Wazee watazuia mafuriko Lowassa na kuliokoa taifa?

Unajua unapoona gari bovu ukiona mtu anang'ang'ania jua ana mzigo wake ndani au gari la jamaa yake wa karibu, watu kama akina Mgana Msindai si vijana na wamelishitukia kuwa hili gari bovu.

Suala la wazee unawakumbuka wale wazee wa iliyokuwa jumuia ya Africa mashariki? Kenya na Uganda walilipwa bila usumbufu hapa licha ya kushinda mahakamani wanazungushwa, wanadhulumiwa na serikali hii ya CCM, je nao wakipata nguvu ya kwenda kupiga kura watatupigia CCM? Mtoa mada kachanganyikiwa shibe imemlevya

Baba awa ni vijana wanao tegemea chama hapa mjini. Wakubwa wanapiga dili wanawakatia kitu kidogo.

Leo wamengangania lowassa lakini hawatuambii. EPA.KAGODA.MEREMETA.KIWIRA.ESCROW.TWIGA.TEMBO. Ni nani anausika?

Mbaya zaidi ESCROW mpaka pesa zinakwenda tolewa STANBIC BANK mchana kweupe na watu wanajulikana. CCM hili hawasemi.

Wanakuja na vituhuma vya mwaka 2008 richmond?

Safari hii halitasalia jiwe juu ya jiwe ccm lazima mwondoke. Tunakwenda kuchoma kichaka chenu kwenye sanduku la kura.

Sasa kazi kwenu ninyi mnao tegemea mafisadi kuishi mjini, mtafute kazi za kufanya wenye nchi tumesha amua. Ni bora fisadi mmoja kuliko mafisadi 1000 waliopo ndani ya chama cha mapinduzi.
 
Hivi mnavyosema vijana wavuta bangi mnamaanisha nini.!?
1.kwamba vijana rundo lote wanavuta bangi.?
2.Mimi na rafiki zangu ni wasomi wazuri tu na tuna kazi nzuri tu lakini ni wafuasi wa ukawa.!? Unaona kuna shida hapo..?!
3.kwa nini ccm ina vijana wenye dharau na kiburi sana ..? Halafu hamna kitu na ni weupe kichwani.!?

tabia uambukiza. Wamesha ambukizwa kiburi na dharau na chama cha mapinduzi. Si ulimwona mkapa? Alivyo baba ndivyo na mtoto alivyo.
 
Ndugu,
Lowassa hawezi kuwa Rais wa Tanzania.

Mbio zake za sakafuni zitaishia ukingoni.

chief, the stats below are likely to interest or rather disappoint you and the like....

image.jpg
 
Ccm wamekata tamaa,hawajui kuwa asilimia kubwa ni vijana subirini tuwashikishe adabu.
 
Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia karibia 70+ ya watu waliojiandikisha kupiga kura ni vijana kuanzia miaka 18 - 45 ... Sasa hao wazee uliowataja kuiokoa ccm ni asilimia 20 tu. Niwashauri tu, kuliko kuwatusi hawa vijana ni bora mrudi muwashawishi kwa hoja labda watawaelewa ... Muda bado upo.
 
Unalaumu ulipo angukia, angalia ulipojikwaa! Hao kama ni wavuta bangi, malofa, wapumbavu, hawajui watendalo na kila aina ya mapungufu...Mwisho wa siku ni Raia wa Tg na Zenj! Huna haki wala sababu ya kuwavua Uraia!
Solution ni Muafaka wa Kitaifa! Hapo Tutaelewana na Kusameheana!
lakini kwa kudharauliana, kuzodoana, kutambuana kwa njia ya walio nacho na walalahoi...Huu utulivu utapotea! Muda utasema!

Kwahiyo utulivu ukipotea unadhani "Who is going to lose?" Vijana mihemko itawafikisha pabaya.Narudia Lowassa atakuwa nyumbani kwake uingereza na familia yake.Mbowe atakuwa nyumbani kwake Dubai na familia yake.Wengine watakuwa wanahudhuria kesi The Hague ingawa watashinda.Wewe na wenye akili finyu wenzenu mtakuwa kaburini muda huo.
 
