Waziri Mkuu apitisha chekeche kwa wakurugenzi wa halmashauri

Mimi bado najiuliza uteuzi wa Wakurugenzi na Wakuu wa idara katika Halmashauri zetu unazingatia vigezo gani? Kufahamiana, utendaji, elimu, utumishi wa mda mrefu au ni nini?

Katika kuangalia sijapata vigezo vinavyotumika labda wadau wasaidie kutoa somo hapa.

Natanguliza shukrani

.......wengi wao wananunua vyeo hivyo, na wanajulikana..........kama wale wawili walioteuliwa kutoka MUFINDI DC, ni pesa tu maana utendaji wao hata kwa madiwani wao ulikuwa wa mashaka......inapendeza lakini kama fedha ndio kigezo........tusubiri yatakayo wakuta huko.

Naona kuna mtu katolewa kwenye u Chief Internal Audit - CIA ofisi ya Mwanasherika Mkuu wa Serikali na kupelekwa kuwa DED Mbarali. Huyu nae kafanyiwa demotion bila ya yeye kujua. Maana huwezi kuwa Mkaguzi Mkuu wa ndani wa kazi zote za Mwanasheria Mkuu wa Serikali zinazofanyika nchi nzima baadae ukateuliwa kuwa Accounting Officer wa Halmashauri ukasema ni Horizontal Transfer! Sasa hivi anaendea kujibu hoja za Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali na zile za CAG. Siwezi kumpongeza zaidi ya kumpa pole na kumtakia kazi njema..

TUMBIRI (PhD in Proges at HULL, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd[/SUP] Overall Best Student in Form six National Exams),

tumbiri@jamiiforums.com
 
kwanini wanateua makaimu tena ???

Mkuu Duble Chris,
Vyeo vyote vya ukurugenzi ndivyo vilivyo serikalini. Unapoteuliwa lazima ukaimu kwanza huku wakiendelea kukumonitor (Probation) kama unamanage hiyo position nadhani for a period of three years. Baada ya hapo wakiridhika na utendaji wako wanakudhibitisha rasmi.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu Duble Chris,
Vyeo vyote vya ukurugenzi ndivyo vilivyo serikalini.
Unapoteuliwa lazima ukaimu kwanza huku wakiendelea kukumonitor (Probation) kama unamanage hiyo position nadhani for a period of three years. Baada ya hapo wakiridhika na utendaji wako wanakudhibitisha rasmi.

Hapo kwenye nyekundu, SIYO KWELI Tumbili. Huu mtindo wa Waziri mkuu/TAMISEMI kuteua KAIMU umeanza this time. Awali, kama nafasi ipo wazi Halmashauri/ baraza la madiwani ndio waliokuwa na jukumu la kuteua kaimu. Mkurugenzi anapendekeza jina/majina ya wakuu wa Idara na BARAZA LA MADIWANI wanaridhia mojawapo. Angalia vizuri katika orodha iliyoletwa na utaona kuwa wengi tu wametoka katika ukuu wa Idara kama DHRO, DPLO, DEO au Afisa Ardhi na wameteuliwa moja kwa moja kuwa Wakurugenzi na most of them mimi nawafahamu. Walikuwa wanakaimu mara moja moja tu labda pale Mkurugenzi amesafiri na siyo kukaimu officially
 
Last edited by a moderator:
TUMBIRI (PhD in Proges at HULL, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd[/SUP] Overall Best Student in Form six National Exams),
Samahani TUMBIRI kwa kuku challenge, nilikuwa sijaisoma CV yako. Mimi nina CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), ECA (SHYCOM) tu + Nine years experience in LGAs
 
Last edited by a moderator:
Mimi bado najiuliza uteuzi wa Wakurugenzi na Wakuu wa idara katika Halmashauri zetu unazingatia vigezo gani? Kufahamiana, utendaji, elimu, utumishi wa mda mrefu au ni nini?

Katika kuangalia sijapata vigezo vinavyotumika labda wadau wasaidie kutoa somo hapa.

Natanguliza shukrani

Hakuna objective criteria inayotumika kuwateua hawa jamaa; ukaribu wake na waziri wa Tamisemi na pia Ukaribu na waziri Mkuu ni deciding factors!!
 
Mh Pinda tembelea na Ofiisi ya mkurugenzi wa Mvomero ujionee alivyojipatia mafedha ya serikali bure bure. Mbopna huyu hamumgusi jamani????? Huyu ni balaa zaidi kuliko hata Harold Senyagwa wa Kyela na hata yule fisadi mdogo wa Geita. Baba tuondolee na huyu,wamejikodisha usafiri wa watumishi kifisadi tupu km 60 kwa siku gali inalaza laki 3 wapi na wapi?jengo lake mil 400 na bado halijaisha na haijulikani lini litaisha? Pesa na mfuko wa jimbo yeye na mbunge wamezimaliza mwaka 2010 ...75m,2011 ....85m na mwaka 2012 hadi juni mil 105. wananchi wameambulia pikipiki 7 na mipira na jezi.
 
tupeni sababu za kutosha wakurugenzi ni viungo katika halmashauri zetu ,wapo kiutendaji na kisiasa pia
 
kuna wakati tulikuwa tunabadilisha makampuni ya ulinzi ofisini kwetu kila wakati sababu ya wizi ....kumbe bwana mwizi tunaye miongoni mwetu hapo ofisini siku tulipo mgunduwa aaaa mambo safi hata ukiacha simu nje kesho mlinzi anakwambia bosi simu yako hii hapa ilusahau .

Nasema hivi watabadilisha sana kila mtu kila mkoa kila wizara si mmeona wameshabadilishwa mawaziri wangapi .......lakini mambo yatakuwa yale yale mpaka ccm itoke au pinda na anna na jk watoke wao ndio hawafai kabisaaaaaa
 
Mkuu Duble Chris,
Vyeo vyote vya ukurugenzi ndivyo vilivyo serikalini. Unapoteuliwa lazima ukaimu kwanza huku wakiendelea kukumonitor (Probation) kama unamanage hiyo position nadhani for a period of three years. Baada ya hapo wakiridhika na utendaji wako wanakudhibitisha rasmi.
[/QUOTE
MKuu Probation kwenye promotion ni Miezi sita tu wakati kwenye ajira mpya ni miezi 12 (Mwaka mmoja) na sio miaka mitatu. Ingawa kwa uzembe wa Mamlaka za ajira mtu anaweza Kuwa Kaimu hata miaka Minne TUMBIRI
 
Last edited by a moderator:
juzi tumesikia katika vyombo vya habari mkurugenzi wa halmashauri ya wilya ya nzega anatuhuma za kifisadi na pia naibu waziri TAMISEMI MH MWANRI alitumwa huko kuchunguza vipi yeye hahusikina mabadiliko haya au hawa ndo wale wenye god father!!!!!????
 
Hapo kwenye nyekundu, SIYO KWELI Tumbili. Huu mtindo wa Waziri mkuu/TAMISEMI kuteua KAIMU umeanza this time. Awali, kama nafasi ipo wazi Halmashauri/ baraza la madiwani ndio waliokuwa na jukumu la kuteua kaimu. Mkurugenzi anapendekeza jina/majina ya wakuu wa Idara na BARAZA LA MADIWANI wanaridhia mojawapo. Angalia vizuri katika orodha iliyoletwa na utaona kuwa wengi tu wametoka katika ukuu wa Idara kama DHRO, DPLO, DEO au Afisa Ardhi na wameteuliwa moja kwa moja kuwa Wakurugenzi na most of them mimi nawafahamu. Walikuwa wanakaimu mara moja moja tu labda pale Mkurugenzi amesafiri na siyo kukaimu officially

Mkuu Polisi,
Labda kwa LGA's taratibu ndivyo ziko hivyo. Wakati natoa mchango wangu mind zangu zilikuwa zina assume kwamba taratibu za kwenye Serikali Kuu ndizo hizo zipo applicable hadi LGA's kumbe nimechanganya. Anyway lakini kwa serikali kuu utararibu ndiyo kama nilivyoeleza hapo awali. Pamoja!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom