Ndugu Suleman Jr, Maendeleo yapo ya aina Mbili
Economic Growth pamoja na Economic Development
Kwa kuwa hivi vyote vinahitajika sisi Tanzania tutaendelea kujenga Miundombinu ili kuboust hali ya Maisha yetu hasa maeneo yasiyofikika kule Jamii ya wengi ilipo, yaani Mikoani, Wilayani, Kata mpaka Vijijini. Huduma Muhimu kama barabara, madaraja ni sehemu kubwa ya kugusa Maendeleo ya watu (Economic Development) Japo Maendeleo ya watu yatajiashiria pale ambapo watu wanaweza kujipatia Mahitaji pasipo shida kubwa; Masoko yawepo, Wamudu Matibabu, Ada za shule walipe bila shida au upande mwingine pato la Taifa lizikave, Maji wapate bila shida kubwa, Chakula bora na cha kutosha kiwepo nyumbani na Mengineyo.
Upande wa Taifa kuingia uchumi wa kati, kupunguza utegemezi kama Madeni, kukuza Pato lake, kuwa na Bajeti Imara pamoja na kupanda Scale au thamani ili siku Moja tuwe wa Tisa Africa, tuwashushe Kenya angalau maana sisi ni wa kumi, hii ni (Economic Growth)
Kiufupi Maendeleo ya kujenga Shule nyingi tena zingine Mpya, Zahanati, Barabara, Miradi ya Maji, Reli, Mabwawa, Madaraja ni Mambo mazuri si ya kupingwa ni ya kushangiliwa na hasa wakati mwingine TUNAPOJENGA KWA PESA ZETU WENYEWE