Waziri Makamba aivunja bodi ya Baraza la Taifa la Mazingira(NEMC)

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
DE735lVWsAAd_dQ.jpg

Waziri Makamba ameivunja Bodi ya Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) kwa tuhuma za rushwa, ucheleweshwaji kibali cha ukaguzi na lugha mbovu.

'Sababu za mabadiliko ya Bodi ya NEMC ni ucheleweshwaji wa vibali vya ukaguzi wa mazingira na tuhuma za rushwa kwenye usimamizi.

Watendaji wa NEMC wamesaidia watu wenye maslahi nao na tuliwataka watueleze jinsi wanavyofanya kazi lakini hawajafanya hivyo.

Sasa kutokana na mapungufu makubwa ndani ya NEMC, tumeamua kuivunja bodi hii kuanzia leo na viongozi wengine tutawatangaza leo

Wapo pia baadhi ya watendaji wa NEMC tuliowasimamisha kazi ili ufanywe uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili kabla kuchukua hatua

Na kuanzia sasa muwekezaji akikamilisha kutoa taarifa ya ujenzi wa kiwanda, ruhusa ya ujenzi itatoka ndani ya siku tatu

Tathmini ya mazingira itafanyika wakati ujenzi wa kiwanda husika unaendelea bila kusubiri cheti cha uthibitisho cha mazingira

Wawekezaji wanaokwenda NEMC wanatakiwa kuanzia kwa washauri elekezi ili kuondoa uhusiano wao na watu wa Baraza la NEMC'

Tutapima maeneo yote yanayofaa ili muwekezaji akipatikana asipate shida ya kutafuta eneo lake, yeye ataona maeneo yakiwa tayari'

'Wote tuliowachukulia hatua leo uchunguzi wa awali ulitosheleza kuwachukulia hatua stahiki, hatua nyingine zitafuata baadaye'

Tutatoa gharama elekezi kwa washauri elekezi wote ili wawekezaji wasilipie gharama kubwa kufanya uwekezaji popote nchini'

Kuna gharama tutazipunguza au kuziondoa kabisa kwenye mchakato wa uwekezaji, tunashindana na nchi nyengine kuvutia wawekezaji.

Kwa hisani ya Millard Ayo.

========

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Januari Makamba amefanya mabadiliko makubwa kwenye Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Akizungumza leo Jumatatu, Julai 17, Makamba amesema amebaini mazingira ya rushwa katika kutengeneza vyeti ambavyo havijafuata mchakato stahiki na urasimu.

Mengine ni kutokuwa na lugha nzuri kwa wateja na kuwatisha ili watoe chochote na kuzitumia kampuni binafsi za watumishi wa NEMC kufanya kazi za ukaguzi/uhakiki wa ndani ya NEMC kwa kisingizio cha kutokuwa na watumishi wa kutosha.

Pia amewasimamisha kazi Manchare Heche, Deus Katwale, Andrew Kalua na Benjamin Dotto huku wengine wakiendelea kuchunguzwa wakati wizara ikiendelea kupokea taarifa za ziada.

Pia Waziri amefanya mabadiliko ya wakuu wa kanda;
*Jafari Chimgege, aliyekuwa Kanda ya Mashariki, sasa atakuwa Mkuu wa Kanda ya Dodoma.


*Goodlove Mwamsojo, aliyekuwa Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu-Mbeya, sasa atakuwa Mkuu wa Kanda ya Mashariki-Dar es Salaam.

*Dk Ruth Rugwisha, aliyekuwa Mkuu wa Kurugenzi ya Sheria, sasa atakuwa Mkuu wa Kanda ya Ziwa Mwanza;

*Dk Vedastus Makota, aliyekuwa Mkurugenzi wa
Mawasiliano, sasa atakuwa Mkuu wa Kanda ya Kusini - Mtwara;

*Joseph Kombe, aliyekuwa Mkuu wa Kurugenzi ya Utafiti na Mipango anakwenda kuwa Mkuu wa Kanda ya Kaskazini-Arusha.

*Dk Menard Jangu aliyekuwa Kanda ya Arusha anarudishwa Makao Makuu ya NEMC kuwa Kaimu Mkuu wa Kurugenzi ya Utafiti na Mipango.

*Jamal Baruti, aliyekuwa Mkuu wa Kanda ya Ziwa, anarudi Makao Makuu NEMC.
*Lewis Nzari aliyekuwa Mkuu wa Kanda ya Kusini –
Mtwara, sasa anakuwa Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
 
Basi unaweza kukuta miongoni mwa wanabodi hao anaingizwa tena kwenye bodi mpya ifuatayo
 
Ni Kweli wanachelewesha sana kibali mpaka utoe rushwa ndiyo upewe kibali na siku zote hawakutembelei kutoa ushauri wa mambo mbalimbali ya kitaalamu wanasubiri ukosee ndiyo wanakuja kuomba rushwa na kukupiga kafaini kakishikaji ili waonekane wanafanya kazi na wanaandamana na waandishi wa habari ili kupata sifa
 
Bodi mpya ikichaguliwa kama sio kuteuliwa, wahakikishe wanawahi kushughulikia matatizo ya maji ya kemikali huko kwenye migodi na viwanda wananchi wanaumia sana! Pia madampo yakae katika standadi inayokubalika
 
Lile Biff la NW na Waziri wake limeisha?? Nasikia amewekewa NW kanda maarum iw rahisi kumdhibiti je ni kweli??? Maana huyu kijana ndio alikuwa msiri wa JK.....kama alivyo Bashite kwa sasa! Yeye ndio anatafuta waganga na kuwalipa!! Kazi ipo watoto pendwa wa awamu 4 na ya 5
 
sasa mtu akirusiwa kujenga kiwanda kabla ya environmental impact accessment ikija kugundulika baadae kama effect yake ni kubwa watafanyeje?
 
huu mchezo unataka akili sana hii ni mbinu ya kumtetea DC yule kufuta ushahidi mbowe kuwa makini hapo hulipwi

iPhone 6
 
Waziri Makamba ameivunja Bodi ya Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) kwa tuhuma za rushwa, ucheleweshwaji kibali cha ukaguzi na lugha mbovu.

Sababu za mabadiliko ya Bodi ya NEMC ni ucheleweshwaji wa vibali vya ukaguzi wa mazingira na tuhuma za rushwa kwenye usimamizi.

Watendaji wa NEMC wamesaidia watu wenye maslahi nao na tuliwataka watueleze jinsi wanavyofanya kazi lakini hawajafanya hivyo.

Sasa kutokana na mapungufu makubwa ndani ya NEMC, tumeamua kuivunja bodi hii kuanzia leo na viongozi wengine tutawatangaza leo.

Wapo pia baadhi ya watendaji wa NEMC tuliowasimamisha kazi ili ufanywe uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili kabla kuchukua hatua.

Na kuanzia sasa muwekezaji akikamilisha kutoa taarifa ya ujenzi wa kiwanda, ruhusa ya ujenzi itatoka ndani ya siku tatu.

'Tathmini ya mazingira itafanyika wakati ujenzi wa kiwanda husika unaendelea bila kusubiri cheti cha uthibitisho cha mazingira.

Wawekezaji wanaokwenda NEMC wanatakiwa kuanzia kwa washauri elekezi ili kuondoa uhusiano wao na watu wa Baraza la NEMC.
 
NEMC Board Members
  1. Prof. Salome Misana............................................Chairperson
  2. Prof. Reuben J.L. Mwamakimbullah (PhD)..........Member
  3. Eng. Bengiel Msofe .............................................Member
  4. Eng. Frida Rweyemamu........................................Member
  5. Bi Anna W. Mtani...................................................Member
  6. Bi Judica H. K. Omari............................................Member
  7. Ndg Juma Mgoo...................................................Member
  8. Mr. Sheha M. J. Makame.....................................Member
 
Siku hizi usipovunja taasisi na kutumbua watu unaonekana hufanyi kazi.

Wahenga walisema nyumba inayomilikiwa na mwendawazimu, wapangaji wake ni vichaaa.
 
Back
Top Bottom