Habari mpendwa mteja wetu
Tunakujulisha kuwa leo ilitokea hitilafu kwenye laini yetu ya nordic inayolisha maeneo husika, wataalamu wetu walifanikiwa kutatua tatizo mara baada ya kufanya ukaguzi wa kina mwenye laini husika,
Aidha tunakusihi kujenga utaratibu wa kitoa taarifa au kuuliza kupitia njia zetu za mawasiliano au kutupatia namba yako yenye whatsApp kwa taarifa za eneo lako
shirika linatambua kuwa kuna changamoyo na ongezeko la mahitaji ya umeme kwa wakazi wa Kimara hadi Kibamba ndio maana ujenzi wa kituo kikubwa cha kupoza umeme umeanza maeno ya Lugurunu, kituo huki kitasaidia sana kuondoka makatizo ya umeme kwa wateja wetu.
Mkuu bila shaka unanikumbuka vizuri kwa jinsi tunavyoparuana kule kwenye uzi wa Tanesco sababu ya katikakatika ya umeme isiyoisha Kimara mwisho.
Hiyo feeder yenu ya nordic haijaanza kusumbua leo.Usidhani taarifa hatuna.
Ni miaka mingi changamoto ya mitambo yenu kuzidiwa nguvu huku Kimara ipo lakini hambadiliki,kila siku ni kutupa majibu laini kama haya ila mwaka unapita maisha yale yale.
Jana pekee kuanzia mida ya saa 12 jioni hadi saa 4 usiku mmekata na kurudisha umeme zaidi ya mara 4 Kimara mwisho!
Tangu October last year hali ni tete!
Miaka ya 2006 mpaka 2014 kulikuwa na tatizo kubwa la low voltage.
Kuanzia 2015 mpaka 2018 ndicho kipindi pekee wakazi wa Kimara na Kibamba tulipata ahueni ya umeme kutulia.
2019 mkalianzisha tena mdogo mdogo na sasa tumesharudi kulekuleee!
Na kila nikifanya uchunguzi sababu kubwa ni distribution network yenu ya huku kuwa weak!huo mtambo wenu wa nordic una muda mrefu sasa unasumbua na hamtaki kuubadilisha ndio unatutesa sana wakazi wa Kimara.
Hebu jiweke nafasi yetu,sisi tumeshanunua luku zenu,tunanunua umeme kila ukiisha,mnatukata kodi kila transaction,haya mengine yanatuhusu nini?tumeshatekeleza upande wetu kama wananchi kuchangia maendelea kwa njia mlizoweka,biashara zetu tunalipia kodi,fremu,etc!Nyinyi mnaposhindwa kutoa huduma na visingizio kibao kila siku mnataka nani awafanyie kazi sasa?!Unataka mimi niende nikanunue hiyo nordic feeder nikuletee?!
Kodi zetu mnapeleka wapi ikiwa miaka na miaka hamtaki kubadilisha mitambo yenu mibovu?!
Kwanini ununuzi wenu wa mitambo hauzingatii utaalamu wakuproject ongezeko la load kila baada ya muda fulani?!trend si zipo?shirika kubwa namna hii linaendeshwaje kienyeji?!
Suala la mji kukua ilipaswa kuwa baraka na fursa ya nyinyi kuichangamkia maana tunavyozidi kuwa wengi au kupandisha matumizi ya umeme ndivyo nyinyi mnavyopata hela,lakini kwenu ni kinyume chake...hivi watanzania nani aliyeturoga?!hizi akili tunatoa wapi?!
Waziri Makamba naona serikali na Tanesco yenu mko bize na project za kuunganisha wateja wapya nchi nzima!Najiuliza kama sisi wateja milioni 3 tu load yetu inaihenyesha mitambo ya Tanesco,mnavyounganisha wateja wengine wengi mmeshafikiria nini kinakwenda kutokea technically?Tutakapofika wateja milioni 4,5,6 Tanesco itakuwa na uwezo wa kuhudumia wote hao au mnaendesha mambo kisiasa tu bila kutazama upande wa kisayansi?!
Mmejitahidi kuwekeza kwenye uzalishaji wa umeme,tunashukuru,sasa ni wakati wa kurudi kwenye distribution nako muwekeze nguvu,vinginevyo huo umeme wenu wa sijui Nyerere sijui wapi hautakuwa na pa kupitia!