Wazee watazuia mafuriko Lowassa na kuliokoa taifa?

Wazee watazuia mafuriko Lowassa na kuliokoa taifa?

2nahitaji mabadiliko na wazee wengi ninaewafahamu wapo na mimi
 
Mimi nadhani this time kura za madiwani, mbunge, rais zote zitangazwe sehemu mahalia, pale pale alipopigiwa kura ili tume isifanye udanganyifu.
2010 kura za rais walikataa zisiwe zinatangazwa
 
Hao wazee watumie busara zao hizo ila tusiombane hela ya kula huko mabarabarani!Tanzania ni nchi ya 91 kati ya nchi 96 zinzojali wazee,sasa hapo wanataka kutumia busara ipi?
Watanzania tusidanganyike na vituzo uchwara ambavyo hupaishwa sana,ukiona tz tumepata tuzo hata ya moja utawala bora basi ujue majirani zetu na nchi za Africa wameshazoa za kutosha moaka wanasema tuwape na wale!Kiufupi hata ni bora taiga lijiongoze kuliko hili dudu ccm!
 
Ndugu,
Wewe endelea kuamini unachokiamini lakini na mimi ninacho kile ninachokifahamu kwa sababu CCM imeanza kujiandaa kwenye uchaguzi huu baada ya uchaguzi wa 2010 kumalizika.

Hii ni sawa na mwanafunzi ambaye amejiandaa vizuri kwa miaka minne kukabiliana na mtihani wa kidato cha nne ambao anategemea kufanya baada ya mwezi mmoja.

Kauli yangu iko palepale, Lowassa hashindi huu uchaguzi.

Lowassa ameanza kujiandaa lini?
 
Kwani wazee unaozungumzia ni kuanzia umri gani? Na je ni asilimia ngapi ya wapiga kura takribani milioni 24? Fanya analysis ya maana.
 
Najisikia uchungu sana ninapoona mtu anaejitoa ufahamu na kujisahaulisha maovu ya Sisiem. Kuna jamaa hapo juu kasema eti sisiem walijiandaa kwa uchaguzi mara baada ya 2010., realy??? Mliwahi kuwaza Magufuli atakua ndo mgombea wenu?? Na kwaakili yako unafikiri UKAWA walianza mbio hizi baada ya nyinyi kumkata EL?? Natamani nitukane sana ila ngoja nigugumie tu, ninachotaka kuwaambia kua hii ni nchi yetu wooooote, nyinyi wenye nacho na sisi makapuku.. nyinyi wezi na sisi wavuta bangi.. All coins are equally..!!!
 
Jisemee nafsi yako. Wewe na nani?

Usiweke fikra zako kama ndiyo mwanvuli wa fikra za Wazee wote.
Kanisemea na mimi. Lowassa anatosha. Waambie hao wazee wenu wa Lumumba wakilazimisha ushindi kweli patachimbika tumechoka kuona upumbavu wa unaowaita wazee ukiendelea. Tanzania bila Ccm inawezekana sana tu.
 
Mwengine nae nilisoma comment yake jana anasema Roma aliandika ule wimbo akiwa amekunywa Kiroba,.. ngoja niwafumbue macho gwandas, MACHAFU huonekana MASAFI yakiwepo, muda mrefu sana mmetuaminisha kua upinzani ni fujo.. ila kwa mnayofanya kule dodoma Amini na waambieni yanatuumiza sana Watanzania, ambao nyinyi mnaona sisi ni wavuta bangi(Jamaica wanatajirika kutokana na zao hili).

Watanzania wanauchungu mwingi sana ni vile wanakosa mahali pa kuanika uchungu wao, msanii anaakisi jamii inayomzunguka, Roma hawezi kuimba tu from no where, anaimba kitu kilichopo ktk jamii, Roma ni aina ya Panya aliejitolea kumvika Paka kengele.. Tunaumia sana hamjui tu.. tumechoka zile Ndiyoooooooooooooooooooo..... tumechoka zile mheshimiwa mbunge Nimesema toka nje....

.. Na zaidi tumechoka zile humu bungeni mimi ndo mkubwa wenuuuuuu..... Ndo sababu mwisho wa siku tunasema bora jiwe kuliko sisiem... Bora tufe tukiwa tunajaribu kujikwamua.. Mfumo wenu wa uongozi umejaa magumashi.. ukiritimba, mko slow, nyodo, dharau, kujisikia, uvivu, tamaa, na kukumbatia uchama badala ya utaifa kwanza..
 
Wazee wamepungua sana. kwanza hawana huduma za afya na chakula. Halafu ndio wapambe wa CCm. Kama CCM inawajali si ingewasadia hata hizo penseni zao? Wakiambiwa adui yao ni magamba hawaelewi, mwisho wake wanaishia mmoja mmoja kabla ya muda wao. Hatudangayiki. Wazee kwisha na ccm kwisha habari yake.
 
Kamanda Moshi binafsi nikiona majina ya hii hata kabla hujaweka maoni yako nayajua.Maana ajenda yenu inajulikana tangu Uhuru.Tatizo lenu jingine mna vichwa ambavyo ni "One direction-programmed".Unazungumzia Upendeleo,rushwa ndani ya CCM.Mbona ninyi chama Hakina demokrasia hata fake,ufisadi wa ruzuku na misaada ndo usiseme.Chama mmebebana ndugu wachagga tupu then eti na nyie mnaona madhaifu ya wengine.Mnajitoa sana akili ndo maana nasema hakuna kijana makini anayewaunga mkono labda anayetoka Arusha na Moshi.
kuangalia jina tena id fake ya JF na kuwa na hitimisho kuwa huyo mtu anatoka wapi ni ufinyu wa fikra mkuu. sitoki huko unapokutaja wala sina chimbuko la huko. na hii inaendelea kudhihirisha ni kiasi gani umekosa hoja na kuanza kubagua watu.
Mimi kama mwananchi na walio wengi pia hatuoni serikali zilizopita kama zilifanya kazi ya kutosha kwenye kuondoa umaskini, kupambana na rushwa, kuongeza vyanzo vya mapato na pia kutengeneza ajira mpya.
unapoongelea ufisadi wa chadema kwenye ruzuku, nyie ndo mpo madarakani na sheria mwasimamia nyie kwa nini msiwawajibishe? huu ndo muendelezo wa uzembe utakaowagharimu hata kwa uchaguzi huu.
Magufuli atafanya nini kipya ambacho hakikufanywa na Kikwete au Mkapa? haya ndo tungependa kusikia na kuyachambua, lakini kuwaita wasiomuunga mkono Magufuli na CCM sio vijana makini, hakika kunakufanya uonekane mtu usiyefikiria vizuri.
 
Naona kalishwa mihela ya kutosha....wakati wa wazee kuifanya nchi yao umepita na wametufikisha hapa tulipo...now we take comand of our country as it is our time.. generation to come will judge us not the baby boom generation...it is time for the millenial to shine...to hell with the rullimg party
 
Wasiwasi wa nini hao wanaomtaka Low as a ni watanzania pia na hiyo ndio demokrasia kama kura zitatosha wapewe nafasi tuone kasi yao katika kutupeleka mbele.
 
Tulianza na Mungu,Tutaendelea na Mungu na Tutamaliza safari na Mungu,Hakuna awezaye kumshinda Mungu hata hao wazee wanatambua

taifa hili kwasasa liko mikononi mwa MUNGU mwenyewe
 
Ni wazee kwa sababu hawa hutawaona kwa wingi katika hamasa za mikutano ya kisiasa au maandamano lakini siku ya uchaguzi kwa sababu hakuna purukushani nyingi watajikongoja wenyewe na wengi wanapiga kura mapema na kuamua hatima ya uchaguzi.

tanzania-population-pyramid-2014.gif


Idadi ya wazee (miaka 50 na zaidi) - takribani milioni 2.5

Idadi ya Vijana (miaka 18-35) - Takribani milioni 7

Idadi ya Watu wa umri wa makamo (36-50) Takribani milioni 2

Nadhani Lula aangalie tena hiyo conclusion yake. Kwa mantiki hii ratio ya watu wa makamo;wazee;vijana ni kama 1;1;3. tukiwagawa watu wa umri wa kati nusu kwa nusu kwa "wazee" na vijana", tunapata ratio ya 1.5;3.5. Kwenye watu "milioni 24" waliojiandikisha (Hiyo takwimu hapo juu haionyeshi wanatoka wapi), tiasuume wazee wote wasimpigie Lowassa ina maana Lowassa hatapata kura milioni 7.2. Tukiassume pia kuwa nusu ya vijana tu wampigie Lowassa, basi atapata kura 16.8m x 50% = 8.4m

Ina maana kama wazee wote wataenda kupiga kura na wasimchague Lowassa, kisha nusu ya vijana tu wakaenda kupiga na kumchagua Lowassa, Lowassa bado atashinda.

ila kiuhalisia
Sio vijana wote watamchagua Lowassa

Sio wazee wote hawatamchagua Lowassa

Sio wazee wote wataenda kupiga kura

Kwa mwamko ulioonekana mwaka huu, huenda zaidi ya nusu ya vijana wataenda kupiga kura
 
tanzania-population-pyramid-2014.gif


Idadi ya wazee (miaka 50 na zaidi) - takribani milioni 2.5

Idadi ya Vijana (miaka 18-35) - Takribani milioni 7

Idadi ya Watu wa umri wa makamo (36-50) Takribani milioni 2

Nadhani Lula aangalie tena hiyo conclusion yake. Kwa mantiki hii ratio ya watu wa makamo;wazee;vijana ni kama 1;1;3. tukiwagawa watu wa umri wa kati nusu kwa nusu kwa "wazee" na vijana", tunapata ratio ya 1.5;3.5. Kwenye watu "milioni 24" waliojiandikisha (Hiyo takwimu hapo juu haionyeshi wanatoka wapi), tiasuume wazee wote wasimpigie Lowassa ina maana Lowassa hatapata kura milioni 7.2. Tukiassume pia kuwa nusu ya vijana tu wampigie Lowassa, basi atapata kura 16.8m x 50% = 8.4m

Ina maana kama wazee wote wataenda kupiga kura na wasimchague Lowassa, kisha nusu ya vijana tu wakaenda kupiga na kumchagua Lowassa, Lowassa bado atashinda.

ila kiuhalisia
Sio vijana wote watamchagua Lowassa

Sio wazee wote hawatamchagua Lowassa

Sio wazee wote wataenda kupiga kura

Kwa mwamko ulioonekana mwaka huu, huenda zaidi ya nusu ya vijana wataenda kupiga kura



Asante.Mkuu Tuko.
Mkuu Ben Saanane kalamu zingine ni kama hoja hii na amini umeisoma!
UKAWA na CDM mfike mahali mchukue hatua muhimu kila kona katika kutoa elimu kama mlivyofanya kwenye suala la ufisadi hata hizi hoja nyepesi zinatakiwa kujibiwa kwa ufasaha.

cc Tumaini Makene.

 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom