Waziri Innocent Bashungwa ni Mtu kazi au bahati tu?

Anaandaliwa!! sasa kazi kwako kujua kuwa Nani!!

Unammkumbuka Dr.Husein Mwinyi enzi zake!!?

Isije ikawa calm, visionary, patriotic, intelligent and strategic akafanikisha next stage!!


Siku hizi wakubwa wanaandaa VIJANA!

Kabla hujawa wanakupitisha wizara tofauti tofauti ili upate uzoefu!!

Namtakia mafanikio KWA malengo ya wanaomuandaa!!
 
Wewe mafanikio yako ni yapi?
Kwani ukiyaelezea hayo mafanikio yake kiutendaji, utapungukiwa nini? Sasa unayaulizia mafanikio yangu mimi, yatakusaidia nini? Mimi ni mwananchi tu mvuja jasho, na pia mlipa kodi.

Hayo ya Bashungwa, ni muhimu kwangu kama mwananchi wa nchi hii kufahamu iwapo tuna waziri ambaye ni asset, au ni liability.
 
Kinachombeba huyu jamaa ni upole,unyenyekevu,heshima,usiri,si mtu wa makundi na anajitahidi kupunguza mihemko kulinganisha na wengine.

Shida kubwa aliyonayo ni kukosa ubunifu na kuna mda anakuwa mzubaifu mzubaifu fulani hivi! Pia ni mzito kufanya maamuzi mpaka ashituliwe.
Kitengo
 
Anaandaliwa!! sasa kazi kwako kujua kuwa Nani!!

Unammkumbuka Dr.Husein Mwinyi enzi zake!!?

Isije ikawa calm, visionary, patriotic, intelligent and strategic akafanikisha next stage!!


Sijui hizi wakubwa wanaandaa VIJANA!

Kabla hujawa wanakupitisha wizara tofauti tofauti ili upate uzoefu!!

Namtakia mafanikio KWA malengo ya wanaomuandaa!!
Tangu zamani vijana wanaandaliwa,na ukionekana unafaa basi hutoki barazani
 
Sioni kwanini ushangazwe na uwepo wa Bashungwa kwenye baraza la mawaziri, nakuona umeathiriwa kiakili na mfumo wa kubebana unaoendekezwa serikalini, kuwepo kwa majina yaleyale hata kama yana kashfa.

Bashungwa nikimtazama kwa muonekano wake anaonekana kuwa na sifa nyingi nzuri zinazomfanya aaminiwe na kiongozi yeyote, na wala asihitaji bahati yoyote.

- Sio mtu wa umbea/majungu.

- Haonekani kuwa na makundi, jamaa anasimama kivyake.

- Hana muda na mitandao ya kijamii ili kujitangaza/onesha kama wafanyavyo wengine.

- Hana ujuaji, kujiona hata naye ni "mtoto wa mama" kama wale visebengo wengine.

- Hana kashfa yoyote ya kuhusu upigaji kama wale wengine.

Binafsi naona uwepo wa huyu jamaa kwenye serikali ya Samia, unamsaidia Rais aaminiwe kiasi fulani kwenye utendaji wake, hasa kutokana na kuzungukwa kwake na watoto wa rafiki zake waliojaa viburi.
Na inawezekana akawa Rais one day huyu jamaa
 
Bashungwa ni MWANASIASA.
Bashungwa hana karama ya kisiasa, kuongea kama wanasiasa! Huwezi kuona intelligence yake kupitia jinsi anavyozungumza ila ana hekima kubwa, ni mtiifu, msikivu, mnyenyekevu,bingwa wa mipango ( Strategies) na exposure pia. Potential yake ni kubwa kiutendaji ila si kisiasa.

Nafikiri ndio maana ameonekana kwasasa anafaa Ulinzi maana si mwanasiasa na hana makuu! Ataweza kwenda na Generals.
 
InnoBash mtu kazi, anajua sema watu wengi wana mu underrate sana.
 
Anaandaliwa!! sasa kazi kwako kujua kuwa Nani!!

Unammkumbuka Dr.Husein Mwinyi enzi zake!!?

Isije ikawa calm, visionary, patriotic, intelligent and strategic akafanikisha next stage!!


Sijui hizi wakubwa wanaandaa VIJANA!

Kabla hujawa wanakupitisha wizara tofauti tofauti ili upate uzoefu!!

Namtakia mafanikio KWA malengo ya wanaomuandaa
 
Rais Samia akipita 2025 nahisi Bashungwa atakuwa waziri mkuu kwani sidhani atampa Kasimu mara ya tatu
Ingawa ana haiba ya majirani wetu wa Kinyarwanda ni mtiifu kwa mamlaka bila kuonyesha ambition za urais
 
Na Charles William

Innocent Bashungwa amekua waziri katika wizara nyingi sana ndani ya muda mfupi, kutoka 2018 - 2022 amekua waziri katika wizara 6 tofauti.
View attachment 2377525
2018 Rais Magufuli alianza kwa kumteua kuwa Naibu Waziri wa Kilimo, mwaka 2019 akamteua kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, kisha 2020 akamteua kuwa waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo. Wizara 3 ndani ya miaka mitatu.

Rais Samia tangu alipoingia Machi 2021 - Oktoba 2022, amemteua Bashungwa kuwa waziri katika wizara 3 tofauti pia. Alianza kumteua kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Januari 2022 Rais Samia akamhamishia Bashungwa katika Wizara ya TAMISEMI na juzi akamteua kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Swali la wengi ni; "kwanini kila panga pangua za mawaziri zikija Bashungwa lazima aguswe kwa kuhamishwa wizara?"

Ingawa mamlaka ya kuteua na sababu za kumteua mtu katika wadhifa fulani ni ya Rais lakini zipo nadharia kadhaa nimewaza kuhusu Bashungwa kuhamishwa kila mara, tunaweza kuzijadili;

1. Huenda Bashungwa ni waziri ambaye Marais wamekua wakiona 'ana kitu' na mwenye ujuzi wa vitu vingi hivyo NI MUHIMU awepo kwenye cabinet ili mchango wake usikosekane na ni 'kiraka' unayeweza kumpa jukumu katika wizara yoyote na akatekeleza kwa ufanisi.

2. Huenda Bashungwa ni mtendaji mzuri na mjuzi sana wa mambo LAKINI BADO mamlaka ya uteuzi haijaridhika na ufanisi katika wizara alizohudumu, hivyo kwa kuwa ana 'potential' mamlaka zinajaribu kutafuta wizara sahihi ambayo kiwango cha juu zaidi cha ubora wake kitaonekana.

3. Huenda 'Inno' amefanya kazi nzuri sana katika wizara za awali alizopita, hivyo mamlaka za uteuzi inamuhamisha wizara kila mara ili akatoe huduma nzuri pia katika maeneo mengine serikalini.

4. Huenda Bashungwa 'ana Mungu' na ana bahati/kismati, hivyo kila uteuzi ukifanyika Mungu wake anaendelea kumpigania na mamlaka za uteuzi zinaendelea kumkumbuka. Kama huamini kwenye Mungu, bahati au kismati ni vigumu kuelewa.

Atakaa muda gani katika wizara ya Ulinzi? Wengi wanaamini kwa kuwa ni mtaratibu na mtulivu sana wa akili, wizara hii itamfaa zaidi kwani haitaki makeke.
Bashungwa; miaka minne, wizara 6. Mtu kazi au bahati?

#KalamuYaCharles

MY TAKE:
Bashushungwa namchukulia kama Familia ya Taifa ya Ukoo wa Kijazi. Usimpende utampenda na ukimpenda ni sawa na umempenda tu. Kitukuu cha mtume.
Nafikiri tayari atakuwa kishaanza kujiona ni Presidential Material kama akina Mwigulu na January.
 
Kwani so tulikubaliana wahaya, nyaki na chaga hakuna kupewa nafasi ya urais kwakuwa Wana tribal negligence.
Yah right. Hizo ni story za mtaani.

Hata huko Zenji walisema GA Mpemba hawezi kupewa..... Then Shein akaukwaa Urais ZNZ na Maza kakalia kiti. Never say never.
 
Back
Top Bottom