Waziri Bashungwa amsimamisha Mkurugenzi wa Mvomero Bw Hassan Njama Hassan kwa Ufisadi wa kutisha

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
2,552
2,184
IMG-20220420-WA0018.jpg
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Inncocent Bashungwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro, Hassani Njama Hassani kuanzia leo tarehe 20.04.2022 ili kupisha uchunguzi.

Waziri Bashungwa amechukua hatua hiyo baada ya Mkurugenzi huyo kushindwa kutekeleza maagizo aliyoyatoa wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya Tarehe 10.03.2022 kwenye Halmashauri hiyo.

Wakati wa ziara hiyo Waziri Bashungwa alibaini upotevu wa Fedha za Miradi na matumizi yasiyo sahihi ya kiasi cha shilingi milioni 231.84 katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Moringe Sokoine zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa bwalo la chakula, jiko na bweni na kumuagiza Mkurugenzi huyo kuwachukulia hatua za kiutumishi Wakuu wote wa ldara na watumishi waliohusika na ukiukwaji wa taratibu za manunuzi katika mradi huo.

Hadi kufikia leo hakuna Mkuu wa ldara yeyote ama mtumishi aliyechukuliwa hatua kufuatia agizo hilo.

Aidha, Waziri Bashungwa ameendelea kuwataka Wakurugenzi wa Halmashuri zote nchini kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo kikamilifu na kuchukua hatua za haraka pale wanapobaini ubadhifu wa fedha za umma.


Source: TAMISEMI
 
Mama hana mchezo na pesa ya Serikali kabisa,

Huwa tunasikia ubadhirifu wa mamilioni kila kukicha na watu wanaishia kufukuzwa kazi
Sasa swali fikirishi ni wangapi wamezirudisha au huwa wanagawana tena baada ya kumbana mhusika?

Maana utasikia tu Takukuru mpo hapa?
Haya mchukueni huyo

Ila baada ya hapo husikii tena kesi zao
Ni mchezo huwa wanachezi eti?
Mbona Hakuna aliefungwa miaka 30 kwa wizi wa hela zetu?
Ila majizi mengine mitaani yanakula mvua kila kukicha?
 
Yaani pamoja na madudu mengi kwenye Riport ya CAG bado kuna mtu ataamini Mkurugenzi kuadhibiwa itakua ndy ishara ya uwajibikaji serikalini.Hapa ilitakiwa ngoma ianze na Pm ang'oke mara moja halafu wachini wafuate kupopolewa.
 
Back
Top Bottom