Waziri Masha ajikanganya?

Ushirombo, Heshima mbele,

Kwa hiyo unataka kumfananisha Masha na Obama? Hivi Masha alishawahi hata kushiriki katika kazi na uongozi wa Kijamii zaidi ya kuwa na law firm yenye Ukungu wa EPA? Ninadiriki kusema Masha hana uzoefu wa kuongoza umma,

Naomba kutokukubaliana

Masha hawezi kuwa sawa na Obama, suala hapa kule kulinganisha kuboronga kwake kwa kigezo cha umri. Nadhani ni vizuri kuweka wazi Masha (41) amelewa madaraka na hajui afanyalo kuliko kutizama kwenye umri, kuna walio wadogo zaidi zake yake lakini wanafanya vizuri.
 
Ushirombo, Heshima mbele,

Kwa hiyo unataka kumfananisha Masha na Obama? Hivi Masha alishawahi hata kushiriki katika kazi na uongozi wa Kijamii zaidi ya kuwa na law firm yenye Ukungu wa EPA? Ninadiriki kusema Masha hana uzoefu wa kuongoza umma,

Naomba kutokukubaliana

Swadakta shadow,
Waziri masha hajawahi kuongoza hata mtaa. Aliwahi kuongoza TOL akaishia kuipeleka shimoni.Hana historia yoyote ya kufanya kazi za kijamii.Waziri masha ana historia ya kuongoza kampuni yake ya IMMA kushiriki wizi wa fedha za EPA. Masha ana historia ya kupindisha taratibu na kukiuka sheria, mfano hai unaokumbukwa na wengi ni jinsi alivyoweza kuingia UDSM bila kupitia JKT kama walivyofanya wenzake na bado hajawahi kujitokeza kuuelezea umma wa watanzania ilikuwaje akakiuka utaratibu huo wa kupitia JKT kabla ya kuingia UDSM. Mimi namuona masha alikurupuka au alitaka kutumia madaraka yake vibaya au alitaka kukiuka sheria kwakuwa ana historia ya kwea kinyume na sheria kutaka kumfumba mdomo mzee mengi. hata kama mzee mengi ana mabaya/mapungufu yake sipingani na hilo lakini katika hii issue ya yeye dhidi ya waziri kijana masha alikuwa sahihi ndo maana alitunisha msuli na hatimaye masha kaamua kuwa mpole.Kwahiyo masha
hawezi kufananishwa kwa jambo lolote lile na Obama.full stop!!!
Halafu huku uswazi inasemekana waziri kijana aliye-propose kuwa mengi afilisiwe ni naibu waziri kijana asiye na adabu kwa wakubwa zake Adam Kighoma Ally Malima, je kuna mwenye ukweli na hizi tetesi?Inasemekana tangia walipokwaruzana nae hadi kupelekea spika kuunda tume iliyotafuna milioni 100 na kubaini kuwaAdam aliliongopea bunge, basi kijana amekuwa nunda kuanzia kwa spika hadi kwa waheshimiwa wengine!!!
 
Ndiyo mana huwa simpendi Mengi na nitasimamia hapo hapo...Mzee huyu anajidai ni msaada kwa watanzania ila hana chochote

Sisi wakristo tunaongozwa na Amri kumi za Mungu na kuna amei moja inayosema Mpende Jirani yako Kama Nafsi yako Pia tunaambiwa tuwapende adui zetu na kuwaombea ka MUNGU........ Kaka GEMBE pole sana nakuonea huruma maana umeshindwa kuendana na haya anayoyataka MUNGU
 
Ndiyo mana huwa simpendi Mengi na nitasimamia hapo hapo...Mzee huyu anajidai ni msaada kwa watanzania ila hana chochote

Kwa swala la kusimamia hapo hapo nakemea kwa JINA LA YESU ubadilike na uwe na upendo kwa wenzako: kwa swala la kuwa msaada kwa watanzania inamaana wewe huoni msaada unaotolewa na Mengi?? Hivi wewe ulishawahi kufuatwa ukaambiwa unadaiwa bills kwa kuangalia Television stations zake?? Je angefuata mfumo wa GTV na DSTV wanyonge wangeweza kujua nini kinaendelea nchini mwao na hata duniani kote?? watu wanaangalia aljazeera na cnn bure through ITV ukienda GTV au DSTV ni pesa ambayo mnyonge hawezi kuimudu sasa huu si msaada tosha??

