TANZIA Waziri Celina Ompeshi Kombani afariki dunia

Kingine Waache kukimbilia india wangekuwa na akili wangeboresha hospital nchini watibiwe humu humu...huko wanafata kifo tu
Kabisa. Lakini nani wa kukusikiliza kilio chako? Wameweka nta masikioni mwao
 
pole yenu wafiwa mtegemeeni Mungu na mtapata faraja ya kweli toka kwake. pumzika kwa amani mama celina.

michango ya watu humu imenifanya ni kumbuke ule ugonjwa wa Dr Mwakiembe, sikumbuki kama tuliambiwa chanzo chake kilikuwa nini hasa? tunasahau wakati mwingine malipo ni hapahapa duniani.
 
Uzima wa mtu uko mikononi mwa Mungu huyu mama was strong na appearance alikua strong vifo hutokea kutufundisha na kutukumbusha team makomeo naona wamekazania kukashifu afya ya Lowasa as if wao hawafi na wana mkataba na Mungu. Gonna too soon R.I.P mama
 
Sasa unamwambia RIP maiti kwani anakusikia? Ujumbe wowote utolewao msibani huwa ni kwa ajili ya walio hai sio maiti.Wanaotoa mambo ya Itikadi wengine kuna ujumbe wanataka kuufikisha hasa kwa wale ambao kila siku wanahubiri majukwaani kuwa Lowassa ni Mgonjwa.Kifo cha Kombani.kiwe funzo kwao kuwa ni Mungu tu ajuaye afya ya mtu na lini Atakuchukua hakuna mwingine ajuaye

Naamini kwenye quote yangu hakuna RIP hapo na kamwe situmii hiyo kitu kwangu haina maana pia. Uzi huu unatosha kusema pole kwa wafiwa. Mengine yanafaa yaanzishiwe uzi mwingine! Ahsante
 
Nasikia Lowasa alipohamia CHADEMA huyu Mama alitamka maneno mabaya sana Kwa Lowasa.Kama Kweli Alisema hayo maneno basi Malipo mi hapahapa duniani

Na Kama Kweli ALIMNENEA MANENO MABAYA LOWASA, Basi Mungu Katenda Haki, Tena Afadhari KURA ZA WANYANG'ANYI ZIMEPUNGUA.
 
Alivyokua akiongea bungeni maneno ya dhihaka dhidi ya wapinzani unawezasema labda hatakufa Acheni Mungu aitwe Mungu.ukweli mchungu.
 
Pumzika kwa aman mama komban,siasa sio uadui zisitufanye tupoteze utu wetu. Kama watanzania tujifunze uvumilivu wa kisiasa licha ya tofaut zetu za kisiasa.
 
Alikuwa mgonjwa kumbe? Mbona hawa ccm wana roho mbaya sana?hawasemi kumbe mama alienda india kutibiwa na kafia india! Wamekazania kupiga push ups na kumkebehi mzee wetu lowasa,kuanzia leo kelele hatutaki kuhusu lowasa,kumbe mna wagonjwa wenu hamsemi

Pengine wangesema tungemuombea na sala zetu zingesaidia.
 
RIP Mama Celina Kombani,
Poleni wote tulioguswa na Msiba huu.


Nasikitika Kuwapa taarifa ya kifo cha Waziri wetu, Celina Kombani kilichotokea huko India..

Celina.jpg


Celina Ompeshi Kombani (19 June 1959 - 24 September 2015) was a Tanzanian CCM politician and Member of Parliament for Ulanga East constituency since 2005.

She was the Minister of State in the President's Office for Public Service Management.
 
rip mama kombani. kamsalimie kapt komba. nakumbuka huyu mama naye alikuwa mstari wa mbele sana kuipinga katiba ya wananchi katika bunge la katiba, ijapokuwa hakuwa mtukanaji kama akina marehemu komba.
 
Daah! Mama Kombani amefariki?! Poleni wafiwa. Mama alikuwa miongoni mwa mawaziri wachache waliyoishi vuzuri na watu wote kwa upendo bila ya unafiq. RIP Celina Ompesh Kombani
 
Nasikitika sana kwa kifo chake! R.I.P. mbunge wangu! Ila kwa nini afie India?

amefia india kwa kuwa hapa kwetu hakuna hospitali za viongozi zaidi ya zile za malofa na wapumbavu. hapo ndipo ujue tofauti iliyopo kati ya malofa na watawala ( watwana na mabwana).
 
Back
Top Bottom