Wazee wenyewe 2.4 nchi ni sensa ya 2012 vijana 1100000 watoto 6 m 35 to 40 waliobaki na wote kura kwa lowassa warioba mkapa na mwenyekiti wa mwalimu foundation wana rekodi za ufisadi
 
KUNA msemo kuwa; “Penye wazee haliharibiki neno”. Msemo huu unatumiwa sana kama tahadhari kwenye masuala ambayo yanaweza kuhusisha vijana au watu wengi ambao labda hawana umri wa kuweza kuwa na hekima ya mambo fulani fulani. Msemo huu unatumiwa zaidi katika kutafuta namna ya kusuluhisha jambo ambalo linaonekana bila ushauri na hekima ya wazee basi linaelekea kubaya.

Ninaamini msemo huu utakuwa kweli katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu hasa baada ya makundi ya vijana kuonekana bila kutaka kutafakari, kufikiri au hata kujiuliza maswali wameamua tu “liwalo na liwe” na sasa wako tayari kulipeleka taifa mikononi mwa kundi la viongozi ambao uongozi wao tayari umeshaonesha madhara makubwa.

Utakuwa kweli kwa sababu baada ya Lowassa kuingizwa Chadema na kupewa ugombea wa urais na hatimaye kusababisha mvurugano mwingine kwenye chama hicho kama aliousababisha na kuuacha ndani ya CCM. Makundi ya vijana hasa wanaonekana kumfurahia wakiamini kuwa nafasi ya kuiondoa CCM madarakani imefika.

Ni kweli kuwa taifa letu linahitaji mabadiliko makubwa ya kiutawala na wasomaji wangu wanaweza kukumbuka vizuri tu kuwa nimeliandika hili mara nyingi katika miaka hii ya mwamko wa kisiasa nchini. Mabadiliko haya hata hivyo yanaonekana sasa hivi yanalazimishwa kubebwa na mtu ambaye hajawahi kuyasimamia, kuyazungumzia au hata kuonesha kuwa anayajua. Lakini vijana wetu wanaonekana hawajali haya yote kwani wao sasa “wameamua” kuiondoa CCM madarakani “liwalo na liwe”.

Na kinachotisha zaidi ni kuwa vijana – wengine ni watu wenye akili tu (za darasani au vinginevyo) – hawana sababu ya msingi ya kwa nini wanamtaka Lowassa kuwa Rais wao zaidi ya matamanio yao ya kuona CCM inaondolewa madarakani. Imefika mahali hata ukiwauliza kwa nini wanamtaka Lowassa hawaoni hata aibu au kusita kwani wanasema tu “hakuna sababu sisi tunataka CCM iondoke!”.

Na wapo wasomi kabisa na watu ambao vinginevyo unaweza kuamini ni makini na wao pia wamedandia treni hili la Lowassa na wao pia hawana sababu wakisema tu “watu wamechoka” na hivyo basi kutokana na kuchoka basi wako tayari kufanya uamuzi yenye hatari.

Kuna sababu ya kwa nini kwa mfano, madereva wa malori wanatakiwa wapewe muda wa kupumzika hasa kama wana safari zile za masafa marefu. Hii ni kwa sababu dereva hata awe bora kiasi gani kama hajapumzika vya kutosha basi yuko hatarini kusababisha ajali na ajali nyingi za malori makubwa au mabasi zinatokana na madereva kutokulala vizuri au kupumzika na hivyo wanapokuwa barabarani wanakuwa wachovu.

Mtu aliyechoka hapaswi kufanya uamuzi mgumu wenye matokeo katika maisha yake kwani anaweza kujidhuru mwenyewe au kudhuru watu wengine. Watanzania waliochoka na utawala wa CCM hawapaswi kufanya uamuzi wa kumkumbatia Lowassa kwa sababu “wamechoka” kwani hilo peke yake linapaswa kuwa sababu ya kufikiria mara mbili kama wanastahili hata kufanya uamuzi huo.

Watanzania hawa waliopigika katika miaka hii hamsini leo hii wanaonekana kama wamepata nafasi ya pekee ya kuiondoa CCM kiulaini na hivyo hawataki kuipoteza. Ukiwasikiliza mashabiki hawa wa Lowassa utaona kuwa wengi wao wamefikia mahali pa kusema kuwa “hata kama ni fisadi, au kiongozi mbaya sisi tutamchagua tu’’. Wengine wamefikia hata kusema kuwa “bora jiwe kuliko CCM” na wanazungumza hivi wakiamini wanazungumza kwa akili kabisa.

