Waziri Kigwangalla, akifunga kiwanda cha Afro American kinachozalisha viroba aina ya Zed na Dollars

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
c86d943b-301a-4e7a-91c9-26c9e82de8f1.jpg

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla, ameendelea na usimamizi wa Operesheni Maalum ya kufuatilia na kuufumua mtandao wa Viroba na Pombe feki na haramu nchini.

Mchana huu amelazimika ku na vinginevyo ambavyo vimekutwa havina vibali vya TFDA na havina usajili wa TFDA, havina Batch Number ya kutambua uhalali wa uzalishaji wake, havina tarehe ya kuzalishwa na wala ya ku-expire. Hivyo ni ngumu kutambua ubora wake na idadi yake halisi kwa maksudi ya kulipa kodi ya serikali.
2dab5f0e-19be-494f-90f9-078aaed996f3 (1).jpg

Wenye kiwanda hawatunzi rekodi za uzalishaji na wamekiri kuwa mitambo yao haina uwezo wa kuweka batch number.

Jana akiendesha operesheni hii maalum, Dkt. Kigwangalla alibaini uwepo wa bidhaa hizi sokoni na hivyo aliagiza wataalamu wafuatilie kinyume nyume kujua zinakotoka. Upelelezi umewafikisha hapa.
15078580_1240030979389156_13060648658799508_n.jpg


=====
UPDATE

Imethibitika kuwa Viroba na Pombe feki zilizokutwa zikitengenezwa zinauzwa katika Mkoa wa Mbeya na Tunduma, inadaiwa mmiliki wa Kiwanda hicho husafirisha bidhaa hizo hatari muda wa usiku kwa ngari mbili za Tani 2.

b6ade7ab-7779-414a-8cf4-79efa1ca43f5.jpg
 
sasa si wangewatoza fine na kuwapa muda walipe waendelee? kama hizo pombe ziko sawa wakifunga sinza watafungua pengine trust me.
wamesema watafungua viwanda 1800 sasa mbona kama wanaanza kuvifungia
mwizi ni mwizi tu ... watarudia wakale wapi
 
Ndio kazi waliobakiza....

Nilitegemea wangekuwa washamkamata aliyetengeneza ARV fake ....

Lakini nasikia jamaa lilishinda kesi na linaidai serikali ya Magufuli mabilion ya pesa........

Only in black continent.....
Kigwangala na wanyonge , akina Mwaka, sasa Dollars! Kigwangala Mungu anakuona. Halafu oh, alikuwa mtenda haki, mpenzi wa watu, hakuwa na visasi . Mapambio matupu
 
Kigwangala hashindwi kitu...! Kama aliwezza kumfungia Dr. Mwaka na akafyata mkia, hakuna wa kumshindwa..
 
Angeanza viroba uchwara
Boss
Ryder
Master
Victoria
Nk
Hiii mikoa.ya mipakan ina.viroba km.aina.mia ZED cha mtoto kabisa

Vjana.wanachoma.main.wanasubili tuu kufa gafla,tunduma,bukoba huko.nk


Viroba
 
Ndio kazi waliobakiza....

Nilitegemea wangekuwa washamkamata aliyetengeneza ARV fake ....

Lakini nasikia jamaa lilishinda kesi na linaidai serikali ya Magufuli mabilion ya pesa........

Only in black continent.....
Black people, black ideas in the black continent
 
Ngoja niunganishe doti, hawa watakua watumiaji wazuri wa hizo mambo sasa baada ya mwenzao mmoja kupiga kitu fake na hangover kugoma kuisha hadi wakati wa kujibu maswali, ndo sasa wameamua wawasake wote waliosababisha mwenzao atumbuliwe, anyway jiokoeni ili na sisi mtuokoe kupitia migongo yenu.
 
Back
Top Bottom