Waziri Mbarawa: Tutajenga barabara ya njia 4, Dar-Moro, ili upite lazima ulipie

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame M. Mbarawa ametangaza mkakati wa ujenzi wa barabara mpya kwa kushirikiana na sekta binafsi kutoka Dar es Salaam – Chalinde hadi Morogoro yenye urefu wa Kilometa 215 itakayojulikana kwa jina la Express way.

Barabara hiyo itakuwa ni ya kulipia pindi mtu anapohitaji kuitumia na wale ambao hawataweza kulipia watalazimika kutumia barabara ya kawaida

“Tanzania hatuna express way tangu tumepata uhuru, haya ndio maendeleo, mfano kutoka Kibaha hadi Morogoro utakuwa unaenda kilometa 120 kwa saa na hauwezi kuingia tu, kutakuwa na maeneo maalum ya interchange ndiyo yatatumika kuingia.

“Itakapofika Aprili au Mei 2023 naamini tutakuwa tumempata mkandarasi ambaye atajenga kwa fedha zake mwenyewe kisha atakuwa anakusanya fedha mradi ukikamilika, magari madogo na makubwa yatakuwa na bei tofauti.

“Wenzetu Kenya wanayo, Uganda, njia yetu itakuwa na njia nne, mbili za kwenda na mbili za kurudi, itapunguza ajali kwa kuwa mtakuwa hamkutani kama iliyo sasa.”

Profesa Mbarawa ameongeza kwa kusema: “Serikali tunakuja na utaratibu mpya wa mtu anakuja na pesa yake anajenga mradi kisha Serikali tunamlipa.

“Pia tunakuna na mabadiliko ya Sheria ili turuhusu watu waendeshe mabehewa yao, TAZARA wameshaanza kufanya hilo jambo, TRC nasi tunataka kufanya hilo jambo."
 
Kodi tulipie na kupata huduma tunalipia hii nchi CCM wameshindwa kuingiza
Umeambiwa huo ni mradi wa mtu binafsi anapewa ajenge barabara sio mradi wa Serikali, atakachopata atakua anailipa Serikali, ulichotakiwa uiambie Serikali ijenge yenyewe kwa kutumia Kodi zetu kisha tupite free bila malipo yoyote km inavyotaka kufanya
 
Tunapo sema CCM mmeshindwa kuiongoza nchi hii MUWE MNATUELEWA ona Sasa Kodi zetu mchumue na ushuru mtutoze haya pro LUMUMBA mkowapi mje kusimamisha vijambio vyenu Huku
 
1km of tarmacadam(tarmac) = Tzs800mil - Tzs 1Bil..215km mpaka Moro mkandarasi awe na kiasi gani kumaliza hii project?

Cjui nani atapewa hii tender/contract!
 
Profesa Mbarawa ameongeza kwa kusema: “Serikali tunakuja na utaratibu mpya wa mtu anakuja na pesa yake anajenga mradi kisha Serikali tunamlipa.

“Pia tunakuna na mabadiliko ya Sheria ili turuhusu watu waendeshe mabehewa yao, TAZARA wameshaanza kufanya hilo jambo, TRC nasi tunataka kufanya hilo jambo."
Eti mkandarasi ajenge kisha serekali tunamlipa..................................ha ha ha

Si aseme tu mkandarasi ajenge kisha wananchi wanaotumia wanamlipa
 
Ajali zitapunguzwa kwa watu kufuata sheria za barabarani + plus kwanini zisiwe 4 kwenda 4 kurudi
 
Imekaa kifisadi. Kama akimaliza kujenga mnamlipa ina maana pesa ya kumlipa mnayo. Kama pesa mnayo kwanini msijenge wenyewe?

Serikali haiwezi kukwepa majukumu yake kwa visingizio vya kenya na uganda.
 
Imekaa kifisadi. Kama akimaliza kujenga mnamlipa ina maana pesa ya kumlipa mnayo. Kama pesa mnayo kwanini msijenge wenyewe?

Serikali haiwezi kukwepa majukumu yake kwa visingizio vya kenya na uganda.
Mzee apo amemaanisha kwamba kila gari itayo pita kwenye hizo barabara italipia na hiyo hela yote atachukua uyo mwekezaji atae tengeneza hio barabara iwe miaka kumi ata mia ni sawa
 
Acha ujinga wewe mbarawa, serikali kama itaacha kukusanya kodi basi hiyo miundombinu ya kulipia ni sahihi kuletwa kwa wananchi.
 
Kuna faida na kuna hasara. Ila kwa km 210 ni Kama bil 300 hivi. Bil 300 ni pesa ya kawaida tu kwa serikali.. ilibidi serikali ikope tujenge wenyewe ili wataolipia pesa iingie serikalini.

Mimi binafsi naona serikali inaweza kabisa kujenga na kukusanya pesa
 
Back
Top Bottom