figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 24,317
- 49,487
Na Charles William
Innocent Bashungwa amekua waziri katika wizara nyingi sana ndani ya muda mfupi, kutoka 2018 - 2022 amekua waziri katika wizara 6 tofauti.
2018 Rais Magufuli alianza kwa kumteua kuwa Naibu Waziri wa Kilimo, mwaka 2019 akamteua kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, kisha 2020 akamteua kuwa waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo. Wizara 3 ndani ya miaka mitatu.
Rais Samia tangu alipoingia Machi 2021 - Oktoba 2022, amemteua Bashungwa kuwa waziri katika wizara 3 tofauti pia. Alianza kumteua kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Januari 2022 Rais Samia akamhamishia Bashungwa katika Wizara ya TAMISEMI na juzi akamteua kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Swali la wengi ni; "kwanini kila panga pangua za mawaziri zikija Bashungwa lazima aguswe kwa kuhamishwa wizara?"
Ingawa mamlaka ya kuteua na sababu za kumteua mtu katika wadhifa fulani ni ya Rais lakini zipo nadharia kadhaa nimewaza kuhusu Bashungwa kuhamishwa kila mara, tunaweza kuzijadili;
1. Huenda Bashungwa ni waziri ambaye Marais wamekua wakiona 'ana kitu' na mwenye ujuzi wa vitu vingi hivyo NI MUHIMU awepo kwenye cabinet ili mchango wake usikosekane na ni 'kiraka' unayeweza kumpa jukumu katika wizara yoyote na akatekeleza kwa ufanisi.
2. Huenda Bashungwa ni mtendaji mzuri na mjuzi sana wa mambo LAKINI BADO mamlaka ya uteuzi haijaridhika na ufanisi katika wizara alizohudumu, hivyo kwa kuwa ana 'potential' mamlaka zinajaribu kutafuta wizara sahihi ambayo kiwango cha juu zaidi cha ubora wake kitaonekana.
3. Huenda 'Inno' amefanya kazi nzuri sana katika wizara za awali alizopita, hivyo mamlaka za uteuzi inamuhamisha wizara kila mara ili akatoe huduma nzuri pia katika maeneo mengine serikalini.
4. Huenda Bashungwa 'ana Mungu' na ana bahati/kismati, hivyo kila uteuzi ukifanyika Mungu wake anaendelea kumpigania na mamlaka za uteuzi zinaendelea kumkumbuka. Kama huamini kwenye Mungu, bahati au kismati ni vigumu kuelewa.
Atakaa muda gani katika wizara ya Ulinzi? Wengi wanaamini kwa kuwa ni mtaratibu na mtulivu sana wa akili, wizara hii itamfaa zaidi kwani haitaki makeke.
Bashungwa; miaka minne, wizara 6. Mtu kazi au bahati?
#KalamuYaCharles
MY TAKE:
Bashushungwa namchukulia kama Familia ya Taifa ya Ukoo wa Kijazi. Usimpende utampenda na ukimpenda ni sawa na umempenda tu. Kitukuu cha mtume.