Nadhani hapa katibu mkuu wa Waziri alikosa, huwezi kumzunguka boss wako. Kitendo cha Katibu mkuu wa waziri Masha kupata maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu kiongozi bila ya Masha kujua, ni sawa na kumzunguka.
Huyo Katibu Mkuu wa Waziri Masha anatakiwa ajieleze inakuwaje anawasiliana na Katibu Mkuu Kiongozi pasipo Waziri kuhusishwa? Na inakuwaje Katibu Mkuu Kiongozi amsikilize Katibu Mkuu wa Wizara bila kuhoji kama Waziri husika alikuwa awareness.
Something is wrong somewhere.
Thank you! Thank you!
So far naona kweli unastahili kujiita "special relativity."
Sikia Mkuu. Hiki kitu "Katibu ndio Mtendaji Mkuu" kinachanganya wengi, wengi sana. Ndio maana mwenyekiti mpya wa Umoja wa Wanawake anadiriki kusema "niko napanga jinsi ya kumsaidia Katibu kuendesha chama chetu."
Noooooo! Mwenyekiti/Waziri au Mkuu yeyote wa Idara hauwezi kusema utendaji ukuu ni wa Katibu Mkuu basi uweke miguu juu usiongoze wala usisimamie kazi wizara/chama/idara. No way Jose! Sehemu ya Waziri au Mwenyekiti kusimamia na kuongoza idara/chama chechote kile ni kujua what is happening under his nose at any given second!
Masha akimuuliza Katibu, hapa nini kinaendelea katika suala X, Y, Z katibu Mkuu hawezi kumwambia Masha "mimi bosi wangu yuko Ikulu...haya wewe hayakuhusu." Atakuwa amekataa "kufunikwa," kama alivyosema Fundi Mchundo, lakini mfumo huu utakuwa vurugu!
Na Luhanjo nae, kama ulivyosema Uwiano, hatakiwi ku get in between the Principal sectretary and his Minister! That's another flaw there.
Ndio maana Masha amekataa huu upuuzi, kwamba mambo ya wizara yake yaingiliwe na wakubwa wengine wa Ikulu wakati yamewekwa chini ya wizara yake. Kaona huu mradi ukiwa screw up wananchi hawatakuwa na muda wa kusoma Government Procurement Act kutafuta mchawi. Mambo ya wizara ya Mambo ya Ndani mwisho wa siku anaulizwa Masha!
Kama kweli habari alizoleta huyu Kinvaba ni za kweli, basi aidha Luhanjo ndio anaoneka alitaka kuingilia hapa, maana na yeye hatakiwi kuwemo katika mchakato. Au nawezekana Masha alitaka kufanya ufisadi, ndio, lakini naona mfumo wenyewe ovyo. Hata mimi nisingekubali upuuzi wa kupewa mzigo, sifa na lawama za uwaziri halafu wajuba wengine ndio wanaamua mambo ya wizara.