Waziri Makamba, anza na Meneja wa TANESCO Kibamba

Waziri Makamba, anza na Meneja wa TANESCO Kibamba

Mkuu bila shaka unanikumbuka vizuri kwa jinsi tunavyoparuana kule kwenye uzi wa Tanesco sababu ya katikakatika ya umeme isiyoisha Kimara mwisho.

Hiyo feeder yenu ya nordic haijaanza kusumbua leo.Usidhani taarifa hatuna.

Ni miaka mingi changamoto ya mitambo yenu kuzidiwa nguvu huku Kimara ipo lakini hambadiliki,kila siku ni kutupa majibu laini kama haya ila mwaka unapita maisha yale yale.

Jana pekee kuanzia mida ya saa 12 jioni hadi saa 4 usiku mmekata na kurudisha umeme zaidi ya mara 4 Kimara mwisho!

Tangu October last year hali ni tete!

Miaka ya 2006 mpaka 2014 kulikuwa na tatizo kubwa la low voltage.

Kuanzia 2015 mpaka 2018 ndicho kipindi pekee wakazi wa Kimara na Kibamba tulipata ahueni ya umeme kutulia.

2019 mkalianzisha tena mdogo mdogo na sasa tumesharudi kulekuleee!

Na kila nikifanya uchunguzi sababu kubwa ni distribution network yenu ya huku kuwa weak!huo mtambo wenu wa nordic una muda mrefu sasa unasumbua na hamtaki kuubadilisha ndio unatutesa sana wakazi wa Kimara.

Hebu jiweke nafasi yetu,sisi tumeshanunua luku zenu,tunanunua umeme kila ukiisha,mnatukata kodi kila transaction,haya mengine yanatuhusu nini?tumeshatekeleza upande wetu kama wananchi kuchangia maendelea kwa njia mlizoweka,biashara zetu tunalipia kodi,fremu,etc!Nyinyi mnaposhindwa kutoa huduma na visingizio kibao kila siku mnataka nani awafanyie kazi sasa?!Unataka mimi niende nikanunue hiyo nordic feeder nikuletee?!

Kodi zetu mnapeleka wapi ikiwa miaka na miaka hamtaki kubadilisha mitambo yenu mibovu?!

Kwanini ununuzi wenu wa mitambo hauzingatii utaalamu wakuproject ongezeko la load kila baada ya muda fulani?!trend si zipo?shirika kubwa namna hii linaendeshwaje kienyeji?!

Suala la mji kukua ilipaswa kuwa baraka na fursa ya nyinyi kuichangamkia maana tunavyozidi kuwa wengi au kupandisha matumizi ya umeme ndivyo nyinyi mnavyopata hela,lakini kwenu ni kinyume chake...hivi watanzania nani aliyeturoga?!hizi akili tunatoa wapi?!

Waziri Makamba naona serikali na Tanesco yenu mko bize na project za kuunganisha wateja wapya nchi nzima!Najiuliza kama sisi wateja milioni 3 tu load yetu inaihenyesha mitambo ya Tanesco,mnavyounganisha wateja wengine wengi mmeshafikiria nini kinakwenda kutokea technically?Tutakapofika wateja milioni 4,5,6 Tanesco itakuwa na uwezo wa kuhudumia wote hao au mnaendesha mambo kisiasa tu bila kutazama upande wa kisayansi?!
Mmejitahidi kuwekeza kwenye uzalishaji wa umeme,tunashukuru,sasa ni wakati wa kurudi kwenye distribution nako muwekeze nguvu,vinginevyo huo umeme wenu wa sijui Nyerere sijui wapi hautakuwa na pa kupitia!
Tumeomba namba zenu kwa ajili ya kuwapatia taarifa na kuwasikiliza bila mafanikio, tunaamini mtatoa ushirikiano zaidi
 
Hawa jamaa mim siwapendi sana..wanachangia kutuletea umaskini...wanamajibu ya hovyo..
TANESCO nimewapa taarifa kuhusu kulipia umeme toka april mpk leo hamjanifungia...nimelipia nyingine nayo mnanizungusha,
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
 
Jifunzeni utaratibu wa kupokea simu na kutoa majibu ya kiungwana kwa wateja wenu.
Mngekua mnapokea simu huyu mteja wenu asingelalamikia huku.
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
 
Wewe jamaa wa tanesco Mimi nakushukuru kwa kujibu hapa. Ila wengi wetu tunatoa taharifa kwa maeneo husika sioni malalamiko ya mtu mmoja mmoja kwenye nyumba yake tu. Ni kwa ajili ya eneo zima kama kibamba. Sasa unaomba namba ya simu ya nini? Au kibamba tanesco hampajui unataka kuelekezwa?
Hahah wanataka kuja home
 
Kwa waziri huyu wa sasa tutarajie majanga zaidi.... Wapiga deal wapo kazini.....
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
Uwenda ikawa mnafanya kazi nzuri lakini mameneja wenu wachache wanawachafua, hivi inawezekana vipi mfano huko Babati vijijini eneo watu wametuma maombi ya umeme ni mwaka sasa unaisha na wiring wamefanya nguzo zimepelekwa na kusimamishwa lakini umeme hawaonganishiwi, wakaenda kuuliza majibu hayaeleweki ni kama wanatengeneza mazingira ya rushwa.

Tunaomba muwasaidie hawa wananchi ambao nyie mnafanya kazi kwa niaba yao, fuatilieni kata ya Dareda, Galapo na Magugu mkajione.
 
Uwenda ikawa mnafanya kazi nzuri lakini mameneja wenu wachache wanawachafua, hivi inawezekana vipi mfano huko Babati vijijini eneo watu wametuma maombi ya umeme ni mwaka sasa unaisha na wiring wamefanya nguzo zimepelekwa na kusimamishwa lakini umeme hawaonganishiwi, wakaenda kuuliza majibu hayaeleweki ni kama wanatengeneza mazingira ya rushwa.

Tunaomba muwasaidie hawa wananchi ambao nyie mnafanya kazi kwa niaba yao, fuatilieni kata ya Dareda, Galapo na Magugu mkajione.
Tafadhali tujulishe umeomba umeme kwa jina gani? Umefanya malipo lini? Namba ya simu na eneo kwa hatua zaidi. Hatuwezi kutoa ufafanuzi bila kujiridhisha na undani wa taafifa husika
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
Search PM yako taarifa zangu zipo...toka April nimeripot mara nyingi...
Kama umefuta sema
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
Tabata mawenzi mtaa wa darajani hakuna umeme tangu saa 12 nini tatizo
 
Habari mpendwa mteja wetu

Tunakujulisha kuwa leo ilitokea hitilafu kwenye laini yetu ya nordic inayolisha maeneo husika, wataalamu wetu walifanikiwa kutatua tatizo mara baada ya kufanya ukaguzi wa kina mwenye laini husika,

Aidha tunakusihi kujenga utaratibu wa kitoa taarifa au kuuliza kupitia njia zetu za mawasiliano au kutupatia namba yako yenye whatsApp kwa taarifa za eneo lako

shirika linatambua kuwa kuna changamoyo na ongezeko la mahitaji ya umeme kwa wakazi wa Kimara hadi Kibamba ndio maana ujenzi wa kituo kikubwa cha kupoza umeme umeanza maeno ya Lugurunu, kituo huki kitasaidia sana kuondoka makatizo ya umeme kwa wateja wetu.
Nyie ni wa kutumbuliwa Tu! Tanesco Kibamba ni uozo mtupu! Mimi nipo Luguluni siku zote matengenezo yapi unaongelea? Acheni Siasa, mnatutia Hasara, wazembe wakubwa nyie!
 
Tabata mawenzi mtaa wa darajani hakuna umeme tangu saa 12 nini tatizo
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

22-09-2021,

TAARIFA YA MABORESHO YA MIUNDOMBINU MKOA WA ILALA

Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Ilala linawataarifu wateja wake wa wilaya ya Tabata kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo.