GEMBE usifiche hekima yako ficha upumbavu wako mkuu
 
Naam hapa siongezi kitu maana umesema yote!!!!!!
 
Haya ndiyo yalikuwa madai ya Mengi:

images

Hivi karibuni waziri mmoja kijana anayeongoza wizara nyeti alipendekeza nibambikiziwe kodi bandia ya kiasi kikubwa nitakachoshindwa kulipa na hatimaye nifilisiwe kama njia pekee ya kuninyamazisha kabisa eti kama alivyofilisiwa tajiri mmoja mkubwa huko Urusi.

Alidai kwamba vyombo vyangu vya habari vimekuwa mno mstari wa mbele kupiga vita ufisadi, jambo ambalo kwa maoni yake siyo zuri kwa sababu linawanyanyasa baadhi ya watu.

Haya ndiyo yalikuwa majibu ya Masha:
455010.jpg

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, amempa siku saba Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, kuthibitisha madai ya kutishiwa kuuawa na suala kwamba kuna waziri anayepanga kumfilisi.

Pia amesema kuwa madai hayo ya Mengi ni mazito na umefika wakati ayathibitishe tuhuma hizo. "Leo hii nitamwandikia ingawa mpaka sasa sijamwandikia barua, ili ndani ya siku saba kuanzia leo (juzi) awe amethibitisha," alisema Masha.

Ufuatao ulikuwa ni msimamo wa baadhi ya wana JF:

Hivi ni nani aliyeanzisha uzushi huu? ..Nadhani ni Mengi... Awe mwanaume and see it to the end... He cannot just use his media outlets to trump up allegations na kukimbia? Let him substantiate his claims and see it to the end...Sheria lazima ichukue mkondo wake na Mengi hawezi kuachiwa hivi hivi kuiyumbisha serikali.

Kaazi kweli kweli. We have a long way to go.
 
Last edited:
Ushirombo, Heshima mbele,

Kwa hiyo unataka kumfananisha Masha na Obama? Hivi Masha alishawahi hata kushiriki katika kazi na uongozi wa Kijamii zaidi ya kuwa na law firm yenye Ukungu wa EPA? Ninadiriki kusema Masha hana uzoefu wa kuongoza umma,

Naomba kutokukubaliana

Sidhani kama Ushirombo alimaanisha kumfananisha Obama na Masha bali nadhani pointi yake ilikuwa ni hoja kuwa vijana hawafai kwasababu ya Masha haina mantiki...Kuna vijana wengi sana tu wenye hekima na busara na wenye kufanya maamuzi inavyotakiwa.
Naomba uelewe pia kuwa nafasi hiyo wa uwaziri wa mambo ya ndani aliteuliwa na hakuchaguliwa,similarity moja na Obama ni kwamba wote walichaguliwa kutoka majmboni mwao kuingia bungeni/senete,ila kwenye uongozi wao wa serikali ni tofauti sana mmoja ni rais aliyechaguliwa na wananchi na mwingine ni waziri wa mambo ya ndani aliyeteuliwa na rais.
 
Naam hapa siongezi kitu maana umesema yote!!!!!!

Unajua kuna wakulu wengine wanaamuaga kukurupuka kuandika mambo mengine ambayo hayana msingi sijui ili waweze kuongeza idadi ya post zao?? Hapa tunahitaji kuitetea jamii na kujitahidi kuwaelekeza hawa wenzetu ambao ni viongozi waweze kuiweka nchi kwenye mstari ulionyooka si mahala pa kuja kusema mauza uza yako kuwa simpendi huyu nampenda huyu inatusaidia nini sisi?? mwaga points za maana watu tutakuwa na wewe ukurasa mmoja lakini si kubwabwaja tu pasipo na sababu za msingi
 
Mkuu Waga msamehe tu bwana Gembe , naamini ameteleza katika kutoa lile lililo moyoni mwake na kulianika ili dunia nzima ijue.Sisi wengine tushamsamehe na tunaamini si msimamo unaoweza kumsaidia wala kumpevusha kimawazo.Hapa JF kunakuelimishana,kupashana, kuyooshana na hatimaye kama mchango ni mswano kabisa kupongezana kwa faida ya wengine wote.
 
Sidhani kama Ushirombo alimaanisha kumfananisha Obama na Masha bali nadhani pointi yake ilikuwa ni hoja kuwa vijana hawafai kwasababu ya Masha haina mantiki...Kuna vijana wengi sana tu wenye hekima na busara na wenye kufanya maamuzi inavyotakiwa.
Naomba uelewe pia kuwa nafasi hiyo wa uwaziri wa mambo ya ndani aliteuliwa na hakuchaguliwa,similarity moja na Obama ni kwamba wote walichaguliwa kutoka majmboni mwao kuingia bungeni/senete,ila kwenye uongozi wao wa serikali ni tofauti sana mmoja ni rais aliyechaguliwa na wananchi na mwingine ni waziri wa mambo ya ndani aliyeteuliwa na rais.

Mkuu JMushi, Heshima Mbele,

Natumaini kama umetizama vizuri sulala nililogusia ni kuhusu uzoefu kati ya wawili hao na hitimisho languni kuwa Masha hana uzoefu. Uzoefu alionao Obama katika kuongoza jamii, Masha hawezi kuhufikia. If I were JK then Masha ningempa kazi ya Kusimamia Masuala ya sheria za CCM na si kingine.
 
Ndugu yangu kumdhuru kivipi? Yani akitokea mtu mwenye msimamo dhidi ya haki za wananchi kutozingatiwa basi yeye ndiyo wenye uwezo wa kumdhuru mwezie? Nani alikuwa amdhuru nani? Nadhani madhara uliyoyazungumzia inawezekana(correct me if iam wrong) ni ya kisiasa ama kisheria,ila madai kuwa mchagga Mengi si rahisi kumdhuru Masha kwasababu kaoa uchaggani....

- Nafikiri kabla hujakurupuka na hii nyepesi, ulitakiwa kujiuliza kwanza nani aliyejitokeza to the public kwanza, kabla ya mwingine, au? Maana nitasema je kua Masha atamdhuru Mengi wakati aliyeanza kushitaki kwetu public ni Mengi?

Then kwanini hukuangalia upande wa pili wa shilingi na kusema Masha hawezi kumdhuru Mengi kwasababu kaoa uchaggani? Kwanini hukusema Masha ama mke wake watapita wapi kama wakimfilisi Mengi kwa njama?

- Mkulu wangu Mushi vipi leo mbona nilishaanza kukuaminia, hivi unajua toka nimuoe mke wangu sijawahi kufika kwao na ninaendelea na maisha kama kawa na huenda nisije kufika kabisa huko kwao, sasa eti unasema kuwa Mengi anaweza ku-afford kukosa kwenda kwao kwa sababu ya Masha na this nonesense? Vipi ndugu yangu yaani umeshindwa hata kuona ishus muhimu za taifa kwenye this sagga kama kutoheshimika kwa sheria na wenye nguvu wawili wasiojua mipaka ya nguvu zao!

Naelewa umekuwa dissapointed mkuu lakini still naomba ubalance ili kuweza kuleta mantiki ya haki na sense kimjadala bila unnecessary biasiness.

- What a joke! nimekua dissappointed off course yes kwa sababu nilitegemea this drama itaenda kwenye sheria ili kuweka muongozo wa sheria kwa the future generation kuhusu mipaka ya utanuaji kwa viongozi na matajiri katika taifa letu, sihitaji balance kwenye kuwa na haya mawazo, na ninaamini betweeen maneno yangu na yako hapa kwenye this thread sio taabu ku-read betweeen the lines hoja za nani kati yangu na wewe zina matatizo ya balance na bias.

Have a nice day mkuu, next time jifunze kusoma betweeen the lines kinachosemwa, kabla ya kukurupuka!
 
Mkjj nimeipenda hiyo,timu zote za mpira hazikuingia uwanjani hivyo mashabiki na watazamaji turudi majumbani lakini je umesahau kua TUMELIPA KIINGILIO?
Je kiingilio chetu inakuaje?
 
Tanzania Daima (Leo)
http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=1507http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=1507Masha amuota Mengi (Read full story on this link)
• Asema wangali wanafuatilia madai yake
..... Hata hivyo, alipobanwa zaidi na kuulizwa kwanini amri yake ya awali ameigeuza kuwa ombi na kushindwa kuchukua hatua dhidi ya Mengi licha ya siku saba alizomuamuru kupita.

“Kwanza naomba unielewe, nilitoa siku saba kwa Mengi kuwasilisha ushahidi wake lakini sikutoa siku saba kwa serikali kushughulikia suala hili. Serikali haijipi siku saba kwa lolote. Suala hili halijaisha. Sijaletewa ushahidi na Mengi lakini serikali ina vyombo na idara zake nyingi za kufanya uchunguzi,” alisema Masha.....

Kazi kweli kweli!
 
Last edited:

alikurupuka wajameni, mtu mzima haombi samahani ahadharani, inawezekana keshamuita mzee Mengi mwenyewe akasema mzee haya mambo inabidi yaishe, kumbukeni na sakata hili la ufisadi wahisani wanatoa hela kwa kupima na kujiko sio kumwaga tu mpaka zibaki BOT waziEPE, kwa hiyo CCM 2010 watahitaji matangazo ya offer au wapunguziwe matangazo ya kampeni tehetehe wakimpoteza Mengi watabaki na TBC1 tu wajameni,Mzee Mengi hivi hamsikii anavyomsifia kikwete kwenye kila hotuba yake sasa wote watoto wa baba atampendelea yupi mnamweka JK njia panda kabisaa,
 
Hahaha humu ndani tunapeana hope tu. Watanzania sisi kweli ni bongo lala sana, huwa tunatoa kura kwa kuangalia shape, mtu kaishi ughaibuni kasomea huko.

Akimess tu ndiyo tunagundua kwamba hana maana. Hivi kwa hili tujiweke group gani sisi wananchi wenyewe???

Tubadilike wa TZ, tusikurupuke.
 
Yeye ndiyo Waziri aliyesema jambo; na yeye mwenyewe kalifuta. Yote mawili yako ndani ya uwezo wake. Sasa, kujaribu kuonesha kuwa kwa vile jambo ambalo yeye alilisema baadaye kaona kuwa hakuna ulazima wa kulitekeleza katika piramidi ya vitu vya muhimu kwake siyo kumtendea haki.

Nadhani tumekubali mwanzoni alisema maneno ambayo hayakuwa na hekima sana na yalikuwa ya kusetup yeye mwenyewe; lakini pia tukubali kuwa hekima imeshinda. Japo kwa wengine wangependa kuona hiyo showdown kati ya mwanasiasa mfanyabiashara, na mfanyabiashara mpenda siasa..

Kama ni mpira, timu zote hazikufia uwanjani; mashabiki rudini majumbani kwenu.

Hapo umemaliza....
Mfanyabiashara amekubali kwamba ameshindwa,kwamba aseme waziwazi aliropoka ni ngumu,kwamba aseme waziwazi hekema ilimtoka ni ngumu,kwamba aseme ameshindwa ni ngumu, lakini katika maneno yake tunaona kwamba amekubali kushindwa.Japo sinema ilitangazwa kwa mbwembwe na tukaona 'adivataizi' tunasikitika kwamba imeahirishwa for unknown period of time.Stay turned.
 
=Field Marshall ES;355273]-
Nafikiri kabla hujakurupuka na hii nyepesi, ulitakiwa kujiuliza kwanza nani aliyejitokeza to the public kwanza, kabla ya mwingine, au? Maana nitasema je kua Masha atamdhuru Mengi wakati aliyeanza kushitaki kwetu public ni Mengi?

Naomba uweke msisitizo kwenye neno ulilotumia "Kumdhuru" Kuhusu public wewe ulisema uchaggani...Ngoja nikupe mfano mmoja rahisi...Unaona wwengi wetu hapa wanadai timu hazikufika uwanjani...Nilipokuwa mtoto mdogo kabisa niliweza kuhudhuria mechi nyingi sana za timu ya chuo cha ushirika cha pale Moshi,kabla hata haipanda daraja la kwanza wakati huo.Nilishangazwa sana timu za Simba ama Yanga zikija pale basi uwanja unagawanyika mara mbili na kusema ukweli inakuwa kama timu ya nyumbani wako ugenini ama uwanja huru.Nilijiukiza ni kivipi watu wanazishabikia timu za nje...Ila ilikuwa tofauti sana timu nyingine zote zikija basi uwanja mzima ni Ushirika.
Ni kwanini basi nimetowa mfano huo hapo juu? Si sahihi kusema tu eti Mengi hatapita huko uchaggani,ninaamini kabisa Mengi ana mashabiki almost nchi nzima,na Masha naye ni kiongozi wa kitaifa na kama ni public damage iwe mara ngapi? Uwanjani ni reference ya mahakamani.Siku saba zilikuwa vipi? Ndio maana nikasema ni kwa manufaa ya Lau kama anavyosema MKJJ kuwa ana hekima,yaishise hapo,ndio ilikuwa maana yangu.

- Mkulu wangu Mushi vipi leo mbona nilishaanza kukuaminia, hivi unajua toka nimuoe mke wangu sijawahi kufika kwao na ninaendelea na maisha kama kawa na huenda nisije kufika kabisa huko kwao, sasa eti unasema kuwa Mengi anaweza ku-afford kukosa kwenda kwao kwa sababu ya Masha na this nonesense? Vipi ndugu yangu yaani umeshindwa hata kuona ishus muhimu za taifa kwenye this sagga kama kutoheshimika kwa sheria na wenye nguvu wawili wasiojua mipaka ya nguvu zao!

Ndio maana nikakupa mfano wa timu za Simba na Yanga,zina washabiki nchi nzima,Masha na yeye ni kiongozi wa serikali anayehusika na usalama wa wananchi wa Taifa zima,kwahiyo basi tusubiri tuone hayo mambo ya sheria.

- What a joke! nimekua dissappointed off course yes kwa sababu nilitegemea this drama itaenda kwenye sheria ili kuweka muongozo wa sheria kwa the future generation kuhusu mipaka ya utanuaji kwa viongozi na matajiri katika taifa letu, sihitaji balance kwenye kuwa na haya mawazo, na ninaamini betweeen maneno yangu na yako hapa kwenye this thread sio taabu ku-read betweeen the lines hoja za nani kati yangu na wewe zina matatizo ya balance na bias.

Have a nice day mkuu, next time jifunze kusoma betweeen the lines kinachosemwa, kabla ya kukurupuka!

FEMS sijakurupuka kabisa kwasababu mjadala huu nilifuatilia toka mwanzo na kusema mimi niko bias si kweli kabisa...Kwenye issue zote nimekuwa nikipinga migawanyiko ndani ya jamii ya watanzania iwe ni ya kidini ama kikabila.
Asante mkulu na nadhani umenielewa.
 
Naomba uweke msisitizo kwenye neno ulilotumia "Kumdhuru" Kuhusu public wewe ulisema uchaggani...

- Mengi hawezi kumuharibia Masha kisiasa na ndio sababu mpaka sasa hajataja jina la huyo waziri, tulioliwa hapa ni wananchi maana hii ni a missed opportunity ya kusimamia utawala wa kisheria, watu wawili wenye nguvu za ajabu in our society wasiojua mipaka ya nguvu zao na kuishia kutusumbua wananchi bure.

- By the way, mbona wakiguswa Mrema, na Mengi unakuwa mkali sana bwana Mushi? au? Bwa! ha! ha! ha!
 
-
Mengi hawezi kumuharibia Masha kisiasa na ndio sababu mpaka sasa hajataja jina la huyo waziri, tulioliwa hapa ni wananchi maana hii ni a missed opportunity ya kusimamia utawala wa kisheria, watu wawili wenye nguvu za ajabu in our society wasiojua mipaka ya nguvu zao na kuishia kutusumbua wananchi bure.

Nadhani pia kutokana na previous statement zako...Masha naye hawezi kumwaribia Mengi na ndiyo maana nikauliza vipi siku saba? Ungesema wote hawawezi kuharibiana ningekuelewa zaidi.

- By the way, mbona wakiguswa Mrema, na Mengi unakuwa mkali sana bwana Mushi? au? Bwa! ha! ha! ha!

Sijui kwanini umemmention Mrema along side Mengi kwenye watu "wawili" ninaonekana kuwa "mkali" kama wakiguswa,sijui..Labda kwasababu wote ni wachagga,nadhani utakuwa happy.
Uzuri hapa ni kwamba hata kama unamtetea mtu ndugu Field Marshall ni lazima uwe na pointi za ku back up na si tu kuwa mnazi...Mimi si mnazi,ni mchambuzi tu na kwa uhakika nitakuwa upande wa wazalendo regardless kuwa ni wakristo,waislam ama wachagga.
 
Back
Top Bottom