TANZIA Waziri Celina Ompeshi Kombani afariki dunia

Habari zilizotufikia jioni hii zinasema kwamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina-Ompeashi-Kombani (pichani), amefariki dunia leo huko India alikokuwa akipata matibabu ya saratani.-

Taarifa kutoka ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na kueleza kwamba mwili wa marehemu unategemewa kuwasili Dar es salaam siku ya Jumatatu, ambapo Bunge na Serikali zitasimamia maandalizi yote ya maziko na kumsafirisha kwa mazishi nyumbani kwa marehemu huko Mahenge ambako alikuwa Mbunge wa jimbo la Ulanga.-

bbc wametangaza mwili utaletwa jumamosi
 
Mungu awape nguvu na faraja ndugu jamaa na marafiki wa marehemu. Poleni sana wafiwa. Roho ya marehemu ipumzike kwa amani.
 
Watanzania akili zetu zimeingiliwa na kitu gani lakini? Hapa tumeletewa tanzia ya kifo ya Mtanzania mwenzetu,badala ya kuhungana na kumuombea apumzike kwa amani peponi, sisi tunatanguliza masuala ya itikadi za vyama na kejeli juu, tunajisahau kabisa kuwa kila nafsi itaonja muhuti!! Huku kama sio kuchanganyikiwa ni nini?
 
Kitu cha ajabu sana, Uzi unazungumzia msiba watu wanaingiza na mitazamo yao.
 
Dah komba na kombani wote kutoka ccm wamefariki kabla ya kushuhudia mabadiriko tarehe 25 october, mungu awalaze mahali pema!!!! Amina
 
Jamani Celina pumzika kwa Amani.Tutakosa uzungumzaji wako wenye hisia bungeni.Poleni sana wa famili,pole sana Mh.Rais
 
Back
Top Bottom