Waziri Kairuki: Almasi kutoka Tanzania imeuzwa USD Milioni 10. 2 huko Antwerp nchini Belgium

Mi hela yote hiyo+kuongezeka kwa makusanyo ya t.r.a.......kwanini deni la taifa linazidi kuongezeka kwa speed ya 4g
 
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio yaliyoanza kupatikana katika sekta ya madini.

Kairuki alisema serikali itapata mrabaha wa Dola za Marekani 124,176.97 (Sh. milioni 276.2), pamoja na ada ya ukaguzi Dola za Marekani 20,695.80 (Sh. milioni 46.036).

Alisema Agosti 31, mwaka huu, serikali ilizuia mzigo wa almasi za kampuni hiyo zilizokuwa zinasafirishwa kwenda Antwerp, Ubelgiji na kwamba mzigo huo bado unashikiliwa hadi sasa.

Hata hivyo, alisema serikali iliiruhusu kampuni hiyo kuendelea na uzalishaji wa almasi ambapo na kuzalisha karati 39,567.96.

“Waliomba waruhusiwe kuuza almasi hiyo, serikali ilikubali na wataalamu wa serikali walithaminisha almasi hizo na kupata thamani ya awali kuwa ni Sh. bilioni 18.2,” alisema.

Alisema mrabaha wa awali ulilipwa Sh. bilioni moja na ada ya ukaguzi ilikuwa Sh. milioni 182.2, hivyo serikali kupata jumla ya Sh. bilioni 1.288.

DSCN2069-1.jpg

Waziri Kairuki alisema Oktoba 20, mwaka huu, almasi hizo zilisafirishwa kwenda Ubelgiji na serikali ilituma maofisa wake kusimamia uuzwaji wa almasi hiyo ambayo huuzwa kwa njia ya mnada.

Alisema juzi almasi hizo ziliuzwa kwa dola za Marekani 10,261,227.76 (Sh. bilioni 22.8) ikiwa ongezeko la Dola za Marekani 2,069,582.77 (Sh. bilioni 4.6) sawa na asilimia 20.16 ya thamani ya uthaminishwaji wa awali.

Aliongeza kuwa katika mzigo huo wa almasi kulikuwa na almasi moja yenye rangi ya pinki yenye uzito wa karati 5.92 ambayo iliuzwa kwa Dola za Marekani 2,005,555 (Sh. bilioni 4.51).

Aidha, Kairuki alisema Oktoba 29, mwaka huu, katika eneo la Kiabakari, mkoani Mara, serikali ilikamata sampuli za miamba ya madini ya dhahabu kilo 600 zilizokuwa zikisafirishwa na kampuni ya ZEM (T) Ltd bila vibali kutoka serikalini.

Alisema sampuni hizo zilichukuliwa na kupelekwa kwenye maabara ya Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na baada ya kufanyika uchunguzi ilithibitika kuwa kweli ni miamba ya dhahabu.

Waziri Kairuki alisema Serikali imeamua kuwapeleka mahakamani, ili sheria ichukue mkondo wake kwa kosa la kusafirisha na kukutwa na sampuli hizo bila kibali.
Credit: Mjengwa Blog
Haya wakajenge na Bandari Chato
 
Naomba mnieleweshe hayo mabilioni ni yapi? Maana nimeona 1.2 bilioni! Pia hata wale jamaa walisema mzigo value yake halisi ni sokoni so baada ya kufika sokoni imeongezeka bilion nne kwa mwenye mzigo sasa kama bilion 18 za awali tumepata 1.2 bilion hiyo bilion nne si tunapata milion 300? Which means total 1.5 bilion sasa hayo mabilion ni yapi? May be nimesahau ile 1% ya 4 bilion mpya ambayo ni 40 milion so all in all hata 1.6 bilion hatujafika. Acheni propaganda kuwaaminisha watu yasiyokuwepo!
 
Tunajinasibu kupata ma billions, lakini tumekuwa wakopaji wakubwa sana.
Hizi kiki hazina faida yoyote
 
...ona sasa akili nyingine za kibashite hizi....BTW talking about kizazi....hivi huyu waziri wa madini anazaa lini???...tuambiane maana watu wa kujua vizazi vya watu nyie....tuambie anazaa lini waziri wako wa madini...ni haki kujua....kama ilivyo haki kujua madini yetu yameuzwa wapi....

Wema hana kizazi, ila angetuletea makengeza mwingine !
 
...ona sasa akili nyingine za kibashite hizi....BTW talking about kizazi....hivi huyu waziri wa madini anazaa lini???...tuambiane maana watu wa kujua vizazi vya watu nyie....tuambie anazaa lini waziri wako wa madini...ni haki kujua....kama ilivyo haki kujua madini yetu yameuzwa wapi....
Mwenyekiti afanye maarifa apate mtoto na miss Tz. Kuna kitu inaitwa IVF
 
Ni muhimu sana kutangaza mafanikio kama alivyofanya Waziri Kairuki. Faida zake ni kama zufuatazo:

1.Watanzania watazidi kuelewa ni kweli tulikuwa tunaibiwa sana.

2. Inawezekana kuwathibiti mabwanyenye kwani viongozi wamewashtukia.

3. Tumbua tumbua anayofanya Rais ni sahihi. Wapo watumishi serikalini wanaoshirikiana na mabwanyenye. Ni kuwatumbua tu, hakuna namna.

4.Watu waliokuwa wakibisha wataubali sasa kwamba ilikuwa sahihi kumwondoa waziri aliyetangulia.
 
Jamani inakuwaje mabilioni wakati mgao ni Dola laki 124 si wenye mzigo ndio wanapata mabilioni? Mbona mnaendelea kututumainisha ujinga, kumbe wawekezaji walikuwa sawa zaidi ya kutaka kuwadhulumu.

Kick zenu balaa

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio yaliyoanza kupatikana katika sekta ya madini.

Kairuki alisema serikali itapata mrabaha wa Dola za Marekani 124,176.97 (Sh. milioni 276.2), pamoja na ada ya ukaguzi Dola za Marekani 20,695.80 (Sh. milioni 46.036).

Alisema Agosti 31, mwaka huu, serikali ilizuia mzigo wa almasi za kampuni hiyo zilizokuwa zinasafirishwa kwenda Antwerp, Ubelgiji na kwamba mzigo huo bado unashikiliwa hadi sasa.

Hata hivyo, alisema serikali iliiruhusu kampuni hiyo kuendelea na uzalishaji wa almasi ambapo na kuzalisha karati 39,567.96.

“Waliomba waruhusiwe kuuza almasi hiyo, serikali ilikubali na wataalamu wa serikali walithaminisha almasi hizo na kupata thamani ya awali kuwa ni Sh. bilioni 18.2,” alisema.

Alisema mrabaha wa awali ulilipwa Sh. bilioni moja na ada ya ukaguzi ilikuwa Sh. milioni 182.2, hivyo serikali kupata jumla ya Sh. bilioni 1.288.

DSCN2069-1.jpg

Waziri Kairuki alisema Oktoba 20, mwaka huu, almasi hizo zilisafirishwa kwenda Ubelgiji na serikali ilituma maofisa wake kusimamia uuzwaji wa almasi hiyo ambayo huuzwa kwa njia ya mnada.

Alisema juzi almasi hizo ziliuzwa kwa dola za Marekani 10,261,227.76 (Sh. bilioni 22.8) ikiwa ongezeko la Dola za Marekani 2,069,582.77 (Sh. bilioni 4.6) sawa na asilimia 20.16 ya thamani ya uthaminishwaji wa awali.

Aliongeza kuwa katika mzigo huo wa almasi kulikuwa na almasi moja yenye rangi ya pinki yenye uzito wa karati 5.92 ambayo iliuzwa kwa Dola za Marekani 2,005,555 (Sh. bilioni 4.51).

Aidha, Kairuki alisema Oktoba 29, mwaka huu, katika eneo la Kiabakari, mkoani Mara, serikali ilikamata sampuli za miamba ya madini ya dhahabu kilo 600 zilizokuwa zikisafirishwa na kampuni ya ZEM (T) Ltd bila vibali kutoka serikalini.

Alisema sampuni hizo zilichukuliwa na kupelekwa kwenye maabara ya Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na baada ya kufanyika uchunguzi ilithibitika kuwa kweli ni miamba ya dhahabu.

Waziri Kairuki alisema Serikali imeamua kuwapeleka mahakamani, ili sheria ichukue mkondo wake kwa kosa la kusafirisha na kukutwa na sampuli hizo bila kibali.
Credit: Mjengwa Blog
 
WAWEKEZAJI WALISEMA YA THAMANI YA BILIONI 32 TUKASEMA WAMEDANGANYA YANA THAMANI YA BILIONI 65. LEO YAMEUZWA KWA BILIONI 22 TUNASHANGILIA HUU SI ULIMBUKENI.
hii inamaanisha unaamini alichosema waziri sayo?
 
...sugu ana hoja zenye akili kuliko mawaziri wengi wa sasa..akiwemo huyu mama....chambua hoja acha ku personalize issues.....
Mkuu kama watu wa aina yako ni tegemeo kwenye chama chenu au familia yako basi nawasikitikia kwa kumtegemea mtu anaeona Sugu ana hoja zenye akili nyingi kuliko Prof. Ndalichako. Siasa zisitusabababishie upofu wa kufikiri.
 
Wewe aliyekwwmbia kila anae comment humu JF ni CHADEMA nani!?...acha ulinganifu wa kibashite humu....btw ....CCM ndio wanaotakiwa kuishi kwa kazi maana ndio wanaong'ang'ania madarakani hata kwa wizi wa kura....

Chadena mnaishi kwa hoja na ccm wanaishi kwa kazi na ukweli.
Je kipi muhimu kwa maendeleo ya nchi?
 
Back
Top Bottom