Siku: ALHAMISI

Tarehe: 23-09-2021

Muda: Saa 01:30asubuhi-07:30 mchana.

SABABU: Kufanya matengenezo katika kituo cha kupooza na kusamba umeme cha Kipawa pamoja na kuhamisha miundombinu ya laini kubwa ya umeme ili kupisha ujenzi wa reli ya mwendokasi SGR.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA
Tabata Dampo, Tabata relini, Aroma, Tabata shule, Kisiwani,Muslim, Bima, Liwiti, Kimanga yote, Ubayaubaya, Makoka, Kisukuru yote, Barakuda, Chang'ombe, Segerea yote, Bonyokwa, Kinyerezi yote, Khanga, Kibaga, Hali ya hewa, King'azi, Kifuru yote na maeneo jirani.


Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza katika kipindi chote cha kukosa huduma.

Tahadhari
Usikanyage wala kugusa waya uliokatika au kulala chini.

Wasiliana nasi kwa simu na.zifuatazo: Dawati la dharura wilaya ya Tabata
0715768589/0684001068.

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz,

Mitandao ya kijamii

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook Kirjaudu sisään Facebookiin

Imetolewa na:

OFISI YA UHUSIANO NA HUDUMA KWA WATEJA- TANESCO TABATA.
 
Dawa Yao unafunga sola, wakikata automatic sola inafanya kaz, yaani “Hybrid“
 
Ni ajabu kila mtu huita waziri when things do not go your way.

Ni kama watoto wadogo wanashitakia kwa mzazi

SIsi wanadamu tuna euphoria ya kipumbavu sana ya kutaka kua under influence ya higher power maana tulianzia kwa wazazi wetu

Tumekua watu wazima still tuna-act kama watoto kupenda kua under influence

Ndio maana tunatawaliwa na mdikteta anaua mamilioni ya watu lakini still we happen to love them regardless

Wanadamu tuna kiherehere cha kupenda wrong people

Akija kiongozi mpenda demokrasia anaetoa uhuru wa kutosha na rule of law na kila kitu,utashangaa anatukanwa anatakiwa dikteta

One another thing,yaani nyie mnapoona watu wako maofisini wanafanyakazi yaani mnadhani hawa watu wazima wanakuja kazini kucheza tu kama watoto,nyie akina USSR ndio mnajua kufanya kazi na ndio watu makini duniani hapa

Tanesco ni watoto tu wanakuja kazini kucheza hivyo wasimamiwe kama vitoto,wachapwe,wapigishwe magoti,etc sababu USSR kasema

Mkuu,wanadamu hawa ni watu wazima,na wanaenda kazini kila siku ku-solve matatizo mpaka unapata umeme,etc.....Hii kukaa hapa na kuwachukulia kama vitoto vidogo vile vinatakiwa vichapwe havijui vinavyofanya waziri akavichape ni trend ile ile ya demonization ya your fellow human beings kwa kujifanya wewe ni upper class sana

Mzizi wa matatizo sio hawa wafanyakazi,they work hard everyday in shifts kufanikisha umeme una enjoy kwenye vibanda vyenu,tatizo ni serikali yako kuingiza politics Tanesco yenye kujenga deni kila siku

Yaani unaongea as if wafanyakazi wa tanesco maofisini mwao wamejaza magodoro wao ni kulala asubuhi mpaka jioni

This is demonization of the highest order..Unawaonea,sio wao,tatizo ni the same govt kupanga policies za kuielekeza tanesco kufanya biashara zake,eti uza mita 23k wakati mita inauzwa China kiwandani dola 50..soma financial statements za Tanesco,they are trying.
Wewe na wazazi wako ndio mna eaphoria , serkali tumeichagu sisi itutumikie na hapa na hapa ndio accountability inaoneka huu huyuhyu makamba Jana aliitwa na makamo wa rais aende kigoma ambapo pia umeme unakatika katika


USSR
 
Tafadhali tujulishe umeomba umeme kwa jina gani? Umefanya malipo lini? Namba ya simu na eneo kwa hatua zaidi. Hatuwezi kutoa ufafanuzi bila kujiridhisha na undani wa taafifa husika
Bro we kausha. Ukijibu kila povu humu linalotolewa utajikuta hufanyi kazi zako nyingine. Mbongo ni kumpa jibu moja tu na kukaa kimya. Ukisema ujibu kila analouliza ujue mtakesha ili mradi tu akusumbue tu, akutishe, akung'ong'e yaani amepata pa kupunguzia ma stress yake.
 
Meneja wa Tanesco Chanika Anaitwa Babu; Huyu mhaya ndio hafai; hana uhusiano na wateja ie customer service zero. Anatukana wateja wake
 
Meneja wa Tanesco Chanika Anaitwa Babu; Huyu mhaya ndio hafai; hana uhusiano na wateja ie customer service zero. Anatukana wateja wake
Nitumie namba yake

USSR
 
Meneja wa Tanesco Chanika Anaitwa Babu; Huyu mhaya ndio hafai; hana uhusiano na wateja ie customer service zero. Anatukana wateja wake
Tunaomba namba yako ya simu tukusikilize tafadhali,

TANESCO MAKAO MAKUU
 
Tumeomba namba zenu kwa ajili ya kuwapatia taarifa na kuwasikiliza bila mafanikio, tunaamini mtatoa ushirikiano zaidi
Kunipa taarifa kwamba siku fulani unanikatia umeme sababu unakata miti au?!
Sijui umeelewa context ya post yangu?!

By the way,sioni umuhimu wa kutoa namba sababu suala hili sio personal,ni la kijamii,ni Kimara yote,Mbezi,Kibamba,ndio maana tunakutajia location,na fact kwamba umekuja hapa na kututajia tatizo la msingi la eneo letu(nordic feeder,na nakubaliana nawe maana najua hilo tatizo) inaonyesha unalifahamu vizuri eneo na tatizo lake,sasa namba za simu za nini?utatuma message kwa watu wangapi?hizo group za whatsapp mtatuunga raia wote wa Kimara,Kibamba?kwanini msiendelee na ule utaratibu wa miaka yote,wa kutumia media,na siku hizi ni rahisi tu sababu ya teknolojia.
Mnaweza hata kuanzisha Tanesco app mtu ukidownload humo unapata taarifa zote,kila eneo,itatusaidia sisi,nyinyi na serikali.
Moja kati ya vitu napenda kuhusu hii mitandao ya kijamii ni transparency,haina unafiki.Mimi nawajibika kusema kitu sahihi,na wewe pia.Hamna longolongo humu,maana kila mdau anaona na kupitia.
Na tunashukuru kwenu kuwemo humu pia.Sasa mtusaidie umeme huu siku hizi kuukata ni tatizo msikate umeme,boresheni miundombinu.

Tena tunavyoandika humu tunawasaidieni maana naamini sio kila jambo limo ndani ya uwezo wenu Tanesco.Mengine najua yamewazidi uwezo,so wananchi tukiandika kama hivi tunawasaidieni sana tu,sijui unananielew ndugu?!

Naamini kabisa suala la kununua feeder mpya au mtambo wowote within your distribution network sio jepesi kwa wewe na meneja wako kulifanyia uamuzi kirahisi tu,hiyo hela huna na uwezo wa kufanya maamuzi hayo uko kwa wenyewe uko juu ambao huenda hawawapeni nyinyi watendaji response ya kutosha kulinganana presha mnayoipata toka kwa raia huku chini na matokeo yake nyie mnakaangwa hapa kati mkiwa innocent kabisa.Kuna kipindi unapiga simu customer care na kuongea kwa ukali ukilaumu watu lakini jinsi wanavyojibu hadi unawaonea huruma,unajistukia kabisa unamlaumu mtu asiye na hatia.Usifikiri wananchi hatujui situation,tunafahamu vizuri tu.Hapa taarifa zishawafikia wenye hela na wafanya maamuzi.Tunakusaidia bwana Tanesco maana tumechoka,tatizo limedumu muda mrefu now.

Let it be known to the hierachy.
 
Back
Top Bottom