Na hapa ndipo ninapoona kuwa – na wananchi wasije kushangaa Oktoba 25 Lowassa akianguka vibaya – Wazee wa Tanzania watakapoingilia kati na kuliokoa taifa kutokana uamuzi wa watu wenye maumivu, waliochoka na ambao kutokana na mapenzi fulani hivi kwa mtu wao hawawezi kufikiri vizuri.

Wazee wataweza kabisa na ninaamini wanasababu ya kuwaangalia hawa vijana wasije kuliingiza taifa kwenye matatizo kama vijana wa mataifa mengine walivyofanya wakiamini wanaleta mabadiliko. “Mabadiliko” yanatokana na msukumo wa hisia (emotional pressure) ni mabadiliko ya hatari kwani hisia hizo zinapoisha (na hisia huisha) mtu anaweza kukaa na kuanza kujuta; lakini kujuta kwa uchaguzi kama huu kutadumu miaka mitano au kumi!

Sidhani kama taifa letu na wazee wetu wanaweza kucheza kamari hiyo na kuona nchi itakuwaje miaka kumi baadaye. Wazee na watoto ndio wanadhurika zaidi yanapotokea mabadiliko makubwa au migongano ambayo haitoisha na hivyo ni kwa maslahi yao wao wenyewe (wazee) na watoto au wajukuu wao kuweza kuleta “neno” zuri la kuzuia mabadiliko yanayosukumwa na hisia ambayo inaonekana makundi ya vijana yanashabikia. Hili ni muhimu kueleweka kwani sasa hivi simulizi (narrative) ambayo ipo mitaani ni imani (msingi wake picha za nyomi) kuwa Lowassa atashinda na endapo hatoshinda basi CCM itakuwa imeibakura.

Hii ina maana kuwa – na hapa mtu anisome mara mbili – kuna uwezekano mkubwa sana wa machafuko endapo Lowassa hatoshinda kwani tayari makundi ya vijana yanaamini tayari ni mshindi. Ambacho vijana wengi hawajui ni kuwa ni wazee wa Tanzania ambao mara zote wamekuwa wakiamua matokeo ya uchaguzi – siyo vijana; ni wazee.

Ni wazee kwa sababu hawa hutawaona kwa wingi katika hamasa za mikutano ya kisiasa au maandamano lakini siku ya uchaguzi kwa sababu hakuna purukushani nyingi watajikongoja wenyewe na wengi wanapiga kura mapema na kuamua hatima ya uchaguzi.

Nina uhakika wa asilimia mia moja kuwa endapo siku ya uchaguzi wazee wengi wataamua kulinda nchi yao na kutoacha viongozi kama Lowassa na wale waliomuingiza kushika hatima ya nchi basi Lowassa siyo tu atashindwa, bali atashindwa na hatoamini; na nina uhakika atajiondoa Chadema mapema asubuhi kwani ndoto yake haitotimia.

Endapo wazee wataamua kukaa pembeni na kuacha vijana wajifunze somo kwa matatizo basi siyo tu watakuwa wanashindwa kutimiza wajibu wao wa kuilinda jamii yao na kuhakikisha wanakirithisha kizazi kijacho nchi ambayo inaweza kuendelezwa.

Wazee na watu wengine wenye hekima hawatoacha Tanzania igeuzwe panya wa maabara ambapo viongozi walioshindwa waje kufanyia majaribio. Mbele ya wazee halitoharibika neno. Hili sina hofu nalo.

CHANZO: RaiaMwema
Mwandishi wa Makala ni Lula wa Ndali Mwananzela.

Pole Lula wa Ndali kwa porojo zako, hivi 54 years bado mna tushawishi kuwa sisiem ni chaguo la watanzania kweli.
Asante sana kwa matusi kuwa sisi ni wavuta banki, ila kikatio hakivuti
 
Nape kamata hiyo ikusaidie kwann watu wanataka hata ng'ombe awaongoze badala ya ccm itakusaidia.
 
Attachments

  • IMG_20150910_223605.jpg
    IMG_20150910_223605.jpg
    13.6 KB · Views: 100
Ccm tumeisoma namba lakini tunawapigia simu mmezima..tumetuma meseji mkiwasha simu mtaikuta meseji tar 25
 
Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia karibia 70+ ya watu waliojiandikisha kupiga kura ni vijana kuanzia miaka 18 - 45 ... Sasa hao wazee uliowataja kuiokoa ccm ni asilimia 20 tu. Niwashauri tu, kuliko kuwatusi hawa vijana ni bora mrudi muwashawishi kwa hoja labda watawaelewa ... Muda bado upo.

Hii makala ni kielelezo tosha kuwa Yericko Nyerere haongopi alipoibua mkakati wa ccm kumuibua mkuu wa majeshi ili 'kuokoa jahazi'

Wazee ni kina nani wenye uwezo wa kuzuia mtu aliyeshinda ktk ballot box asiwe kiongozi ktk nchi ya kidemokrasia kama sio kuanzisha vurugu ili jeshi lipate sababu ya 'kuchukua nchi'
Just narrating my dream
 
Last edited by a moderator:
Mnapoteza muda tu na magazeti yenu uchwara,narudia tena hata mimi nina elimu ya masters lakini nasema kwa mwaka huu mnatapatapa tu.Tena mshukuru ujinga wa watanzania kwa kuwanyima elimu ndiyo bado mnaendelea kuwatawala kwa kutojitambua.Msomi yeyote mwenye akili timamu atakayeipigia kura CCM ni ama ananufaika na system au akili zake ni pungufu.Kati ya miaka yote hakuna kipindi CCM ilivyohubiri kushindwa kama kipindi hiki.Alianza kinana na mawaziri mizigo hakuna aliyeweza kutuondolea ile mizigo kwakuwa hakuna mwenye unafuu,Lowasa kabla hajahama chama chenu tulimwita fisadi hakuna mwanaccm aliyethubutu kutuunga mkono watanzania na mkaanza kuhubiri kuwa tume ya mwakyembe haikumkuta na jinai so akawajibika kisiasa.Leo amehamia upinzani mnahubiri ni fisadi.Nilichokigundua ni nini?ukitaka kuendelea kupiga madili na ubebwebebwe na madudu yako jifiche kwenye chaka la ccm.Leo wakina chenge,tibaijuka,ngereja,wakina ridhiwan hawatajwi na CCM hata chembe lakini je usafi wao hauna shaka kwa watanzania? KOMBE NI LA MONDULI.
 
Tanzania imekuwa mfano wa panya wa maabara kwa miaka mingi sana..... Sasa wakati umefika wa kuiondoa nchi kutoka kwenye mikono ya "wafanya majaribio"... Nchi inatakiwa irudi mikononi mwa wananchi chini ya uongozi uliosimikwa na idadi kubwa ya wananchi..!! Bahati nzuri ni kuwa takwimu hazidanganyi...Idadi kubwa ya wananchi kwa sasa ni vijana...!!!

Hakuna njia nzuri sana ya kujifunza kitu zaidi ya kuthubutu.... Hao wazee walithubutu kwa wakati wao wakiwa vijana wakamuondoa mkoloni mweupe... Waliweza hawakuweza...??? Je waliwasubiri wazee ndo wawaamulie nini cha kufanya...?? Walichukua nchi wakampa Mwl. J.K Nyerere bila kujali mengine yote..!!

Kadhalika leo hii... vijana wanaona kuna haja ya kuwaondoa wakoloni weusi .... Kwamba uwezo wanao... nia wanayo...na nguvu wanazo... Wazee walifanya hivi sasa kwa nini wawakatalie vijana wao...!! Vijana wameamua Lowassa awe rais wao iwe mvua iwe jua..!

ccm wajaribu karata nyingine ..... hii ya wazee haitowasaidia...!!
 
Kwahiyo utulivu ukipotea unadhani "Who is going to lose?" Vijana mihemko itawafikisha pabaya.Narudia Lowassa atakuwa nyumbani kwake uingereza na familia yake.Mbowe atakuwa nyumbani kwake Dubai na familia yake.Wengine watakuwa wanahudhuria kesi The Hague ingawa watashinda.Wewe na wenye akili finyu wenzenu mtakuwa kaburini muda huo.

kwa taarifa hao mihemko hawana cha kupoteza, hawana reference yeyote! wewe unae ijua the Hague wenzio hata hawaijui!
That in our approach to a problem we should start from objective facts, not from abstract definitions, and that we should delivered our guiding principles, policies and measures from an analysis of this facts!
 
Aisee......
 
