Wazee watazuia mafuriko Lowassa na kuliokoa taifa?

Ndugu,
Wewe endelea kuamini unachokiamini lakini na mimi ninacho kile ninachokifahamu kwa sababu CCM imeanza kujiandaa kwenye uchaguzi huu baada ya uchaguzi wa 2010 kumalizika.

Hii ni sawa na mwanafunzi ambaye amejiandaa vizuri kwa miaka minne kukabiliana na mtihani wa kidato cha nne ambao anategemea kufanya baada ya mwezi mmoja.

Kauli yangu iko palepale, Lowassa hashindi huu uchaguzi.

Mwanadiwani
Kama Lowasa hashindi huu uchaguzi si mtulie. Mnahangaika nini sasa? Kila kuchikicha Lowasa Lowasa. Nadhani hata usiku mkilala huwa mnaweweseka kwenye ndoto Lowasa Lowasa!
Ukweli mnaujua kuwa Lowasa ndiye rais ajae ila imekuwa ngumu kumeza ukweli huu.
La msingi hapa, nashauri wewe na wana sisiemu wenzako muanze kujiandaa kisaikologia na zaidi muanze kuhamisha makorokoro yenu pale magogoni mapema kabla Oct 25
 
hapo ndo mnapokosea mkuu,nawajua vijana wengi sana wengine wana pHD zao na wengine wana masters, achana na ambao ni darasa la saba kama ulivosema, hawavuti bangi, wana familia zao na kipato halali kabisa, lakini wanamuunga mkono Lowasa.

ukisema hakuna kijana makini anayemuunga mkono Lowasa, nina imani tafsiri ya neno makini kwako ni tofauti na tafsiri halisi tunayoijua sie.Tatizo la CCM sio Lowasa, tatizo la CCM ni Ufisadi wa viongozi, Upendeleo wa wazi kwa familia za viongozi, Rushwa kwa vyombo vya uma kama Police, Mahakama, Hospitali na huduma nyingine za jamii, Umaskini mkubwa miongoni mwa watanzania, kukosa ubunifu wa vyanzo vya mapato inayosababisha mwananchi kapuku kabisa ndo kulipa kila kodi na matajiri kuachwa, dharau kwa wananchi kutoka kwa viongozi wa serikali na CCM na pia ukosefu wa ajira kwa vijana.

Hayo hapo juu ndo yanayoiponza CCM, na kama ukijidanganya kuwa hawatakuamulia raisi hao vijana unaowaona ni wavuta bangi, basi endelea kujidanganya, siku ukipata uelewa itakuwa too late!

Asilimia kubwa ya wachangiaji wa hoja humu jamvini wana mtizamo kama wako Kamanda Moshi. Na mimi nilikuwa na mtizamo huo wa kutaka CCM ipumzishwe kwanza kwani ilifikia hali ambayo viongozi ndani ya CCM walijiita "huyu ni mwenzetu". Nilipata matumaini zaidi CHADEMA ilipoanza kupambana na ufisadi kwenye majukwaa ya siasa. Nikatoa pumzi ya auheni "mh! Hatimaye dawa ya kupambana na rushwa na ufisadi ipo CHADEMA". Kumbe nilikuwa naota ndoto za mchana maana hao waliotukanwa mafisadi ni lulu kwa CHADEMA kuingia Ikulu. Du! Kweli hati shetani anaweza kuwa malaika CHADEMA. NASEMA HAPANA KURA YANGU kwa viongozi vigeugeu na wanafiki. Ni UHUNI wa kisiasa.

Wengine wanataka tu CCM iondoke madarakani kwa kuwa imekaa muda mrefu - labda hawa pia wangetaka wazazi wao waondoke duniani ili mali waliochuma waitafune bila uangalizi. Hoja gani hii ya kipumbavu! Hao vijana wasomi (digrii za uzamili na uzamivu) wamezipata ndani ya Serikali ya CCM, au siyo!

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Last edited by a moderator:
Ukiona mgombea anatembea na wasanii 70 kwenye kampeni yake ujue hamkani si shwari...
 
Wazee na watu wengine wenye hekima hawatoacha Tanzania igeuzwe panya wa maabara ambapo viongozi walioshindwa waje kufanyia majaribio. Mbele ya wazee halitoharibika neno. Hili sina hofu nalo.

CHANZO: RaiaMwema
Mwandishi wa Makala ni Lula wa Ndali Mwananzela.

Kwa kweli umefichua siri kubwa. Ina mmaana chaguzi zote si demokrasia iliyoamua bali wazee waliamua. Huo ni ukweli kwa mifano chaguzi zote za Zanzibar "wazee" wanaamua si sanduku la kura. Hapa kwetu tume ya uchaguzi inatangaza si matokeo ya sanduku la kura.

Una sababu za msingi za kuhofia machafuko mara mtakapotumia GOLI LA MKONO. ILA ONDOA SHAKA CCM INAONDOKA NA NI BUSARA HEKIMA NA MUIAFAKA IONDOKE NA IFE.

Umri wangu kwa sasa ni miaka 66 ni mwanachama mwanzilishi wa CCM sasa ni mwanachama mfu kama tulivyo wengi Nimeamua kutumia kura yangu CCM IONDOKE MADARAKANI LIWALO NA LIWE
 
Chaliii...It doesn't matter Lowasa ataiibia nchi hii akiingia ikulu au la.....Ni Bora lowasa mmoja kuliko Majizi milioni yaliyoko CCM

I will Vote for Lowassa

Lowasa Lazima ashinde Uchaguzi huu
 
MwanaDiwani

Sisi wazee bdo tuko nsitari wa mbele kuikataa CCM huyu anazungumzia wazee wapi?! au hajafanya utafiti?!!Kwa jweli CCM imetuterekeza kabisa wazee na udanganyifu kibaao. Wengine tulikuwa wafanyakazi serikalini wa kiwango ambacho serikali ilikuwa haitowi pensheni, sasa huwezi amini kama tulikuwa wafanyakazi serikalini.

Unajua unapoona gari bovu ukiona mtu anang'ang'ania jua ana mzigo wake ndani au gari la jamaa yake wa karibu, watu kama akina Mgana Msindai si vijana na wamelishitukia kuwa hili gari bovu.

Suala la wazee unawakumbuka wale wazee wa iliyokuwa jumuia ya Africa mashariki? Kenya na Uganda walilipwa bila usumbufu hapa licha ya kushinda mahakamani wanazungushwa, wanadhulumiwa na serikali hii ya CCM, je nao wakipata nguvu ya kwenda kupiga kura watatupigia CCM? Mtoa mada kachanganyikiwa shibe imemlevya
 
Last edited by a moderator:
Tutawaadhibu tu kwa kutudharau na kuifanya TZ sehemu ya kupigia dili nawatoto wenu.
 
Kila siku mimi nawaambia ninyi Bavicha hakuna asiyeweza kuzomea,kufanya vurugu amma maandamano.Mkiachwa mnajiona washindi.Ila naona mmeanza kuchokwa.Na mtapigwa tu.Anyways nchi yetu ndogo sana na hatuna pa kwenda pakiharibika.MBOWE atakuwa dubai maana ana jumba la kifahari huko na familia yake na Lowassa ana familia yake uingereza.Sisi tuendelee kuandamana tu maana hata wazazi wetu wametuchoka,tutafute ukombozi.
Ukiwa CCM lazima uwe punguani? Lini na wapi Chadema wameua CCM? Arusha kwenye mkutano wa chadema wa kuhitimisha kampeni za madiwani lilirushwa bomu na kuwaua wananchi wasio na hatia, maandamano ya amani kupinga kuchakachuliwa matokeo ya udiwani Arusha polisi wa CCM waliwaua wananchi.

Kushindwa kuficha upumbavu wako hivi kwa matajiri wenye majumba nje ya nchi umewaona Mbowe na Lowassa tu? Ama kweli pumbavu halijifichi
 
Asilimia kubwa ya wachangiaji wa hoja humu jamvini wana mtizamo kama wako Kamanda Moshi. Na mimi nilikuwa na mtizamo huo wa kutaka CCM ipumzishwe kwanza kwani ilifikia hali ambayo viongozi ndani ya CCM walijiita "huyu ni mwenzetu". Nilipata matumaini zaidi CHADEMA ilipoanza kupambana na ufisadi kwenye majukwaa ya siasa. Nikatoa pumzi ya auheni "mh! Hatimaye dawa ya kupambana na rushwa na ufisadi ipo CHADEMA". Kumbe nilikuwa naota ndoto za mchana maana hao waliotukanwa mafisadi ni lulu kwa CHADEMA kuingia Ikulu. Du! Kweli hati shetani anaweza kuwa malaika CHADEMA. NASEMA HAPANA KURA YANGU kwa viongozi vigeugeu na wanafiki. Ni UHUNI wa kisiasa.

Wengine wanataka tu CCM iondoke madarakani kwa kuwa imekaa muda mrefu - labda hawa pia wangetaka wazazi wao waondoke duniani ili mali waliochuma waitafune bila uangalizi. Hoja gani hii ya kipumbavu! Hao vijana wasomi (digrii za uzamili na uzamivu) wamezipata ndani ya Serikali ya CCM, au siyo!

TAFAKARI CHUKUA HATUA
,
asante mkuu kwa kuyaona haya, lakini unaposema hizo degree wamezipata ndani ya serikali ya ccm inaweka kama vile ilikuwa ni msaada wanapewa...Je CCm hawakuwa wanakusanya kodi?na isitoshe hao hao viongoz wengi ndo wanapata misamaha ya kodi na ndio wenye kupewa huduma za bure nyingi kwa kodi hiyo hiyo ya walalahoi. kusoma na hata kupata matibabu sio jambo la hiari kwa serikali kulifanya, maadamu wanachukua kodi basi hayo yote ni lazima wayafanye.
Swali ni je yanafanywa kwa kiwango tunachochangia kodi?jibu ni hapana.
Hoja ya ufisadi kwa walioenda Chadema, nikimaanisha hapa Lowasa, nimejaribu kufuatilia lakini sijapata uthibitisho pasi na shaka wa tuhuma hizo. Aliyoyasema Slaa hii juzi kati hakukuwa na kingine kipya ambacho hakusema Mwakyembe ile 2008 Bungeni.
Swali ni kama Lowasa ni fisadi kwa nini hajachukuliwa hatua mpaka leo?huu ushahid anao nani?na kwa nini serikali yetu kama ipo adilifu iwalinde wala rushwa?
kwa nini kuna hofu kubwa upinzani wasichukue uongozi?kuna nini huko kwa serikali kinachofichwa hivo?tupeni ukweli, sie ambao hatuamua rasmi kura yetu iwe wapi ili tujue, otherwise hujaniconvice hata kidogo kwa nini niichague ccm na sio upinzani.
CCm imefail mambo mengi sana, na ndio iliyopo madarakani miaka yote hii, kwa hivo nataka majibu ya mapungufu yao na kwa nini mara hii wanaamini wataweza.
Hivi wanyama wetu si walipakiwa kwa ndege iliyotua kwa uwanja wa serikali?au ulikuwa uchawi ule macho ya kawaida hayawezi ona?
 
CCM walikuwa wanatoa hela mfukoni mwao , tumia akili kufikiria siyo masaburi, na suala la ufisadi toka mwaka 2008 Lowassa alipotoka madarakani na ufisadi ukaisha serikalini? Aliyetoa maamuzi ya mwisho kwenye sakata la Richmond na ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la mawaziri kwa nini hamtaki kumuwajibisha Kikwete kwa hili? Wana CCM unafiki ndiyo unawafanya muonekane mataahira.

Mwaka huu Lowassa atosha kama mimba ziwatoke tu maana hamna namna nyingine.
 
Last edited by a moderator:
Vijana wenyewe ni vijana wavuta bangi,wafanya fujo,wazomeaji na wapenda vurugu wamenunuliwa na fisadi EL eti watuamulie rais.HAITATOKEA KAMWE.Hakuna kijana makini anayemuunga mkono FISADI LOWASSA.Kelele za BAVICHA na 4U Movement zisiwape shida.

Unalaumu ulipo angukia, angalia ulipojikwaa! Hao kama ni wavuta bangi, malofa, wapumbavu, hawajui watendalo na kila aina ya mapungufu...Mwisho wa siku ni Raia wa Tg na Zenj! Huna haki wala sababu ya kuwavua Uraia!
Solution ni Muafaka wa Kitaifa! Hapo Tutaelewana na Kusameheana!
lakini kwa kudharauliana, kuzodoana, kutambuana kwa njia ya walio nacho na walalahoi...Huu utulivu utapotea! Muda utasema!
 
,
asante mkuu kwa kuyaona haya, lakini unaposema hizo degree wamezipata ndani ya serikali ya ccm inaweka kama vile ilikuwa ni msaada wanapewa...Je CCm hawakuwa wanakusanya kodi?na isitoshe hao hao viongoz wengi ndo wanapata misamaha ya kodi na ndio wenye kupewa huduma za bure nyingi kwa kodi hiyo hiyo ya walalahoi. kusoma na hata kupata matibabu sio jambo la hiari kwa serikali kulifanya, maadamu wanachukua kodi basi hayo yote ni lazima wayafanye.
Swali ni je yanafanywa kwa kiwango tunachochangia kodi?jibu ni hapana.
Hoja ya ufisadi kwa walioenda Chadema, nikimaanisha hapa Lowasa, nimejaribu kufuatilia lakini sijapata uthibitisho pasi na shaka wa tuhuma hizo. Aliyoyasema Slaa hii juzi kati hakukuwa na kingine kipya ambacho hakusema Mwakyembe ile 2008 Bungeni.
Swali ni kama Lowasa ni fisadi kwa nini hajachukuliwa hatua mpaka leo?huu ushahid anao nani?na kwa nini serikali yetu kama ipo adilifu iwalinde wala rushwa?
kwa nini kuna hofu kubwa upinzani wasichukue uongozi?kuna nini huko kwa serikali kinachofichwa hivo?tupeni ukweli, sie ambao hatuamua rasmi kura yetu iwe wapi ili tujue, otherwise hujaniconvice hata kidogo kwa nini niichague ccm na sio upinzani.
CCm imefail mambo mengi sana, na ndio iliyopo madarakani miaka yote hii, kwa hivo nataka majibu ya mapungufu yao na kwa nini mara hii wanaamini wataweza.
Hivi wanyama wetu si walipakiwa kwa ndege iliyotua kwa uwanja wa serikali?au ulikuwa uchawi ule macho ya kawaida hayawezi ona?

Natamani ningekuwa na majibu ya maswali yako, ila kama umekuwa ukifuatilia mada na hoja humu jamvini kuba majibu tosha. Hata hao mamluki wamekaririwa, bado wakiwa CCM, wakitoa sifa kedekede za CCM - au ndo hiyo unayosema hata hawa walinufanikiwa na misamaha kodi!!!

Nimekwisha andika mada humu jamvini kuhusu misingi ya maendeleo, kama alivyofalsafa Mwl Nyerere - ambaye wengi tunapenda kumnukuu sana kwa machache ya kukidhi haja zetu - kwamba ni Ardhi, Watu, Siasa safi na Uongozi bora. Kinachokosekana ni uongozi bora tu kama ulivyobainisha.

Kama hujaamua, fikiri kidogo tu na kujiuliza kati ya wagombea Urais 8 ni yupi ana sifa za kiongozi wa kuaminika! Nami nipe sababu za unayemwamini, niweze kutumia kura yangu vizuri. Ni kura yangu, yako, yake na wao itakayotupa Rais kwa miaka 5 ijayo.

Sikubaliani na hoja isiyo na mshiko ya kutaka kuiondoa CCM kama vile sera zake ni mbaya.
 
kwa maelezo haya hapa juu na hasa mstari wa mwisho ni wazi kuwa wewe ni ccm, na huwezi ona mapungufu yake kwa maana tayari una mahaba nayo.
ccm haiwezi kujivua lawama kwa matatizo ya kujitakia yaliyopo nchini hivi sasa, wala haiwezi kukataa kuyalea na kuwalea viongozi wabovu kabisa mpaka hivi leo, na hili hasaa ndio changamoto kwetu...kuwa itabadilika vipi ilihali wale wachafu woote bado wapo ndani yake na tena wana maamuzi?
ni lipi jipya amabalo walishindwa kufanya kwenye miaka yote hamsini waliyokuwa madarakani na eti sasa wataweza? why walishindwa at first place?
 
Mwananzela kwa taarifa yako mm ni above 60.Naifahamu vizuri nchi yetu toka uongozi wa awamu ya kwanza hadi sasa lakini nami bado naona kwa sasa kuna umuhimu CCM kuwekwa pembeni.
Mwananchi anahitaji kuona serkali inayojali kumpatia unafuu ktk maisha yake ya kila sku.Sasa kama kila uchao unasema afadhari ya jana huku akilipa kodi kwenye bidhaa anazotumia kila siku unategemea.achukue uamuzi upi.Ccm. si kwamba hawajui ni kwa nn vijana wanadai ni heri kuchagua hata jiwe.Wanaelewa ila badala ya kujikita kutueleza ni kwa nn miaka yote 50+ tuko hivi wanajitia kuja na ahadi hizo hizo ambazo wameshindwa kuzitekeleza.
Kwa taarifa tu ni kwamba wananchi walitakiwa wawe wameshaipumzisha ccm muda mrefu ila ulofa na upumbavu wetu ndo ulisababisha wawepo hadi sasa nahatimaye mwaka huu tunaambiwa kabisa bila chenga kwamba sisi ni malofa na wapumbavu.
CCm vilevile haitaki kusoma alama za nyakati kwamba hapo nyuma watu walikuwa hawajitambui ila kwa sasa kwa shule zao za kayumba hizo hizo walau baadhi ya watanzania wametambua kwamba wanadanganywa sasa hawataki kudanganywa tena.Hii inajidhihirisha kwamba ccm bado inapendwa vijijini tu ambako kuna kundi kubwa ambalo bado watu hawajui kwamba wanalipa kodi kwa ajili ya kupewa hudumana serkali.Yetu macho tuombeane tufike Oct. tuone kama kundi kubwa bado liko gizani au kwenye mwanga.MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
 
KUNA msemo kuwa; “Penye wazee haliharibiki neno”. Msemo huu unatumiwa sana kama tahadhari kwenye masuala ambayo yanaweza kuhusisha vijana au watu wengi ambao labda hawana umri wa kuweza kuwa na hekima ya mambo fulani fulani. Msemo huu unatumiwa zaidi katika kutafuta namna ya kusuluhisha jambo ambalo linaonekana bila ushauri na hekima ya wazee basi linaelekea kubaya.

Ninaamini msemo huu utakuwa kweli katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu hasa baada ya makundi ya vijana kuonekana bila kutaka kutafakari, kufikiri au hata kujiuliza maswali wameamua tu “liwalo na liwe” na sasa wako tayari kulipeleka taifa mikononi mwa kundi la viongozi ambao uongozi wao tayari umeshaonesha madhara makubwa.

Utakuwa kweli kwa sababu baada ya Lowassa kuingizwa Chadema na kupewa ugombea wa urais na hatimaye kusababisha mvurugano mwingine kwenye chama hicho kama aliousababisha na kuuacha ndani ya CCM. Makundi ya vijana hasa wanaonekana kumfurahia wakiamini kuwa nafasi ya kuiondoa CCM madarakani imefika.

Ni kweli kuwa taifa letu linahitaji mabadiliko makubwa ya kiutawala na wasomaji wangu wanaweza kukumbuka vizuri tu kuwa nimeliandika hili mara nyingi katika miaka hii ya mwamko wa kisiasa nchini. Mabadiliko haya hata hivyo yanaonekana sasa hivi yanalazimishwa kubebwa na mtu ambaye hajawahi kuyasimamia, kuyazungumzia au hata kuonesha kuwa anayajua. Lakini vijana wetu wanaonekana hawajali haya yote kwani wao sasa “wameamua” kuiondoa CCM madarakani “liwalo na liwe”.

Na kinachotisha zaidi ni kuwa vijana – wengine ni watu wenye akili tu (za darasani au vinginevyo) – hawana sababu ya msingi ya kwa nini wanamtaka Lowassa kuwa Rais wao zaidi ya matamanio yao ya kuona CCM inaondolewa madarakani. Imefika mahali hata ukiwauliza kwa nini wanamtaka Lowassa hawaoni hata aibu au kusita kwani wanasema tu “hakuna sababu sisi tunataka CCM iondoke!”.

Na wapo wasomi kabisa na watu ambao vinginevyo unaweza kuamini ni makini na wao pia wamedandia treni hili la Lowassa na wao pia hawana sababu wakisema tu “watu wamechoka” na hivyo basi kutokana na kuchoka basi wako tayari kufanya uamuzi yenye hatari.

Kuna sababu ya kwa nini kwa mfano, madereva wa malori wanatakiwa wapewe muda wa kupumzika hasa kama wana safari zile za masafa marefu. Hii ni kwa sababu dereva hata awe bora kiasi gani kama hajapumzika vya kutosha basi yuko hatarini kusababisha ajali na ajali nyingi za malori makubwa au mabasi zinatokana na madereva kutokulala vizuri au kupumzika na hivyo wanapokuwa barabarani wanakuwa wachovu.

Mtu aliyechoka hapaswi kufanya uamuzi mgumu wenye matokeo katika maisha yake kwani anaweza kujidhuru mwenyewe au kudhuru watu wengine. Watanzania waliochoka na utawala wa CCM hawapaswi kufanya uamuzi wa kumkumbatia Lowassa kwa sababu “wamechoka” kwani hilo peke yake linapaswa kuwa sababu ya kufikiria mara mbili kama wanastahili hata kufanya uamuzi huo.

Watanzania hawa waliopigika katika miaka hii hamsini leo hii wanaonekana kama wamepata nafasi ya pekee ya kuiondoa CCM kiulaini na hivyo hawataki kuipoteza. Ukiwasikiliza mashabiki hawa wa Lowassa utaona kuwa wengi wao wamefikia mahali pa kusema kuwa “hata kama ni fisadi, au kiongozi mbaya sisi tutamchagua tu’’. Wengine wamefikia hata kusema kuwa “bora jiwe kuliko CCM” na wanazungumza hivi wakiamini wanazungumza kwa akili kabisa.

Na hapa ndipo ninapoona kuwa – na wananchi wasije kushangaa Oktoba 25 Lowassa akianguka vibaya – Wazee wa Tanzania watakapoingilia kati na kuliokoa taifa kutokana uamuzi wa watu wenye maumivu, waliochoka na ambao kutokana na mapenzi fulani hivi kwa mtu wao hawawezi kufikiri vizuri.

Wazee wataweza kabisa na ninaamini wanasababu ya kuwaangalia hawa vijana wasije kuliingiza taifa kwenye matatizo kama vijana wa mataifa mengine walivyofanya wakiamini wanaleta mabadiliko. “Mabadiliko” yanatokana na msukumo wa hisia (emotional pressure) ni mabadiliko ya hatari kwani hisia hizo zinapoisha (na hisia huisha) mtu anaweza kukaa na kuanza kujuta; lakini kujuta kwa uchaguzi kama huu kutadumu miaka mitano au kumi!

Sidhani kama taifa letu na wazee wetu wanaweza kucheza kamari hiyo na kuona nchi itakuwaje miaka kumi baadaye. Wazee na watoto ndio wanadhurika zaidi yanapotokea mabadiliko makubwa au migongano ambayo haitoisha na hivyo ni kwa maslahi yao wao wenyewe (wazee) na watoto au wajukuu wao kuweza kuleta “neno” zuri la kuzuia mabadiliko yanayosukumwa na hisia ambayo inaonekana makundi ya vijana yanashabikia. Hili ni muhimu kueleweka kwani sasa hivi simulizi (narrative) ambayo ipo mitaani ni imani (msingi wake picha za nyomi) kuwa Lowassa atashinda na endapo hatoshinda basi CCM itakuwa imeibakura.

Hii ina maana kuwa – na hapa mtu anisome mara mbili – kuna uwezekano mkubwa sana wa machafuko endapo Lowassa hatoshinda kwani tayari makundi ya vijana yanaamini tayari ni mshindi. Ambacho vijana wengi hawajui ni kuwa ni wazee wa Tanzania ambao mara zote wamekuwa wakiamua matokeo ya uchaguzi – siyo vijana; ni wazee.

Ni wazee kwa sababu hawa hutawaona kwa wingi katika hamasa za mikutano ya kisiasa au maandamano lakini siku ya uchaguzi kwa sababu hakuna purukushani nyingi watajikongoja wenyewe na wengi wanapiga kura mapema na kuamua hatima ya uchaguzi.

Nina uhakika wa asilimia mia moja kuwa endapo siku ya uchaguzi wazee wengi wataamua kulinda nchi yao na kutoacha viongozi kama Lowassa na wale waliomuingiza kushika hatima ya nchi basi Lowassa siyo tu atashindwa, bali atashindwa na hatoamini; na nina uhakika atajiondoa Chadema mapema asubuhi kwani ndoto yake haitotimia.

Endapo wazee wataamua kukaa pembeni na kuacha vijana wajifunze somo kwa matatizo basi siyo tu watakuwa wanashindwa kutimiza wajibu wao wa kuilinda jamii yao na kuhakikisha wanakirithisha kizazi kijacho nchi ambayo inaweza kuendelezwa.

Wazee na watu wengine wenye hekima hawatoacha Tanzania igeuzwe panya wa maabara ambapo viongozi walioshindwa waje kufanyia majaribio. Mbele ya wazee halitoharibika neno. Hili sina hofu nalo.

CHANZO: RaiaMwema
Mwandishi wa Makala ni Lula wa Ndali Mwananzela.
huyu ni mpuuzi kwa kutuona atujui kwanini tuna mchagua Lowasa .kwa chama cha chadema aka ukawa.aoni tunacho tegemea kupata .kama katiba ya wananchi.elimu bure..kupitiwa upya mikataba ya kifisadi.kuondoa genge la wezi ccm.walio nyamazia kama sio ndio walioiba.epa.meremeta.escrow na ataa Richmond.Mwananzela umetuzarau sana .unatakiwa utuombe msamaha wananchi .na zaidi huu upuuzi na umbea wako peleka ccm.sisi huku ni mabadiliko Lowasa.
 
Vijana wenyewe ni vijana wavuta bangi,wafanya fujo,wazomeaji na wapenda vurugu wamenunuliwa na fisadi EL eti watuamulie rais.HAITATOKEA KAMWE.Hakuna kijana makini anayemuunga mkono FISADI LOWASSA.Kelele za BAVICHA na 4U Movement zisiwape shida.
Hivi mnavyosema vijana wavuta bangi mnamaanisha nini.!?
1.kwamba vijana rundo lote wanavuta bangi.?
2.Mimi na rafiki zangu ni wasomi wazuri tu na tuna kazi nzuri tu lakini ni wafuasi wa ukawa.!? Unaona kuna shida hapo..?!
3.kwa nini ccm ina vijana wenye dharau na kiburi sana ..? Halafu hamna kitu na ni weupe kichwani.!?
 
kwa maelezo haya hapa juu na hasa mstari wa mwisho ni wazi kuwa wewe ni ccm, na huwezi ona mapungufu yake kwa maana tayari una mahaba nayo.
ccm haiwezi kujivua lawama kwa matatizo ya kujitakia yaliyopo nchini hivi sasa, wala haiwezi kukataa kuyalea na kuwalea viongozi wabovu kabisa mpaka hivi leo, na hili hasaa ndio changamoto kwetu...kuwa itabadilika vipi ilihali wale wachafu woote bado wapo ndani yake na tena wana maamuzi?
ni lipi jipya amabalo walishindwa kufanya kwenye miaka yote hamsini waliyokuwa madarakani na eti sasa wataweza? why walishindwa at first place?

Kamanda, mbona tunazunguka kwenye suala moja hilohilo na huji na jibu niridhike! Nimehoji hawa waliotoka CCM na kukumbatiwa na UKAWA walifanya nini wakiwa ndani ya Serikali ya CCM ambayo kwa kauli yako "haiwezi kujivua lawama kwa matatizo ya kujitakia yaliyopo nchini hivi sasa". Yawezekana sauti yao ya mabadiliko haikusikilizwa, kama ni hivyo kweli, kwa nini hawakuondoka mapema badala yake waliomba tena uongozi ndani ya chama hicohicho, na matokeo ni kukatwa. Kama unaamini ni wanamabadiliko na walitaka kufanya hayo mabadiliko wakiwa ndani ya CCM, amini pia waliobaki humo wanaweza kufanya mabadiliko. Mabadiliko ya kwanza ni kuwakata wasio waadilifu, yaani mamluki wanaonekana lulu UKAWA kwa sasa.
 
KUNA msemo kuwa; “Penye wazee haliharibiki neno”. Msemo huu unatumiwa sana kama tahadhari kwenye masuala ambayo yanaweza kuhusisha vijana au watu wengi ambao labda hawana umri wa kuweza kuwa na hekima ya mambo fulani fulani. Msemo huu unatumiwa zaidi katika kutafuta namna ya kusuluhisha jambo ambalo linaonekana bila ushauri na hekima ya wazee basi linaelekea kubaya.

Ninaamini msemo huu utakuwa kweli katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu hasa baada ya makundi ya vijana kuonekana bila kutaka kutafakari, kufikiri au hata kujiuliza maswali wameamua tu “liwalo na liwe” na sasa wako tayari kulipeleka taifa mikononi mwa kundi la viongozi ambao uongozi wao tayari umeshaonesha madhara makubwa.

Utakuwa kweli kwa sababu baada ya Lowassa kuingizwa Chadema na kupewa ugombea wa urais na hatimaye kusababisha mvurugano mwingine kwenye chama hicho kama aliousababisha na kuuacha ndani ya CCM. Makundi ya vijana hasa wanaonekana kumfurahia wakiamini kuwa nafasi ya kuiondoa CCM madarakani imefika.

Ni kweli kuwa taifa letu linahitaji mabadiliko makubwa ya kiutawala na wasomaji wangu wanaweza kukumbuka vizuri tu kuwa nimeliandika hili mara nyingi katika miaka hii ya mwamko wa kisiasa nchini. Mabadiliko haya hata hivyo yanaonekana sasa hivi yanalazimishwa kubebwa na mtu ambaye hajawahi kuyasimamia, kuyazungumzia au hata kuonesha kuwa anayajua. Lakini vijana wetu wanaonekana hawajali haya yote kwani wao sasa “wameamua” kuiondoa CCM madarakani “liwalo na liwe”.

Na kinachotisha zaidi ni kuwa vijana – wengine ni watu wenye akili tu (za darasani au vinginevyo) – hawana sababu ya msingi ya kwa nini wanamtaka Lowassa kuwa Rais wao zaidi ya matamanio yao ya kuona CCM inaondolewa madarakani. Imefika mahali hata ukiwauliza kwa nini wanamtaka Lowassa hawaoni hata aibu au kusita kwani wanasema tu “hakuna sababu sisi tunataka CCM iondoke!”.

Na wapo wasomi kabisa na watu ambao vinginevyo unaweza kuamini ni makini na wao pia wamedandia treni hili la Lowassa na wao pia hawana sababu wakisema tu “watu wamechoka” na hivyo basi kutokana na kuchoka basi wako tayari kufanya uamuzi yenye hatari.

Kuna sababu ya kwa nini kwa mfano, madereva wa malori wanatakiwa wapewe muda wa kupumzika hasa kama wana safari zile za masafa marefu. Hii ni kwa sababu dereva hata awe bora kiasi gani kama hajapumzika vya kutosha basi yuko hatarini kusababisha ajali na ajali nyingi za malori makubwa au mabasi zinatokana na madereva kutokulala vizuri au kupumzika na hivyo wanapokuwa barabarani wanakuwa wachovu.

Mtu aliyechoka hapaswi kufanya uamuzi mgumu wenye matokeo katika maisha yake kwani anaweza kujidhuru mwenyewe au kudhuru watu wengine. Watanzania waliochoka na utawala wa CCM hawapaswi kufanya uamuzi wa kumkumbatia Lowassa kwa sababu “wamechoka” kwani hilo peke yake linapaswa kuwa sababu ya kufikiria mara mbili kama wanastahili hata kufanya uamuzi huo.

Watanzania hawa waliopigika katika miaka hii hamsini leo hii wanaonekana kama wamepata nafasi ya pekee ya kuiondoa CCM kiulaini na hivyo hawataki kuipoteza. Ukiwasikiliza mashabiki hawa wa Lowassa utaona kuwa wengi wao wamefikia mahali pa kusema kuwa “hata kama ni fisadi, au kiongozi mbaya sisi tutamchagua tu’’. Wengine wamefikia hata kusema kuwa “bora jiwe kuliko CCM” na wanazungumza hivi wakiamini wanazungumza kwa akili kabisa.

Na hapa ndipo ninapoona kuwa – na wananchi wasije kushangaa Oktoba 25 Lowassa akianguka vibaya – Wazee wa Tanzania watakapoingilia kati na kuliokoa taifa kutokana uamuzi wa watu wenye maumivu, waliochoka na ambao kutokana na mapenzi fulani hivi kwa mtu wao hawawezi kufikiri vizuri.

Wazee wataweza kabisa na ninaamini wanasababu ya kuwaangalia hawa vijana wasije kuliingiza taifa kwenye matatizo kama vijana wa mataifa mengine walivyofanya wakiamini wanaleta mabadiliko. “Mabadiliko” yanatokana na msukumo wa hisia (emotional pressure) ni mabadiliko ya hatari kwani hisia hizo zinapoisha (na hisia huisha) mtu anaweza kukaa na kuanza kujuta; lakini kujuta kwa uchaguzi kama huu kutadumu miaka mitano au kumi!

Sidhani kama taifa letu na wazee wetu wanaweza kucheza kamari hiyo na kuona nchi itakuwaje miaka kumi baadaye. Wazee na watoto ndio wanadhurika zaidi yanapotokea mabadiliko makubwa au migongano ambayo haitoisha na hivyo ni kwa maslahi yao wao wenyewe (wazee) na watoto au wajukuu wao kuweza kuleta “neno” zuri la kuzuia mabadiliko yanayosukumwa na hisia ambayo inaonekana makundi ya vijana yanashabikia. Hili ni muhimu kueleweka kwani sasa hivi simulizi (narrative) ambayo ipo mitaani ni imani (msingi wake picha za nyomi) kuwa Lowassa atashinda na endapo hatoshinda basi CCM itakuwa imeibakura.

Hii ina maana kuwa – na hapa mtu anisome mara mbili – kuna uwezekano mkubwa sana wa machafuko endapo Lowassa hatoshinda kwani tayari makundi ya vijana yanaamini tayari ni mshindi. Ambacho vijana wengi hawajui ni kuwa ni wazee wa Tanzania ambao mara zote wamekuwa wakiamua matokeo ya uchaguzi – siyo vijana; ni wazee.

Ni wazee kwa sababu hawa hutawaona kwa wingi katika hamasa za mikutano ya kisiasa au maandamano lakini siku ya uchaguzi kwa sababu hakuna purukushani nyingi watajikongoja wenyewe na wengi wanapiga kura mapema na kuamua hatima ya uchaguzi.

Nina uhakika wa asilimia mia moja kuwa endapo siku ya uchaguzi wazee wengi wataamua kulinda nchi yao na kutoacha viongozi kama Lowassa na wale waliomuingiza kushika hatima ya nchi basi Lowassa siyo tu atashindwa, bali atashindwa na hatoamini; na nina uhakika atajiondoa Chadema mapema asubuhi kwani ndoto yake haitotimia.

Endapo wazee wataamua kukaa pembeni na kuacha vijana wajifunze somo kwa matatizo basi siyo tu watakuwa wanashindwa kutimiza wajibu wao wa kuilinda jamii yao na kuhakikisha wanakirithisha kizazi kijacho nchi ambayo inaweza kuendelezwa.

Wazee na watu wengine wenye hekima hawatoacha Tanzania igeuzwe panya wa maabara ambapo viongozi walioshindwa waje kufanyia majaribio. Mbele ya wazee halitoharibika neno. Hili sina hofu nalo.

CHANZO: RaiaMwema
Mwandishi wa Makala ni Lula wa Ndali Mwananzela.

huu upumbavu wapelekeeni mama zenu na ulaf wenu huo
 
Back
Top Bottom