Waziri Bashe ameukonga moyo wangu!

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,585
4,268
Nilimsikiliza Waziri Bashe sijui ilikuwa ni ufunguzi wa kiwanda cha mbolea
pamoja na mambo mengi, kwenye hotuba yake alisema; Wataalam wa ofisi ya kilimo wakae na muekezaji wamuelekeze mahitahi ya mbolea inayoendana na udongo wa maeneo tarajiwa (target market) ili azalishe mbolea inayohitajiwa sokoni na kusiwe na visingizio baadae kuwa mbolea haina ubora unaostahili
 
Pembejeo za kilimo ni bomu linalowaangamiza wakulima.

Nchi hii kila tamko likitoka basi kuna watu wenyewe watakuja kusifia tu.

Sisi Watanzania ni viumbe wa hovyo sana.
 
Na ndio sababu nimeguswa na huyu ambaye ameonesha kutambua kuwa tatizo sio pembejeo tu; Tatizo kubwa ni pembejeo sahihi
Mf: Mikoa muhimu kwa uzalishaji wa mahindi (songea, Iringa, Rukwa nk) wanajanga la udongo kuwa na Acid kutokana na matumizi ya mbolea za viwandani kwa muda mrefu. Inamaana hata ungeweka mbolea kiasi gani, bila kutengeneza mbolea sahihi kwa maendeo hayo au kutengenezewa Chokaa ya kutoa acid utakuwa hujawasaidia (hii ni kwa kitaalam zaidi, sio siasa)
 
Nilimsikiliza Waziri Bashe sijui ilikuwa ni ufunguzi wa kiwanda cha mbolea
pamoja na mambo mengi, kwenye hotuba yake alisema; Wataalam wa ofisi ya kilimo wakae na muekezaji wamuelekeze mahitahi ya mbolea inayoendana na udongo wa maeneo tarajiwa (target market) ili azalishe mbolea inayohitajiwa sokoni na kusiwe na visingizio baadae kuwa mbolea haina ubora unaostahili

Politics! Mere words, implementation? He he he! Mfanya biashara anaangalia Faida, sio aina Za udongo, labda Kama kuna government subsidies, Tanzania? He he he!
 
atapaje faida akitengeneza bidhaa isiyohitajika sokoni?
huo ushauri wa waziri ni msaada mkubwa kwenye marketing, kwa bidhaa za kawaida huo ushauri unanunuliwa( huwezi kupata bure); Labda uajiri wataalam wakufanyie market research kujua aina za udongo na mahitaji yake
 
Back
Top Bottom