Jambo jema sana lililochelew*Waziri Makamba ameivunja Bodi ya Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) kwa tuhuma za rushwa, ucheleweshwaji kibali cha ukaguzi na lugha mbovu.
'Sababu za mabadiliko ya Bodi ya NEMC ni ucheleweshwaji wa vibali vya ukaguzi wa mazingira na tuhuma za rushwa kwenye usimamizi.
Watendaji wa NEMC wamesaidia watu wenye maslahi nao na tuliwataka watueleze jinsi wanavyofanya kazi lakini hawajafanya hivyo.
Sasa kutokana na mapungufu makubwa ndani ya NEMC, tumeamua kuivunja bodi hii kuanzia leo na viongozi wengine tutawatangaza leo
Wapo pia baadhi ya watendaji wa NEMC tuliowasimamisha kazi ili ufanywe uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili kabla kuchukua hatua
Na kuanzia sasa muwekezaji akikamilisha kutoa taarifa ya ujenzi wa kiwanda, ruhusa ya ujenzi itatoka ndani ya siku tatu
Tathmini ya mazingira itafanyika wakati ujenzi wa kiwanda husika unaendelea bila kusubiri cheti cha uthibitisho cha mazingira
Wawekezaji wanaokwenda NEMC wanatakiwa kuanzia kwa washauri elekezi ili kuondoa uhusiano wao na watu wa Baraza la NEMC'
Tutapima maeneo yote yanayofaa ili muwekezaji akipatikana asipate shida ya kutafuta eneo lake, yeye ataona maeneo yakiwa tayari'
'Wote tuliowachukulia hatua leo uchunguzi wa awali ulitosheleza kuwachukulia hatua stahiki, hatua nyingine zitafuata baadaye'
Tutatoa gharama elekezi kwa washauri elekezi wote ili wawekezaji wasilipie gharama kubwa kufanya uwekezaji popote nchini'
Kuna gharama tutazipunguza au kuziondoa kabisa kwenye mchakato wa uwekezaji, tunashindana na nchi nyengine kuvutia wawekezaji.
Kwa hisani ya Millard Ayo.
Ni Kweli wanachelewesha sana kibali mpaka utoe rushwa ndiyo upewe kibali na siku zote hawakutembelei kutoa ushauri wa mambo mbalimbali ya kitaalamu wanasubiri ukosee ndiyo wanakuja kuomba rushwa na kukupiga kafaini kakishikaji ili waonekane wanafanya kazi na wanaandamana na waandishi wa habari ili kupata sifa
Migodi na viwanda ikitiririsha sumu mnaanza kulalama serikali haifanyi kazi haijali wananchi wake..Kila Waziri anatafuta sifa
You are right mkuuGuys, try to think big please. Sababu za kuvunja hii Bodi ya NEMC si issue ya Uwekezaji baali ni baada ya Mahakama wilaya ya Hai kumtia hatiani DC kwa kuharibu shamba la Mhe. Mbowe kwa kisingizio cha kuharibu Mazingira huku NEMC wakimkana DC kuwa hawakumtuma!! Kwanini Bodi ivunjwe sasa baada ya tukio la Hai na siyo kabla???
Nilijua tu CCM ni ya wajinga na masikini (TWAWEZA)Migodi na viwanda ikitiririsha sumu mnaanza kulalama serikali haifanyi kazi haijali wananchi wake..
Inapoamua kuchukua hatua kwa kuwalinda wananchi wake mnasema anatafuta sifa.
Kweli Tanzania tunastahili namba moja kwa unafiki Duniani.
Mashuuuz jazz band at its bestLile Biff la NW na Waziri wake limeisha?? Nasikia amewekewa NW kanda maarum iw rahisi kumdhibiti je ni kweli??? Maana huyu kijana ndio alikuwa msiri wa JK.....kama alivyo Bashite kwa sasa! Yeye ndio anatafuta waganga na kuwalipa!! Kazi ipo watoto pendwa wa awamu 4 na ya 5
Na wewe mwananchi unanufaikaKila Waziri anatafuta sifa
Kivipi?
Hii awamu ni ya kuvunja na kuteua upya.Hapo utaonekana mtendaji mzuri
Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app