DOKEZO Waziri aagiza mabasi 60, Kampuni ya Esther

DOKEZO Waziri aagiza mabasi 60, Kampuni ya Esther

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Endapo ni kweli, basi yaonesha wazi akili fupi za waliowengi Tanzania, hata hao elites. Yaani una hela kama hizo hukuona cha kufanya katika dunia hii mpya isipokuwa biashara 'traditional' za kizamani, nawe ni Waziri wa fedha?

Hujui kuna kununua Bitcoins au ku invest katika stock za Japan, Marekani, Australia ambazo zitakuletea maradufu ya mabasi yote hayo kwa miezi sita tu? Au kuanzisha kiwanda ukaajiri kwa muda mrefu, start up katika info technology?
 
Tatizo siyo kununua, pesa amezipata wapi na mshahara wake wajulikana? Au atuoneshe amechukua wapi mkopo? Watu wengine hata wakiibiwa waona sawa tu endapo aibaye ni Waziri! Mwizi ni mwizi tu.
Akionesha michakato yake ya kupata mahela mtatulia?😂😂😂
 
Yaani aendeshe Timu ya mpira harafu ashindwe kuagiza vibasi hivyo ?

Lini sheria ilikataza watumishi kufanya biashara? Hii mentality ya wizi kila kitu ndio inawafanya mzidi kuwa maskini ..

Nikuulize umewahi kuona wapi mbunge wa ccm ni maskini au anagombea ubunge hana pesa?

Kwa hiyo kwa akili zako mbovu kuna mtu ambae TISS hawana taarifa yake?

Ukishaanza kuwa na kacheo na hela huko kitaa lazima Tiss wakujue au hata ukiwa mtu mwenye ushawishi kwenye jamii lazima wajue..

Yaani watu Wana kampuni za ujenzi zina set kama 5 za equipments harafu unazungumzia huto tumabasi? Kuwa serious Mzee.
Kama yuko hivyo, apumzishwe tu. Anapata wapi wasaa wa kushughulikia mambo ya taifa? Ndiyo maana kila anachojua juu ya kupata revenue ni tozo. Hana wakati wa kubuni.
 
Kaka Paskali,
Unadhani ni fair waziri wa fedha kumiliki kampuni ya betting wakati wizara anayoisimamia ndiyo inayosimamia betting nchini, is it ethical ?
It depends, kama alimiliki kabla hajawa waziri na baada ya kuteuliwa kuwa waziri kule alijiuzulu kujihusisha na kampuni hiyo, hakuna tatizo.
Mhe. Jerry Solomon Sumari, alikuwa ni mmiliki wa Solomon Brokers ambaye ni wakala wa DSE na CMSA, alipoteuliwa naibu Fedha, kule alijiuzulu na kumteua mkewe.

Kama baada ya kuwa MFI ndipo akaanzisha kampuni ya betting, that is unethical
P
 
Hata kama katiba basi ni mwizi mzuri

Kuiba na kuwekeza nchini na kuongeza ajira ni kuzuri kuliko kuiba na kupeleka pesa nje uswisi nk

Mabasi 60 kila basi linakuwa na madereva wawili na wahudumu wawili jumla wanne

Nne Mara mabasi 60 ni kuwa yataongeza Ajira za watu 240

Hao 240 wana wategemezi chukulia kila mmoja anawategemezi wawili jumla ya watakaofaidika ni wao 240 jumlisha wategemezi 480 .Wataokafaidika direct na hizo ajira ni 720

Bado kuna TRA hapo wanafaidi,bado wenye nyumba za kupangisha wanafaidi, bado vituo vya mafuta vitafaidi kujaza mafuta hayo magari,bado magereji watafaidi nk

Watanzania tuache utoto tukiona wazawa wanawekeza kwenye nchi tuachane na wivu wa kijinga

Watu wabaya ni waenda kuficha pesa nje

Binafsi kama ni kweli kaagiza mabasi 60 nampongeza
Hakuna wizi mbaya au mzuri wizi ni wizi tu.

Fedha ni za wananchi sio za mtu binafsi.

Matumizi yake yanapaswa kuelekezwa kwenye huduma za kijamii na sio matumizi binafsi.
 
Watu wa aina yako ndio mlikua mkishangilia madaraja na barabara kuona yanajengwa mkijua ndio maendeleo,
Maendeleo sio barabara na masoko peke yake kuna mengi zaidi
Ndugu Suleman Jr, Maendeleo yapo ya aina Mbili

Economic Growth pamoja na Economic Development

Kwa kuwa hivi vyote vinahitajika sisi Tanzania tutaendelea kujenga Miundombinu ili kuboust hali ya Maisha yetu hasa maeneo yasiyofikika kule Jamii ya wengi ilipo, yaani Mikoani, Wilayani, Kata mpaka Vijijini. Huduma Muhimu kama barabara, madaraja ni sehemu kubwa ya kugusa Maendeleo ya watu (Economic Development) Japo Maendeleo ya watu yatajiashiria pale ambapo watu wanaweza kujipatia Mahitaji yao pasipo shida kubwa; Masoko ya mazao yao yawepo yakiwa na bei nzuri, Wamudu Matibabu, ada za shule walipe bila shida au upande mwingine pato la Taifa lizikave, Maji wapate bila shida kubwa, Chakula bora na cha kutosha kiwepo nyumbani na Mengineyo.

Upande wa Taifa kuingia uchumi wa kati, kupunguza utegemezi kama Madeni, kukuza Pato lake, kuwa na Bajeti Imara pamoja na kupanda Scale au thamani ili siku Moja tuwe wa Tisa Africa, tuwashushe Kenya angalau maana sisi ni wa kumi, hii ni (Economic Growth)

Kiufupi Maendeleo ya kujenga Shule nyingi tena zingine Mpya, Zahanati, Barabara, Miradi ya Maji, Reli, Mabwawa, Madaraja ni Mambo mazuri si ya kupingwa ni ya kushangiliwa na hasa wakati mwingine TUNAPOJENGA KWA PESA ZETU WENYEWE
 
It depends, kama alimiliki kabla hajawa waziri na baada ya kuteuliwa kuwa waziri kule alijiuzulu kujihusisha na kampuni hiyo, hakuna tatizo.
Mhe. Jerry Solomon Sumari, alikuwa ni mmiliki wa Solomon Brokers ambaye ni wakala wa DSE na CMSA, alipoteuliwa naibu Fedha, kule alijiuzulu na kumteua mkewe.

Kama baada ya kuwa MFI ndipo akaanzisha kampuni ya betting, that is unethical
P
Hata kama ali-transfer umiliki kwenda mkewe, is it ethical? Kwenye nchi zilizostaarabika, hata kuhamishia umiliki kwa mke/mme bado huwezi kuondoa conflict of interest ndiyo maana wengine either huuza share zao completely au kuamua kuachana na nafasi ya kisiasa.
 
Waziri wa fedha anaruhusiwaje kumiliki kampuni ya betting wakati wizara anayoisimamia inatengeneza policy zinazoisimamia betting? Hii nchi ni lawless.
Tangu CCM walipokuja na uvumbuzi wa kufanya siasa siyo service, na kwamba mwanasiasa aruhusiwa kufanya biashara.....ndipo nchi hii ilipoangamia.
Wamelifanya hilo makusudi na cynically. Wanajua fika katika nchi maskini ukimwekea kiongozi bakuli la ugali atalikupua tu, hata akiwa Malaika!
Hay ndiyo matokeo ya kawaida.
 
Kwa hiyo umenuna mtu kujinunulia magari?Hebu acha akili za kimasikini mkuu!Au haupendi tukalione ziwa Singidani?[emoji23][emoji23][emoji23]
Ebu na wewe ficha haibu yako kidogo basi. Yaani mtu anaagiza mabasi kwa kutumia kodi na tozo za watanzania alafu unaropoka eti akili za kimaskini! Nadhani wewe ndiyo juha kabisa!
 
Hata kama ali-transfer umiliki kwenda mkewe, is it ethical? Kwenye nchi zilizostaarabika, hata kuhamishia umiliki kwa mke/mme bado huwezi kuondoa conflict of interest ndiyo maana wengine either huuza share zao completely au kuamua kuachana na nafasi ya kisiasa.
Acheni kupoteza nda mgari yale ni ya mchaga wa rombo,
 
Acheni kumshambulia whistleblower! Yeye kapuliza kipenga TU ni juu yenu kuingia field mtuletee hayo maushahidi hapa. Acheni uvivu wa kuusaka ukweli!

Huyu sio WB Ni mmbeya. Kama kila mtu akileta habari ya kuchafua watu JF bila evidence itakuwa Chaos.
 
Back
Top Bottom