Wazee watazuia mafuriko Lowassa na kuliokoa taifa?

Wazee watazuia mafuriko Lowassa na kuliokoa taifa?

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Posts
5,536
Reaction score
2,268
KUNA msemo kuwa; “Penye wazee haliharibiki neno”. Msemo huu unatumiwa sana kama tahadhari kwenye masuala ambayo yanaweza kuhusisha vijana au watu wengi ambao labda hawana umri wa kuweza kuwa na hekima ya mambo fulani fulani. Msemo huu unatumiwa zaidi katika kutafuta namna ya kusuluhisha jambo ambalo linaonekana bila ushauri na hekima ya wazee basi linaelekea kubaya.

Ninaamini msemo huu utakuwa kweli katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu hasa baada ya makundi ya vijana kuonekana bila kutaka kutafakari, kufikiri au hata kujiuliza maswali wameamua tu “liwalo na liwe” na sasa wako tayari kulipeleka taifa mikononi mwa kundi la viongozi ambao uongozi wao tayari umeshaonesha madhara makubwa.

Utakuwa kweli kwa sababu baada ya Lowassa kuingizwa Chadema na kupewa ugombea wa urais na hatimaye kusababisha mvurugano mwingine kwenye chama hicho kama aliousababisha na kuuacha ndani ya CCM. Makundi ya vijana hasa wanaonekana kumfurahia wakiamini kuwa nafasi ya kuiondoa CCM madarakani imefika.

Ni kweli kuwa taifa letu linahitaji mabadiliko makubwa ya kiutawala na wasomaji wangu wanaweza kukumbuka vizuri tu kuwa nimeliandika hili mara nyingi katika miaka hii ya mwamko wa kisiasa nchini. Mabadiliko haya hata hivyo yanaonekana sasa hivi yanalazimishwa kubebwa na mtu ambaye hajawahi kuyasimamia, kuyazungumzia au hata kuonesha kuwa anayajua. Lakini vijana wetu wanaonekana hawajali haya yote kwani wao sasa “wameamua” kuiondoa CCM madarakani “liwalo na liwe”.

Na kinachotisha zaidi ni kuwa vijana – wengine ni watu wenye akili tu (za darasani au vinginevyo) – hawana sababu ya msingi ya kwa nini wanamtaka Lowassa kuwa Rais wao zaidi ya matamanio yao ya kuona CCM inaondolewa madarakani. Imefika mahali hata ukiwauliza kwa nini wanamtaka Lowassa hawaoni hata aibu au kusita kwani wanasema tu “hakuna sababu sisi tunataka CCM iondoke!”.

Na wapo wasomi kabisa na watu ambao vinginevyo unaweza kuamini ni makini na wao pia wamedandia treni hili la Lowassa na wao pia hawana sababu wakisema tu “watu wamechoka” na hivyo basi kutokana na kuchoka basi wako tayari kufanya uamuzi yenye hatari.

Kuna sababu ya kwa nini kwa mfano, madereva wa malori wanatakiwa wapewe muda wa kupumzika hasa kama wana safari zile za masafa marefu. Hii ni kwa sababu dereva hata awe bora kiasi gani kama hajapumzika vya kutosha basi yuko hatarini kusababisha ajali na ajali nyingi za malori makubwa au mabasi zinatokana na madereva kutokulala vizuri au kupumzika na hivyo wanapokuwa barabarani wanakuwa wachovu.

Mtu aliyechoka hapaswi kufanya uamuzi mgumu wenye matokeo katika maisha yake kwani anaweza kujidhuru mwenyewe au kudhuru watu wengine. Watanzania waliochoka na utawala wa CCM hawapaswi kufanya uamuzi wa kumkumbatia Lowassa kwa sababu “wamechoka” kwani hilo peke yake linapaswa kuwa sababu ya kufikiria mara mbili kama wanastahili hata kufanya uamuzi huo.

Watanzania hawa waliopigika katika miaka hii hamsini leo hii wanaonekana kama wamepata nafasi ya pekee ya kuiondoa CCM kiulaini na hivyo hawataki kuipoteza. Ukiwasikiliza mashabiki hawa wa Lowassa utaona kuwa wengi wao wamefikia mahali pa kusema kuwa “hata kama ni fisadi, au kiongozi mbaya sisi tutamchagua tu’’. Wengine wamefikia hata kusema kuwa “bora jiwe kuliko CCM” na wanazungumza hivi wakiamini wanazungumza kwa akili kabisa.

Na hapa ndipo ninapoona kuwa – na wananchi wasije kushangaa Oktoba 25 Lowassa akianguka vibaya – Wazee wa Tanzania watakapoingilia kati na kuliokoa taifa kutokana uamuzi wa watu wenye maumivu, waliochoka na ambao kutokana na mapenzi fulani hivi kwa mtu wao hawawezi kufikiri vizuri.

Wazee wataweza kabisa na ninaamini wanasababu ya kuwaangalia hawa vijana wasije kuliingiza taifa kwenye matatizo kama vijana wa mataifa mengine walivyofanya wakiamini wanaleta mabadiliko. “Mabadiliko” yanatokana na msukumo wa hisia (emotional pressure) ni mabadiliko ya hatari kwani hisia hizo zinapoisha (na hisia huisha) mtu anaweza kukaa na kuanza kujuta; lakini kujuta kwa uchaguzi kama huu kutadumu miaka mitano au kumi!

Sidhani kama taifa letu na wazee wetu wanaweza kucheza kamari hiyo na kuona nchi itakuwaje miaka kumi baadaye. Wazee na watoto ndio wanadhurika zaidi yanapotokea mabadiliko makubwa au migongano ambayo haitoisha na hivyo ni kwa maslahi yao wao wenyewe (wazee) na watoto au wajukuu wao kuweza kuleta “neno” zuri la kuzuia mabadiliko yanayosukumwa na hisia ambayo inaonekana makundi ya vijana yanashabikia. Hili ni muhimu kueleweka kwani sasa hivi simulizi (narrative) ambayo ipo mitaani ni imani (msingi wake picha za nyomi) kuwa Lowassa atashinda na endapo hatoshinda basi CCM itakuwa imeibakura.

Hii ina maana kuwa – na hapa mtu anisome mara mbili – kuna uwezekano mkubwa sana wa machafuko endapo Lowassa hatoshinda kwani tayari makundi ya vijana yanaamini tayari ni mshindi. Ambacho vijana wengi hawajui ni kuwa ni wazee wa Tanzania ambao mara zote wamekuwa wakiamua matokeo ya uchaguzi – siyo vijana; ni wazee.

Ni wazee kwa sababu hawa hutawaona kwa wingi katika hamasa za mikutano ya kisiasa au maandamano lakini siku ya uchaguzi kwa sababu hakuna purukushani nyingi watajikongoja wenyewe na wengi wanapiga kura mapema na kuamua hatima ya uchaguzi.

Nina uhakika wa asilimia mia moja kuwa endapo siku ya uchaguzi wazee wengi wataamua kulinda nchi yao na kutoacha viongozi kama Lowassa na wale waliomuingiza kushika hatima ya nchi basi Lowassa siyo tu atashindwa, bali atashindwa na hatoamini; na nina uhakika atajiondoa Chadema mapema asubuhi kwani ndoto yake haitotimia.

Endapo wazee wataamua kukaa pembeni na kuacha vijana wajifunze somo kwa matatizo basi siyo tu watakuwa wanashindwa kutimiza wajibu wao wa kuilinda jamii yao na kuhakikisha wanakirithisha kizazi kijacho nchi ambayo inaweza kuendelezwa.

Wazee na watu wengine wenye hekima hawatoacha Tanzania igeuzwe panya wa maabara ambapo viongozi walioshindwa waje kufanyia majaribio. Mbele ya wazee halitoharibika neno. Hili sina hofu nalo.

CHANZO: RaiaMwema
Mwandishi wa Makala ni Lula wa Ndali Mwananzela.
 
Vijana wenyewe ni vijana wavuta bangi,wafanya fujo,wazomeaji na wapenda vurugu wamenunuliwa na fisadi EL eti watuamulie rais.HAITATOKEA KAMWE.Hakuna kijana makini anayemuunga mkono FISADI LOWASSA.Kelele za BAVICHA na 4U Movement zisiwape shida.
 
Vijana wenyewe ni vijana wavuta bangi,wafanya fujo,wazomeaji na wapenda vurugu wamenunuliwa na fisadi EL eti watuamulie rais.HAITATOKEA KAMWE.Hakuna kijana makini anayemuunga mkono FISADI LOWASSA.Kelele za BAVICHA na 4U Movement zisiwape shida.
Ndugu,
Lowassa hawezi kuwa Rais wa Tanzania.

Mbio zake za sakafuni zitaishia ukingoni.
 
Vijana wenyewe ni vijana wavuta bangi,wafanya fujo,wazomeaji na wapenda vurugu wamenunuliwa na fisadi EL eti watuamulie rais.HAITATOKEA KAMWE.Hakuna kijana makini anayemuunga mkono FISADI LOWASSA.Kelele za BAVICHA na 4U Movement zisiwape shida.

hapo ndo mnapokosea mkuu,nawajua vijana wengi sana wengine wana pHD zao na wengine wana masters, achana na ambao ni darasa la saba kama ulivosema, hawavuti bangi, wana familia zao na kipato halali kabisa, lakini wanamuunga mkono Lowasa.

ukisema hakuna kijana makini anayemuunga mkono Lowasa, nina imani tafsiri ya neno makini kwako ni tofauti na tafsiri halisi tunayoijua sie.Tatizo la CCM sio Lowasa, tatizo la CCM ni Ufisadi wa viongozi, Upendeleo wa wazi kwa familia za viongozi, Rushwa kwa vyombo vya uma kama Police, Mahakama, Hospitali na huduma nyingine za jamii, Umaskini mkubwa miongoni mwa watanzania, kukosa ubunifu wa vyanzo vya mapato inayosababisha mwananchi kapuku kabisa ndo kulipa kila kodi na matajiri kuachwa, dharau kwa wananchi kutoka kwa viongozi wa serikali na CCM na pia ukosefu wa ajira kwa vijana.

Hayo hapo juu ndo yanayoiponza CCM, na kama ukijidanganya kuwa hawatakuamulia raisi hao vijana unaowaona ni wavuta bangi, basi endelea kujidanganya, siku ukipata uelewa itakuwa too late!
 
Ndugu,
Lowassa hawezi kuwa Rais wa Tanzania.

Mbio zake za sakafuni zitaishia ukingoni.

mkuu heshima kwako, naamini hiyo ni kauli tu ya kisiasa as uamuzi wa mwisho upo mikononi mwa watanzania. kusema ni mbio za sakafuni kunatufanya sie tulio neutral tujiulize mara mbili mbili, uchaguzi huu wanaochagua ni wananchi au tumeshapangiwa nani atatuongoza?
Lowasa na Magufuli wote wana nafasi sawa ya kushinda...hakuna aliye kwenye mbio za sakafuni kati yao...!!Ndicho nachoamini...
 
MwanaDiwani

Sisi wazee bdo tuko nsitari wa mbele kuikataa CCM huyu anazungumzia wazee wapi?! au hajafanya utafiti?!!Kwa jweli CCM imetuterekeza kabisa wazee na udanganyifu kibaao. Wengine tulikuwa wafanyakazi serikalini wa kiwango ambacho serikali ilikuwa haitowi pensheni, sasa huwezi amini kama tulikuwa wafanyakazi serikalini.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo lenu ninyi wanaccm hamjielewi kwa sasa kila kitu Lowassa mbona kuna mauchafu kibao yametokea baada ya Lowassa kutoka madarakani? Hamuyasemi mfano Escrow waliopewa pesa kwenye Bank ya Stanbinc mbona imebaki kitendawili mpk leo,acheni upotoshaji,watanzania tuchague wenyewe na c kubabaishwa na maneno yenu ya chuki dhidi ya LOWASSA mpende msipende LOWASSA ndo Rais wetu.
 
Wazee wamepigika miaka yote,wamekuwa wakidanganywa na CCM eti matibabu bure wakati wakifika hospital wanalipia,wazee tunaowatunza sisi vijana huku vijijini wanasema CCM ya sasa inahitaji kupumzishwa,ila sijui wazee unaowaongelea ni wanamna gani..Nasema tunahitaji mabadiliko nje ya CCM.
 
Wazee wanaowasema ni wahovyo yaani hawaendi mikutanoni kusikilza SERA ZA WAGOMBEA lakini siku ya kupga kura wachague CCM eti ndio Maamuzi ya busara..CCM mnatia aibu,Lowasa kawashika pabaya
 
Hivi unajua kwamba mwaka huu vijana ndio wengi waliojiandikisha? Miaka ya nyuma ndio ilikuwa wazee ndo wengi ila mwaka huu hamtaamini kitakachotokea, sasa hivi hata mvutabangi ana kikatio chake
Pia kumbuka
Kura ya mvutabangi/teja/au mnywa viroba mmoja = kura ya Magufuli au ya kikwete
Hamna kura ya Veto.
 
Mwanadiwani, mimi nadhani mwaka ngoja tu tumpe Lowasa liwalo na liwe.
 
mkuu heshima kwako, naamini hiyo ni kauli tu ya kisiasa as uamuzi wa mwisho upo mikononi mwa watanzania. kusema ni mbio za sakafuni kunatufanya sie tulio neutral tujiulize mara mbili mbili, uchaguzi huu wanaochagua ni wananchi au tumeshapangiwa nani atatuongoza?
Lowasa na Magufuli wote wana nafasi sawa ya kushinda...hakuna aliye kwenye mbio za sakafuni kati yao...!!Ndicho nachoamini...
Ndugu,
Wewe endelea kuamini unachokiamini lakini na mimi ninacho kile ninachokifahamu kwa sababu CCM imeanza kujiandaa kwenye uchaguzi huu baada ya uchaguzi wa 2010 kumalizika.

Hii ni sawa na mwanafunzi ambaye amejiandaa vizuri kwa miaka minne kukabiliana na mtihani wa kidato cha nne ambao anategemea kufanya baada ya mwezi mmoja.

Kauli yangu iko palepale, Lowassa hashindi huu uchaguzi.
 
Kamanda Moshi binafsi nikiona majina ya hii hata kabla hujaweka maoni yako nayajua.Maana ajenda yenu inajulikana tangu Uhuru.Tatizo lenu jingine mna vichwa ambavyo ni "One direction-programmed".Unazungumzia Upendeleo,rushwa ndani ya CCM.Mbona ninyi chama Hakina demokrasia hata fake,ufisadi wa ruzuku na misaada ndo usiseme.Chama mmebebana ndugu wachagga tupu then eti na nyie mnaona madhaifu ya wengine.Mnajitoa sana akili ndo maana nasema hakuna kijana makini anayewaunga mkono labda anayetoka Arusha na Moshi.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu,
Wewe endelea kuamini unachokiamini lakini na mimi ninacho kile ninachokifahamu kwa sababu CCM imeanza kujiandaa kwenye uchaguzi huu baada ya uchaguzi wa 2010 kumalizika.

Hii ni sawa na mwanafunzi ambaye amejiandaa vizuri kwa miaka minne kukabiliana na mtihani wa kidato cha nne ambao anategemea kufanya baada ya mwezi mmoja.

Kauli yangu iko palepale, Lowassa hashindi huu uchaguzi.

Sisi wazee Tumeshaamua kura zetu kwa Lowasa tuu
 
Sijaona wa kumzuia lowasa wazee sawa na uji unakuunguza huku unakupa shibe
 
Back
Top Bottom