakina Sirro wanapata wapi kiburi cha kujibizana na mamlaka ya raisi.

Unapomletea ukaidi waziri ni kukaidi amri ya raisi mpaka raisi mwenyewe aipinge.
 
Joseph lebai

JF-Expert Member
Jul 19, 2017
6,638
2,000
Katika mambo ya serikali hizo ofisi zinahusika? Kama ndio, waziri mkuu ndio msimamimizi wa shughuli zote za serikali.
 
issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,619
2,000
Ana uwezo wa kuagiza lakini wao wakafuata taratibu zote.

Lakini haimaanishi akisema basi hapohapo wanakamata watu.

Hivyo TAKUKURU watachunguza na DPP ataangalia kama kuna ushahidi na kama upo hao wezi watashughulikiwa.

Kama hakuna basi ndo sie huona ukimya na case closed.
Unaelewa maana ya hii sentensi "waziri Mkuu amewapa takukuru/ofisi ya DPP siku nne wawe wamewafikisha watuhumiwa mahakamani"?
 
wa kupuliza

JF-Expert Member
Jun 15, 2012
8,806
2,000
Waziri mkuu anawajibika kwa raisi tu ndani ya Tanzania watendaji wote serikalini yeye ndio boss wao kila taasisi ya serikali unayoijua wewe Majaliwa ndio boss wao; anaweza kumpa amri hata IGP Sirro akiamua.

Waziri yoyote anamwakilisha raisi moja kwa moja kwenye sector aliyokabidhiwa, kauli yake ndio ya raisi; unless raisi mwenyewe aikane.

Unashangaa kuona watu kama hakina Sirro wanapata wapi kiburi cha kujibizana na mamlaka ya raisi.

Unapomletea ukaidi waziri ni kukaidi amri ya raisi mpaka raisi mwenyewe aipinge.
Makonda alimdindia Waziri mkuu na Majaliwa cha kumfanya akashindwa.
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
37,283
2,000
Huu uzi wako sio tu ni wa kushangaza, lakini pia ni ushahidi kwamba huijui nchi yako.Hadi leo hujui ya kwamba katika nchi ya Tanzania viongozi wa kisiasa huwa wanaiweka mihimili ya nchi mfukoni mwao kwa faida zao binafsi?Kwa nini unashangaa kitu ambacho ni cha kawaida Tanzania na kinajulikana?

Hili suala la Watanzania walio wengi kuwa na akili ndogo za kufikiri kama za mleta uzi huwa linanikera sana!
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
24,622
2,000
Katika gazeti la Raia Mwema la leo, Jumatano, August 18, 2021, kuna habari kwamba Waziri Mkuu, Majaliwa, amewapa TAKUKURU na DPP siku nne kuwafikisha mahakamani watuhumiwa fulani wa ufisadi. Haya maagizo sio tu ni ya kushangaza, lakini pia ni ushahidi kwamba nchi yetu ina viongozi ambao hawajui mipaka ya kazi zao.

Ofisi ya DPP ipo kikatiba na ni ofisi ambayo inapaswa kufanya kazi zake bila kushinikizwa na kinyamkera yeyote yule. Charging decision ni prosecutorial discretion ya DPP. Akijiridhisha kwamba kuna ushahidi wa kutosha dhidi ya mtuhumiwa, DPP atapeleka kesi mahakamani. Vinginevyo hapeleki. Hapapaswi kuwa na mtu yeyote wa kumuagiza kufanya hiki au kutokufanya kile. Not even the President.

Wanasiasa, tafadhali sana fahamuni mipaka ya authorities zenu. Mnatia aibu

..kwa hapa Tanzania katiba haifuatwi, kinachofuatwa ni amri za viongozi wa CCM.
 
PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
17,228
2,000
Katika gazeti la Raia Mwema la leo, Jumatano, August 18, 2021, kuna habari kwamba Waziri Mkuu, Majaliwa, amewapa TAKUKURU na DPP siku nne kuwafikisha mahakamani watuhumiwa fulani wa ufisadi. Haya maagizo sio tu ni ya kushangaza, lakini pia ni ushahidi kwamba nchi yetu ina viongozi ambao hawajui mipaka ya kazi zao.

Ofisi ya DPP ipo kikatiba na ni ofisi ambayo inapaswa kufanya kazi zake bila kushinikizwa na kinyamkera yeyote yule. Charging decision ni prosecutorial discretion ya DPP. Akijiridhisha kwamba kuna ushahidi wa kutosha dhidi ya mtuhumiwa, DPP atapeleka kesi mahakamani. Vinginevyo hapeleki. Hapapaswi kuwa na mtu yeyote wa kumuagiza kufanya hiki au kutokufanya kile. Not even the President.

Wanasiasa, tafadhali sana fahamuni mipaka ya authorities zenu. Mnatia aibu
Hata rais hana mamlaka ya kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya siasa.

Except kwenye cases za state of emergency na public safety. Ndipo anapoweza kutumia mamlaka yake kususpend some constitutional rights
 
PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
17,228
2,000
Waziri mkuu anawajibika kwa raisi tu ndani ya Tanzania watendaji wote serikalini yeye ndio boss wao kila taasisi ya serikali unayoijua wewe Majaliwa ndio boss wao; anaweza kumpa amri hata IGP Sirro akiamua.

Waziri yoyote anamwakilisha raisi moja kwa moja kwenye sector aliyokabidhiwa, kauli yake ndio ya raisi; unless raisi mwenyewe aikane.

Unashangaa kuona watu kama hakina Sirro wanapata wapi kiburi cha kujibizana na mamlaka ya raisi.

Unapomletea ukaidi waziri ni kukaidi amri ya raisi mpaka raisi mwenyewe aipinge.
Unauelewa kidogo wa katiba na utawala?
 
Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
496
1,000
Huu uzi wako sio tu ni wa kushangaza, lakini pia ni ushahidi kwamba huijui nchi yako.Hadi leo hujui ya kwamba katika nchi ya Tanzania viongozi wa kisiasa huwa wanaiweka mihimili ya nchi mfukoni mwao kwa faida zao binafsi?Kwa nini unashangaa kitu ambacho ni cha kawaida Tanzania na kinajulikana?

Hili suala la Watanzania walio wengi kuwa na akili ndogo za kufikiri kama za mleta uzi huwa linanikera sana!
Acha upuuzi wa kuwadharau watu usiowajua wewe tambala la deki,huu Uzi unashida gani?? Mbona hii platform imejaa matahira wengi Sana?! Kuna haja gani ya kuchangia kila thread tena kwa kuwadharau wenzenu??
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom