mimimkweli
New Member
- Mar 24, 2010
- 1
- 0
Tangu mwaka huu 2025 umeanza TANESCO wamekuwa na huduma mbaya ndani ya Mkoa huu wa kwao wa kiutendaji (KINONDONI SOUTH) hasa njia ya umeme ya kutoa huduma kuanzia Kimara mpaka Kibamba.
Umeme Kila siku unakatika katika ndani ya muda mfupi na wakati mwingine kukatwa kwa muda mrefu kwa maelekezo kuwa wanarekebisha miundombinu lakini tatizo haliishi.
Taarifa hii iwafikie viongozi wa TANESCO na SERIKALI kwa ujumla. Mijadala ya kwenye kundi la WhatsApp la Tanesco inatosha kuelezea tatizo hili.
Yafaa kupatiwa utatuzi wa uhakika wa mara moja.
Tunaomba watuletee majibu ya uhakika kwani Hali ni mbaya na shughuli za kiuchumi zinasimama.
Kiukweli shirika limekuwa likihujumu uchumi wa watu binafsi na SERIKALI. Tunaomba utatuzi wa mapema.
Pia soma: KERO - TANESCO mnakata umeme kuanzia Kimara mpaka Mbezi kwa zaidi ya masaa 12 kila siku bila ya kutoa taarifa yoyote ile ya kueleweka