Waziri Mkuu arejesha tena usafiri wa "Mchomoko" Simiyu

KwetuKwanza

Member
Mar 13, 2023
35
82
Sasa ni rasmi ile biashara ya Magari madogo kubeba abiria katika mkoa wa Simiyu maarufu kama Mchomoko, imereja rasmi baada ya tarkibani miezi tisa tangu yazuiliwe kufanya kazi hiyo ndani ya mkoa huo.

Hiki ni kicheko na furaha kubwa kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu hasa vijana ambao walikuwa wamejiajiri kupitia shughuli hiyo ya ujaslimali.

Jana Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akaondoa zuio hilo, wakati akizungumza na mamia ya wananchi hasa vijana wa Mkoa wa Simiyu katika eneo la Barabara ya Mzunguko Mjini Bariadi.

Waziri mkuu jana ameondoa zuio hilo, lakini akawataka madereva wa magari hayo kuzingatia sheria, kubeba abiria wanaotakiwa, kuendesha kwa mwendo unaotakiwa na kuzingatia sheria zote za usalama Barabarani.

Kubwa Zaidi Waziri Mkuu akawaonya viongozi wa serikali ngazi zote ndani ya Mkoa, kuacha tabia ya kupenda kufunga Biashara za wajaslimali, kwani ndiyo ajira zao na wanajipatia kipato halali.

Sasa Magari hayo yatasajiliwa na LATRA kama ambavyo Waziri Mkuu ameagiza jana, lakini wasizuiwe kufanya biashara zao za kwenda sehemu yeyote muhimu wazingatia masharti na sheria zote za usalama Barabarani.
 
Mwana kulitafuta.
Nani asiye jua kwamba madereva wa michonoko sio watu makini?
Nani asiyejua michomoko hua inajaza watu kupindukia?
Nani asiyejua michomoko inabeba mizigo kupindukia.
 
Usalama uzingatiwe kuanzia ngazi za juu!! Sio kuwalaumu polisi walikuwa wapi
 
Mwana kulitafuta.
Nani asiye jua kwamba madereva wa michonoko sio watu makini?
Nani asiyejua michomoko hua inajaza watu kupindukia?
Nani asiyejua michomoko inabeba mizigo kupindukia.
Kwahiyo ufumbuzi wa hayo mambo ndo kuyafungia?.Mbona ni mambo madogo sana yakuweka tu utaratibu wa sheria na usimamizi.
 
Yuko sahihi kule hutumia baiskeli wilaya hadi wilaya .simchezo msishangae wakipakia trey za mayai dar
 
Back
Top Bottom