Waziri Dkt. Mwigulu atoa ufafanuzi wa baadhi ya tozo alizowasilisha wakati wa Mapendekezo ya Bajeti Kuu na kuleta mkanganyiko kwa wananchi

Wameacha kukwapua pesa Kutoka kwa akaunti zetu, sasa wanazichukua kwa kisheria zaidi. Kodi ya majengo kupitia Luku ni wizi wa wazi kabisa. Kama nyumba ina mita za Luku Zaidi ya moja ina maana kila mita Itakatwa Kodi ya jengo.
Unataka maendeleo hutaki changia
 
Lipa kodi tupate pesa za kuwalipa akina Halima Mdee miposho wawapo bungeni
 
Watanzania tunataka maendeleo ila hatutaki kulipa kodi.
Je una habari kuwa wanaotafuna mabilioni ya kodi zetu bila kulala kama nzige hawalipi kodi? Ni upumbavu kuwalipisha kodi wanaohangaika juani kwa nguvu zao wakitafuta pesa huku wanasiasa na wagonga meza bungeni, wanaokula jasho letu kivulini kwenye viyoyozi, hawalipi hata senti. Inashangaza, inaudhi na inasikitisha...!
 
Wengine hata vyama vya siasa hawana wanakula mpunga wanajua mandondocha yatalipa tu
 
Yaani huyu mtu sijui kasoma uchumi upi! Yaani kila nikununua muda wa maongezi nakatwa halafu anasema siyo mzigo! Hii miradi si walisema wana hela! Mwendazake kaondoka nazo? Mbona kodi tunalipa nyingi tu! Kama vipi hiyo miradi waisitishe kama hawana hela. Mbona wao wabunge hawalipi kodi? Kwanini wao hawaonyeshi uzalendo? Uzalendo ni sisi tu wananchi?
 
Sijaona Shida hapo, pesa kidogo sana hiyo ndugu zangu tulipe Kodi nchi iende mbele
 
Tena sana!!!!
 
Hongera Sana Waziri wa Fedha, nchi yetu bado ni changa, wananchi shine tulipe Kodi...!
Yaani wewe Ndebile! Ungekuwa karibu Kofi lingekuhusu! Wao mbona hawalipi kodi? Wao wako nchi gani?
 
Angetoa na pendekezo la kupunguza mishahara yao na kuweka kodi kwenye kiwango kitakacho salia na kupunguza kiwango cha pesa kwenye kiinua mgongo ,Ili kuonesha kwa vitendo kwamba wanataka kufanikisha hiyo miradi, sio kutufinya wananchi peke yetu
 
Nyumba nilopanga tuko wapangaji wawili na kila mmoja ana mita yake sasa tutalipaje hiyo kodi ya majengo.
Hafu mita yenyewe ina jina la mpangaji wa zamani
Hiyo ni advantage kwa serikali kama nyumba itakuwa na mita zaidi ya moja, pia inajazilizia nyumba zisizokuwa na Umeme, cha muhimu kuliko vyote wigo wa mapato umepanuka.
 
Inasikitisha sana MBUNGE anapata MSHAHARA wa Sh.Mil.11 na KIINUA MGONGO cha Sh.Mil.200 na Hakatwi KODI na huo Mshahara na Kiinua Mgongo ni KODI za WANANCHI leo Anasimama MBUNGE na Kudai Wananchi Wakatwe KODI ya UZALENDO .Kama ni UZALENDO anzeni nyinyi WABUNGE wenye MISHAHARA ya MAMILIONI Kukatwa Pesa na Ziende kwenye MIRADI ya MAENDELEO Majimboni Kwenu Huo Utakuwa UZALENDO.Wananchi Wanyonge na Masikini Mnawarundikia UTITIRI wa KODI nyinyi MNASTAREHE kwa MISHAHARA MINONO na MAGARI Mazuri Hebu Waoneeni Huruma Wapiga KURA
 
Inasikitisha sana MBUNGE anapata MSHAHARA wa Sh.Mil.11 na KIINUA MGONGO cha Sh.Mil.200 na Hakatwi KODI na huo Mshahara na Kiinua Mgongo ni KODI za WANANCHI leo Anasimama MBUNGE na Kudai Wananchi Wakatwe KODI ya UZALENDO .Kama ni UZALENDO anzeni nyinyi WABUNGE wenye MISHAHARA ya MAMILIONI Kukatwa Pesa na Ziende kwenye MIRADI ya MAENDELEO Majimboni Kwenu Huo Utakuwa UZALENDO.Wananchi Wanyonge na Masikini Mnawarundikia UTITIRI wa KODI nyinyi MNASTAREHE kwa MISHAHARA MINONO na MAGARI Mazuri Hebu Waoneeni Huruma Wapiga KURA
 
Nafikiri sasa wawe wanawajibishwa. Shida yetu tumeruhusu wawe untouchables. Suala la kulipa kodi sio suala la bargaining. Ni la lazima.
Kuhusu matumizi ya kodi, wananchi tuwabane wakusanya kodi watumie kwa weledi. Wafujaji wawajibishwe na sio wanalindwa.
 
This is rubbish
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…