Waziri Masha ajikanganya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Masha ajikanganya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dark City, Jan 8, 2009.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Leo katika mahojiano na TBC1, Waziri Masha amesema kuwa Mengi hakuleta uthibitisho wake kuhusu tuhuma alizozitoa za kutishiwa kufilisiwa na Waziri kijana. Lakini hawatamchukulia hatua na suala hilo wameachana nalo badala yake wanashughulikia SMS alizotumiwa. Hata hivyo amesahau kuwa katika maelezo yake ya awali alisema endapo hataleta uthibitisho ndani ya siku saba atamchukulia hatua. Sasa hapa kuna nini? Nadhani anatakiwa kutupa maelezo zaidi kwa nini amebadili msimamo. Vinginevyo ni hatari sana kwa waziri (serikali) kushindwa kutekeleza maagizo aliyoyatoa mwenyewe.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jan 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Yeye ndiyo Waziri aliyesema jambo; na yeye mwenyewe kalifuta. Yote mawili yako ndani ya uwezo wake. Sasa, kujaribu kuonesha kuwa kwa vile jambo ambalo yeye alilisema baadaye kaona kuwa hakuna ulazima wa kulitekeleza katika piramidi ya vitu vya muhimu kwake siyo kumtendea haki.

  Nadhani tumekubali mwanzoni alisema maneno ambayo hayakuwa na hekima sana na yalikuwa ya kusetup yeye mwenyewe; lakini pia tukubali kuwa hekima imeshinda. Japo kwa wengine wangependa kuona hiyo showdown kati ya mwanasiasa mfanyabiashara, na mfanyabiashara mpenda siasa..

  Kama ni mpira, timu zote hazikufia uwanjani; mashabiki rudini majumbani kwenu.
   
 3. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji et all,

  Masha kakubali kushindwa,amekataa kufanya kile alichoamini ni sahihi na hii itapelekea kuanguka kwake kisiasa.Time will tell

  Naju unafurahi sababu umejua pa kumshikia pale atakpokuja kuna tena kuzungumza..

  Mtakumbuka wakati Flani mkulu alikuwa akitoa kauli tata sana na alipogundua anachemeka akaamua kuwaachia kina salva wachemke
   
  Last edited: Jan 8, 2009
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kiongozi yeyote wa jamii sifa yake moja ni mtu makini; sasa unapokuwa na viongozi katika serikali ambao wanalopokalopoka mambo then ujue kuna walakini katika mfumo mzima wa uteuzi wao na hilo speaks a lot about the appointing authority!! Mwanakijiji, huyu bwana alilopoloka mambo yaliyo huzunisha jamii kwahiyo kusema kuwa kwa vile yeye ndiye aliyetoa altimatum ya kumuadabisha Mengi na yeye anaweza kuifuta altimatum hiyo bila maelezo ya kina si sahihi!! Masha ana wajibu wa kuelezea jamii kwanini amewithdraw altimatum yake. Mengi alimshtumu waziri wa serikali kuwa anataka kuleta hujuma; waziri huyo Mengi hajamtaja mpaka sasa na ni muhimu serikali ikamfahamu kwani hafai kuwa kiongozi wa serikali.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jan 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280


  sidhani kama kutomchukulia hatua Mengi kutamuangusha kisiasa; labda kitu kingine.

  Nashangazwa mara zote na watu wanaojua kilichomo ndani ya ubongo wangu. Una kipaji kweli.


  hiyo inaitwa hekima.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jan 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Si kweli; kiongozi wa kijamii ana sifa zaidi ya moja.

  Hapo ni extension ya argument ambayo bila kuiwekea mipaka inavunjika on contact.

  Ni sahihi kwa sababu, hakuna mahali ambapo panamkataza Waziri kufuta kauli yake au uamuzi wake wa awali. Kama alikuwa na uwezo wa kusema alichosema nina uhakika ana uwezo wa kufuta alichokisema. Hata hukumu ya kifo yaweza kufutwa!


  Hana wajibu wa kuelezea maamuzi yake hayo. Labda kwa ajili ya curiosity zetu. Ndio maana inaitwa hekima. Kwa sababu chochote atakachokisema kitataka maelezo zaidi.

  Kwani Mengi alisema atamtaja? Nakumbuka alisema "amewasamehe". Kama serikali yenyewe imeona hakuna ulazima wa kumjua Waziri huyo kwa vile walilishughulikia vibaya tangu mwanzo well... hiyo ndiyo gharama ya kukurupuka. Nilisema tangu awali, baada ya Masha kuzungumza hakukuwa na uwezekano tena wa kumjua "Waziri" huyo.
   
 7. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  1.Nafurahi kusikia hivyo,na i quote your word na siku nyingine usije ukaanz kukumbushia mambo haya kama Masha akikosea kutoa kauli tena,I know you well when it comes a tie you want someone to step out


  2.Nadhani kukusoam sana kuhusu habariz ao kunanifanya niweze kujua unataka kusema nini hata kabla haujaanza kusema.Ni uwezo nilio nao tu
   
 8. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ...kama mtu kigeu geu hivi ndio tunampa wizara nyeti kama hiyo tutegemee nini?
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jan 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  unafikiri you know me well! sorry to disappoint you; akifanya jingine nitamhukumu kwa hilo; na mimi kusema kuwa hili amelimaliza sijasema kuwa Masha hajakosea. Ninasema, yeye kaamua kulimaliza kwanini hutaki unataka liendelezwe. NImesema anazo nguvu zote za kisheria na kimadaraka kufanya hivyo. what is the problem?

  well.. una nguvu fulani za kiungu, itabidi nianze kukusujudia!
   
 10. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu Mwanakijiji, kupima upepo wa kasheshe lenyewe ndio ukubwa.Masha atapata credits kwa kukaa kumya baada ya kuona sakata lenyewe halimsaidii kwa vyovyote,sana sana litamharibia.Waswahili walisema"funika kombe wa....... wapite"
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Jan 8, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji, nimemsikiliza kwa makini na hakuna sehemu ambayo Masha amesema anafuta agizo lake. Akiwa anaulizwa kwa woga na Mtangazaji wa TBC1 (Elisha Eliya) na yeye kujibu kwa wasi wasi kidogo, amesema kuwa wameachana nalo. Hakusema kuwa amefuta agizo lake hata kidogo. Na akaongeza kuwa Polisi wataendelea kufuatilia suala la SMS. Labda kama na wewe umekuwa na kipaji cha kusoma hisia zake. Kama ni hekima basi angekiri kuwa agizo lake halitekelezeki hivyo amaelifuta rasmi. Vingenvyo mimi (labda na wengine) namwona kama mtu ambaye hajui analofanya. Sidhani kama vitisho vyote alivyotoa awali ilikuwa ni utani au kutishia mtoto nyau! Kwa maoni yangu ameidhalilisha nafasi ya Uwaziri (ambayo tunajua ilishawahi kukaliwa na watu wenye uwezo wa kufuatilia mambo kama Mrema), Rais aliyemteua na serikali yote. Mimi sijaridhika na maelezo ya juu juu katika issue nyeti kama hii. Vinginevyo amwachie mtu mwingine ofisi afanye kazi naye arudie kazi yake ya uwakili.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Jan 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  anaposema kuwa ameachana nalo, maana yake amelifuta. na anaposema kuwa wanashughulikia sms, maana yake ni hiyo. Kama waziri ana nguvu hizo. SIjui kwanini unataka liwe kubwa kuliko lilivyo.

  Mwanzoni alionesha jazba ya ujana, na sasa ameonesha utulivu wa utu uzima. Kwa hili miye sina tatizo kabisa. So.. endeleeni kudhani kuna tatizo. Waziri kasema wameachana na la Mengi, and that settles it! Hata mahakamani mtu anaweza kuamua kufuta kesi aliyoileta mwenyewe.
   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Jan 8, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Lole, kama angekaa kimya kama ilivyokuwa kabla ya leo, wenye akili tungejua limeisha kiutu uzima. Ila kwa kutoa maelezo yasiyo sahihi kwa umma kwamba wameachana suala hilo; wakati labda wameshinikizwa na wenye busara zao kwamba waliache au wameogopa kuumbuka si sahihi. Alisema serikali ina nguvu na sheria za kutumia iwapo Mengi angekataa kupeleka uthibitisho. Sasa amekataa, wametumia lipi kati ya aliyosema wanayo kumshikisha adabu ili kesho mimi na wewe au mtu mwingine asiibuke na kuirushia serikali tuhuma nzito bila ushahidi? Kufanya jambo ambalo linapoteza credibility ya serikali nadhani ni kosa kubwa. Kama ndiyo amepata hekima basi anastahili kuwajibika kwa kukurupuka. Ofisi anayoongoza itakuwa ni kubwa kuliko uwezo wake.
   
 14. Miwani

  Miwani Senior Member

  #14
  Jan 8, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 182
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mzee mwanakijiji usikasilike unapokosolewa, otherwise inabidi tukutambue kama kibalaka wa Masha.

  Nafikiri mawaziri inabidi watulie kabla hawajatoa tuhuma kwa mzee Mengi, kwani hata Masilingi alikurupuka na baadaye kuishia patumu. mzee Mengi huwa akurupuki tuu na akisema kitu anazo evidence za kutosha
   
 15. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #15
  Jan 8, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji kwa speculation..
  ukisoma maelezo ya hapo juu inaonesha ya kuwa habari iliyoletwa hapa hakikuhaririwa vizuri.Mtu alibebe mawazo yake tu!
   
 16. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #16
  Jan 8, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Mengi mwenyewe si alishasema amemsamehe huyo waziri kijana? wengi wetu tulishajua hili swala litaishia hewani tu.
   
 17. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #17
  Jan 8, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Sidhani kama kuna sehemu yoyote kwenye kanuni za utumishi zinazompa nafasi boss kufanya maamuzi ya jazba kwa sababu tu kijana! Kama ni hivyo naona vijana wote hatufai kushika ofisi kubwa kwani tunaweza kufanya mambo kwa jazba "ya ujana". Hiyo excuse haipo. Jamaa alitumia vibaya madaraka yake na anastahili kuwajibika. Huu ni ufisadi wa kutumia madaraka. Angekuwa mtu mdogo labda angeshaozea keko. Hili siyo suala la kuchekea.
   
 18. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #18
  Jan 8, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Yaani awajibike kwa kusema atachukua hatua kama uthibitisho hautatolewa? Ama nimeelewa hoja zenu vibaya?

  Mimi sioni sababu ya kuwajibika na kumlazimisha Rais kuteua Waziri mwingine kwasababu tu, aliekuwepo alikosea kusema "Mengi athibitishe kauli yake ndani ya siku saba. La sivyo tutamchukulia hatua" ama maneno kama hayo. Haiwezekani. Haiwezekani kwasababu alikuwa na uwezo kweli wa kuchukua hatua, inawezekana ameamua vinginevyo, na hiyo ni haki yake kama msemaji. Haiwezekani kwasababu sio kosa lenye madhara kitaifa (halina hasara kwa taifa) kwa namna yoyote. Kama kuna madhara, yanamhusu yeye msemaji, kwakuwa alijihisi. Sidhani kuwa alisema angechukua hatua kama serikali (niko tayari kusahihishwa kama siko sahihi).
   
 19. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #19
  Jan 8, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mengi na Masha, hawakututendea haki wananchi na taifa zima kwa ujumla, kwa sababu watuwazima wamekuja kutishiana nyau kwa expense yetu taifa na hasa sisi wananchi walalahoi, for what hasa?

  - Mengi ametuhakikishia kwamba ni very powerful na anaweza kuitikisa serikali at any of his time na Masha ametuhakikishia tu kwamba hana uhakika na either sheria au mipaka ya kazi yake, kwa sababu kwa dataz nilizonazo ni kwamba alifikia mahali aliamuru Mengi akamatwe, lakini wakulu wa polisi aliowapa amri wakamcheka sana kwamba haitakuja kutokea, what an-embarrassment kwa waziri na serikali!

  - In the end wananchi walalahoi ambao wengi tulikuwa tume-invest a lot in this sagga, tume-lost maana ni majuzi tu Mengi na Masha walikuwa mahali wakioengea na kucheka as nothing happened, nilijua Mchagga Mengi sio rahisi kumdhuru kijana aliyeoa mtoto wa Mareale Chifu wa wachagga, kamwe haitakuja kutokea maana Mengi atapita wapi huko Uchaggani?

  Turudi tu backo to the really ishus za taifa! maana aliyejuu labda umfuatie huko huko juu, yale ya zamani ya kumngojea chini hashuki ng'o maana anaweza kutumia parachute asianguke! Tunamuombea Mengi aendele kusaidia wananchi wanyonge kama anavyofanya, maana kwenye hilo atalipwa na Mungu tu, ingawa kwenye ishu ya Masilingi hakuwa mkweli na what real went down!.
   
 20. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #20
  Jan 8, 2009
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Masha katika hili amechemsha.....na ubaya nchini kila kukicha kunatokea inshu nyingine na kupoteza mjadala...hapa watanzania lazima wajua namna na aina ya viongozi walionao kwani hajaja kukanusha kauli zake wala kuchukua hatua yoyote.

  Inshu nyingi kwetu zinazimwa kwa staili hii...huyu jamaa aalipaswa ajiuzulu kwani alisha ahidi mwenyewe kwa mdomo wake!
   
Loading...