KUNA msemo kuwa; “Penye wazee haliharibiki neno”. Msemo huu unatumiwa sana kama tahadhari kwenye masuala ambayo yanaweza kuhusisha vijana au watu wengi ambao labda hawana umri wa kuweza kuwa na hekima ya mambo fulani fulani. Msemo huu unatumiwa zaidi katika kutafuta namna ya kusuluhisha jambo ambalo linaonekana bila ushauri na hekima ya wazee basi linaelekea kubaya.

Ninaamini msemo huu utakuwa kweli katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu hasa baada ya makundi ya vijana kuonekana bila kutaka kutafakari, kufikiri au hata kujiuliza maswali wameamua tu “liwalo na liwe” na sasa wako tayari kulipeleka taifa mikononi mwa kundi la viongozi ambao uongozi wao tayari umeshaonesha madhara makubwa.

Utakuwa kweli kwa sababu baada ya Lowassa kuingizwa Chadema na kupewa ugombea wa urais na hatimaye kusababisha mvurugano mwingine kwenye chama hicho kama aliousababisha na kuuacha ndani ya CCM. Makundi ya vijana hasa wanaonekana kumfurahia wakiamini kuwa nafasi ya kuiondoa CCM madarakani imefika.

Ni kweli kuwa taifa letu linahitaji mabadiliko makubwa ya kiutawala na wasomaji wangu wanaweza kukumbuka vizuri tu kuwa nimeliandika hili mara nyingi katika miaka hii ya mwamko wa kisiasa nchini. Mabadiliko haya hata hivyo yanaonekana sasa hivi yanalazimishwa kubebwa na mtu ambaye hajawahi kuyasimamia, kuyazungumzia au hata kuonesha kuwa anayajua. Lakini vijana wetu wanaonekana hawajali haya yote kwani wao sasa “wameamua” kuiondoa CCM madarakani “liwalo na liwe”.

Na kinachotisha zaidi ni kuwa vijana – wengine ni watu wenye akili tu (za darasani au vinginevyo) – hawana sababu ya msingi ya kwa nini wanamtaka Lowassa kuwa Rais wao zaidi ya matamanio yao ya kuona CCM inaondolewa madarakani. Imefika mahali hata ukiwauliza kwa nini wanamtaka Lowassa hawaoni hata aibu au kusita kwani wanasema tu “hakuna sababu sisi tunataka CCM iondoke!”.

Na wapo wasomi kabisa na watu ambao vinginevyo unaweza kuamini ni makini na wao pia wamedandia treni hili la Lowassa na wao pia hawana sababu wakisema tu “watu wamechoka” na hivyo basi kutokana na kuchoka basi wako tayari kufanya uamuzi yenye hatari.

Kuna sababu ya kwa nini kwa mfano, madereva wa malori wanatakiwa wapewe muda wa kupumzika hasa kama wana safari zile za masafa marefu. Hii ni kwa sababu dereva hata awe bora kiasi gani kama hajapumzika vya kutosha basi yuko hatarini kusababisha ajali na ajali nyingi za malori makubwa au mabasi zinatokana na madereva kutokulala vizuri au kupumzika na hivyo wanapokuwa barabarani wanakuwa wachovu.

Mtu aliyechoka hapaswi kufanya uamuzi mgumu wenye matokeo katika maisha yake kwani anaweza kujidhuru mwenyewe au kudhuru watu wengine. Watanzania waliochoka na utawala wa CCM hawapaswi kufanya uamuzi wa kumkumbatia Lowassa kwa sababu “wamechoka” kwani hilo peke yake linapaswa kuwa sababu ya kufikiria mara mbili kama wanastahili hata kufanya uamuzi huo.

Watanzania hawa waliopigika katika miaka hii hamsini leo hii wanaonekana kama wamepata nafasi ya pekee ya kuiondoa CCM kiulaini na hivyo hawataki kuipoteza. Ukiwasikiliza mashabiki hawa wa Lowassa utaona kuwa wengi wao wamefikia mahali pa kusema kuwa “hata kama ni fisadi, au kiongozi mbaya sisi tutamchagua tu’’. Wengine wamefikia hata kusema kuwa “bora jiwe kuliko CCM” na wanazungumza hivi wakiamini wanazungumza kwa akili kabisa.

Na hapa ndipo ninapoona kuwa – na wananchi wasije kushangaa Oktoba 25 Lowassa akianguka vibaya – Wazee wa Tanzania watakapoingilia kati na kuliokoa taifa kutokana uamuzi wa watu wenye maumivu, waliochoka na ambao kutokana na mapenzi fulani hivi kwa mtu wao hawawezi kufikiri vizuri.

Wazee wataweza kabisa na ninaamini wanasababu ya kuwaangalia hawa vijana wasije kuliingiza taifa kwenye matatizo kama vijana wa mataifa mengine walivyofanya wakiamini wanaleta mabadiliko. “Mabadiliko” yanatokana na msukumo wa hisia (emotional pressure) ni mabadiliko ya hatari kwani hisia hizo zinapoisha (na hisia huisha) mtu anaweza kukaa na kuanza kujuta; lakini kujuta kwa uchaguzi kama huu kutadumu miaka mitano au kumi!

Sidhani kama taifa letu na wazee wetu wanaweza kucheza kamari hiyo na kuona nchi itakuwaje miaka kumi baadaye. Wazee na watoto ndio wanadhurika zaidi yanapotokea mabadiliko makubwa au migongano ambayo haitoisha na hivyo ni kwa maslahi yao wao wenyewe (wazee) na watoto au wajukuu wao kuweza kuleta “neno” zuri la kuzuia mabadiliko yanayosukumwa na hisia ambayo inaonekana makundi ya vijana yanashabikia. Hili ni muhimu kueleweka kwani sasa hivi simulizi (narrative) ambayo ipo mitaani ni imani (msingi wake picha za nyomi) kuwa Lowassa atashinda na endapo hatoshinda basi CCM itakuwa imeibakura.

Hii ina maana kuwa – na hapa mtu anisome mara mbili – kuna uwezekano mkubwa sana wa machafuko endapo Lowassa hatoshinda kwani tayari makundi ya vijana yanaamini tayari ni mshindi. Ambacho vijana wengi hawajui ni kuwa ni wazee wa Tanzania ambao mara zote wamekuwa wakiamua matokeo ya uchaguzi – siyo vijana; ni wazee.

Ni wazee kwa sababu hawa hutawaona kwa wingi katika hamasa za mikutano ya kisiasa au maandamano lakini siku ya uchaguzi kwa sababu hakuna purukushani nyingi watajikongoja wenyewe na wengi wanapiga kura mapema na kuamua hatima ya uchaguzi.

Nina uhakika wa asilimia mia moja kuwa endapo siku ya uchaguzi wazee wengi wataamua kulinda nchi yao na kutoacha viongozi kama Lowassa na wale waliomuingiza kushika hatima ya nchi basi Lowassa siyo tu atashindwa, bali atashindwa na hatoamini; na nina uhakika atajiondoa Chadema mapema asubuhi kwani ndoto yake haitotimia.

Endapo wazee wataamua kukaa pembeni na kuacha vijana wajifunze somo kwa matatizo basi siyo tu watakuwa wanashindwa kutimiza wajibu wao wa kuilinda jamii yao na kuhakikisha wanakirithisha kizazi kijacho nchi ambayo inaweza kuendelezwa.

Wazee na watu wengine wenye hekima hawatoacha Tanzania igeuzwe panya wa maabara ambapo viongozi walioshindwa waje kufanyia majaribio. Mbele ya wazee halitoharibika neno. Hili sina hofu nalo.

CHANZO: RaiaMwema
Mwandishi wa Makala ni Lula wa Ndali Mwananzela.

We kanjanja kabisa, unajichanganya mwenyewe unasema takwimu zinaonyesha vijana ni wengi kuliko wazee hapo hapo unadai wazee watafanikisha ushindi kwa CCM kwa kura wakati vijana ndo wana kura nyingi.!!
 
Kamanda Moshi binafsi nikiona majina ya hii hata kabla hujaweka maoni yako nayajua.Maana ajenda yenu inajulikana tangu Uhuru.Tatizo lenu jingine mna vichwa ambavyo ni "One direction-programmed".Unazungumzia Upendeleo,rushwa ndani ya CCM.Mbona ninyi chama Hakina demokrasia hata fake,ufisadi wa ruzuku na misaada ndo usiseme.Chama mmebebana ndugu wachagga tupu then eti na nyie mnaona madhaifu ya wengine.Mnajitoa sana akili ndo maana nasema hakuna kijana makini anayewaunga mkono labda anayetoka Arusha na Moshi.

Uongo uliokubuhu mi ni wa MTWARA na piga ua CHADEMA na UKAWA ndio kila kitu kwangu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom