Waziri Innocent Bashungwa ni Mtu kazi au bahati tu?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,483
54,852
Na Charles William

Innocent Bashungwa amekua waziri katika wizara nyingi sana ndani ya muda mfupi, kutoka 2018 - 2022 amekua waziri katika wizara 6 tofauti.
1-1664948283404.jpg

2018 Rais Magufuli alianza kwa kumteua kuwa Naibu Waziri wa Kilimo, mwaka 2019 akamteua kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, kisha 2020 akamteua kuwa waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo. Wizara 3 ndani ya miaka mitatu.

Rais Samia tangu alipoingia Machi 2021 - Oktoba 2022, amemteua Bashungwa kuwa waziri katika wizara 3 tofauti pia. Alianza kumteua kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Januari 2022 Rais Samia akamhamishia Bashungwa katika Wizara ya TAMISEMI na juzi akamteua kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Swali la wengi ni; "kwanini kila panga pangua za mawaziri zikija Bashungwa lazima aguswe kwa kuhamishwa wizara?"

Ingawa mamlaka ya kuteua na sababu za kumteua mtu katika wadhifa fulani ni ya Rais lakini zipo nadharia kadhaa nimewaza kuhusu Bashungwa kuhamishwa kila mara, tunaweza kuzijadili;

1. Huenda Bashungwa ni waziri ambaye Marais wamekua wakiona 'ana kitu' na mwenye ujuzi wa vitu vingi hivyo NI MUHIMU awepo kwenye cabinet ili mchango wake usikosekane na ni 'kiraka' unayeweza kumpa jukumu katika wizara yoyote na akatekeleza kwa ufanisi.

2. Huenda Bashungwa ni mtendaji mzuri na mjuzi sana wa mambo LAKINI BADO mamlaka ya uteuzi haijaridhika na ufanisi katika wizara alizohudumu, hivyo kwa kuwa ana 'potential' mamlaka zinajaribu kutafuta wizara sahihi ambayo kiwango cha juu zaidi cha ubora wake kitaonekana.

3. Huenda 'Inno' amefanya kazi nzuri sana katika wizara za awali alizopita, hivyo mamlaka za uteuzi inamuhamisha wizara kila mara ili akatoe huduma nzuri pia katika maeneo mengine serikalini.

4. Huenda Bashungwa 'ana Mungu' na ana bahati/kismati, hivyo kila uteuzi ukifanyika Mungu wake anaendelea kumpigania na mamlaka za uteuzi zinaendelea kumkumbuka. Kama huamini kwenye Mungu, bahati au kismati ni vigumu kuelewa.

Atakaa muda gani katika wizara ya Ulinzi? Wengi wanaamini kwa kuwa ni mtaratibu na mtulivu sana wa akili, wizara hii itamfaa zaidi kwani haitaki makeke.
Bashungwa; miaka minne, wizara 6. Mtu kazi au bahati?

#KalamuYaCharles

MY TAKE:
Bashushungwa namchukulia kama Familia ya Taifa ya Ukoo wa Kijazi. Usimpende utampenda na ukimpenda ni sawa na umempenda tu. Kitukuu cha mtume.
 
Sioni kwanini ushangazwe na uwepo wa Bashungwa kwenye baraza la mawaziri, nakuona umeathiriwa kiakili na mfumo wa kubebana unaoendekezwa serikalini, kuwepo kwa majina yaleyale hata kama yana kashfa.

Bashungwa nikimtazama kwa muonekano wake anaonekana kuwa na sifa nyingi nzuri zinazomfanya aaminiwe na kiongozi yeyote, na wala asihitaji bahati yoyote.

- Sio mtu wa umbea/majungu.

- Haonekani kuwa na makundi, jamaa anasimama kivyake.

- Hana muda na mitandao ya kijamii ili kujitangaza/onesha kama wafanyavyo wengine.

- Hana ujuaji, kujiona hata naye ni "mtoto wa mama" kama wale visebengo wengine.

- Hana kashfa yoyote ya kuhusu upigaji kama wale wengine.

Binafsi naona uwepo wa huyu jamaa kwenye serikali ya Samia, unamsaidia Rais aaminiwe kiasi fulani kwenye utendaji wake, hasa kutokana na kuzungukwa kwake na watoto wa rafiki zake waliojaa viburi.
 
Kinachombeba huyu jamaa ni upole,unyenyekevu,heshima,usiri,si mtu wa makundi na anajitahidi kupunguza mihemko kulinganisha na wengine.

Shida kubwa aliyonayo ni kukosa ubunifu na kuna mda anakuwa mzubaifu mzubaifu fulani hivi! Pia ni mzito kufanya maamuzi mpaka ashituliwe.
 
Only unyenyekevu , na pia yupo open Sana Kwa mabosi wake Ila hayupo open Kwa wengine
 
Inno anaonekana kuwa mnyenyekevu, msikivu na haonekani kuwa na makundi wala majivuno. Hivyo kubadilishwa katika Wizara zaidi ya moja katika muda mfupi sio zari wala kismati bali ni utendaji na uwajibikaji wake kayika majukumu.
 
Bashungwa hana karama ya kisiasa, kuongea kama wanasiasa! Huwezi kuona intelligence yake kupitia jinsi anavyozungumza ila ana hekima kubwa, ni mtiifu, msikivu, mnyenyekevu,bingwa wa mipango ( Strategies) na exposure pia. Potential yake ni kubwa kiutendaji ila si kisiasa.

Nafikiri ndio maana ameonekana kwasasa anafaa Ulinzi maana si mwanasiasa na hana makuu! Ataweza kwenda na Generals.
 
You are right , akiongea utamuonea huruma , hawezi kabisa ….ila mara nyingi watu ambao sio wasemaji wana uwezo mkubwa wa kufikiria na kuandika
 
Kila wizara anafeli tu ila chakufurahisha zaidi ana ngekewa(bahati).
 
Na Charles William

Innocent Bashungwa amekua waziri katika wizara nyingi sana ndani ya muda mfupi, kutoka 2018 - 2022 amekua waziri katika wizara 6 tofauti.
View attachment 2377525
2018 Rais Magufuli alianza kwa kumteua kuwa Naibu Waziri wa Kilimo, mwaka 2019 akamteua kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, kisha 2020 akamteua kuwa waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo. Wizara 3 ndani ya miaka mitatu.

Rais Samia tangu alipoingia Machi 2021 - Oktoba 2022, amemteua Bashungwa kuwa waziri katika wizara 3 tofauti pia. Alianza kumteua kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Januari 2022 Rais Samia akamhamishia Bashungwa katika Wizara ya TAMISEMI na juzi akamteua kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Swali la wengi ni; "kwanini kila panga pangua za mawaziri zikija Bashungwa lazima aguswe kwa kuhamishwa wizara?"

Ingawa mamlaka ya kuteua na sababu za kumteua mtu katika wadhifa fulani ni ya Rais lakini zipo nadharia kadhaa nimewaza kuhusu Bashungwa kuhamishwa kila mara, tunaweza kuzijadili;

1. Huenda Bashungwa ni waziri ambaye Marais wamekua wakiona 'ana kitu' na mwenye ujuzi wa vitu vingi hivyo NI MUHIMU awepo kwenye cabinet ili mchango wake usikosekane na ni 'kiraka' unayeweza kumpa jukumu katika wizara yoyote na akatekeleza kwa ufanisi.

2. Huenda Bashungwa ni mtendaji mzuri na mjuzi sana wa mambo LAKINI BADO mamlaka ya uteuzi haijaridhika na ufanisi katika wizara alizohudumu, hivyo kwa kuwa ana 'potential' mamlaka zinajaribu kutafuta wizara sahihi ambayo kiwango cha juu zaidi cha ubora wake kitaonekana.

3. Huenda 'Inno' amefanya kazi nzuri sana katika wizara za awali alizopita, hivyo mamlaka za uteuzi inamuhamisha wizara kila mara ili akatoe huduma nzuri pia katika maeneo mengine serikalini.

4. Huenda Bashungwa 'ana Mungu' na ana bahati/kismati, hivyo kila uteuzi ukifanyika Mungu wake anaendelea kumpigania na mamlaka za uteuzi zinaendelea kumkumbuka. Kama huamini kwenye Mungu, bahati au kismati ni vigumu kuelewa.

Atakaa muda gani katika wizara ya Ulinzi? Wengi wanaamini kwa kuwa ni mtaratibu na mtulivu sana wa akili, wizara hii itamfaa zaidi kwani haitaki makeke.
Bashungwa; miaka minne, wizara 6. Mtu kazi au bahati?

#KalamuYaCharles

MY TAKE:
Bashushungwa namchukulia kama Familia ya Taifa ya Ukoo wa Kijazi. Usimpende utampenda na ukimpenda ni sawa na umempenda tu. Kitukuu cha mtume.
Vinaweza kuwa ni vitu viwili; bahati na pamoja na potential ya kazi iliyo ndani ya kiongozi huyu. Kuna kitu viongozi watakuwa wanakiona ndani yake na si wale tu wanaohusika na mamlaka za uteuzi.

Mbali na hayo, "facial look" yake anaonekana ni mtu mpole mwenye hekina na anyeheshimu sana watu.

Katika kujaribu viongozi wake kuendelea kumnoa, kwa mabadiliko mengine yatakayomhusu iwapo kama yatatokea, basi napendekeza WABADILISANE WIZARA NA SULEIMAN JAFFO!
 
Ni mtu anayeaminika sana pia inaonekana hata level yake ya uadilifu ni kubwa. Sio mwongeaji sana na mtu wa showoff za mitandaoni..exposure imemjenga sana Hana ulimbukeni wa kisiasa. Atatufaa huyu mbele kwenye uraisi hekima ipo. Sio kama wale makanjanja wa Tozo na mwenzie wa nishati.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
🤣🤣🤣🤣+ mtusi naye analia na utoroshaji...!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom