Wazee wa Dar es Salaam ni akina nani?

Wazee wa Dar es Salaam ni akina nani?

Kutokana na vifo vya mfululizo vya vijana...bodi ya vifo na uhai imeamua kupunguza umri wa uzee...sasa hivi uzee unaanzia miaka 30....
 
jana nilikuwa nasikia tangazo toka ofisi ya mkuu wa mkoa kuwa wazee walnaotakiwa kufika kwenye mkutano na Rais ni wale tu waliopata mualiko rasmi, wazee wengine mtamsikiliza Rais kupitia ktk vyombo vyenu vya mawasiliano, La ajabu leo nikiwa namimi nimekaa nyumbani nikimsikiliza Rais nimeona si wazee bali hata watoto wapo............!!!
 
Hili swali hata mimi najiuliza sipati jibu. Hawa wazee wa DSM ni akina nani? Nyerere alipokuwa anakutana na wazee wa DSM, alikuwa anakutana na wazee ambao alikuwa na historia nao. Waliomsupport waka ti wa harakati za kuwang'oa wakoloni. Sasa hawa wazee wa sasa hivi ni akina nani?? Sisi wengine hatuhusuki katika masuala muhimu ya nchi yetu? Au sisi wapangaji? Sijui hao wazee ni akina nani!!!!!
Sijajua masuala mazito yahusuyo hatima ya nchi yetu kupitia mchakato wa Katiba mpya kuzungumzwa kwa "wazee wa CCM wa Dar es Salaam!" Najua baadhi yenu mtasema kuwa Rais alikuwa anaongea kwa Taifa zima lakini implication iliyoonekana imekaa kichama zaidi kuliko kitaifa!

Hivi nchi hii imebaki ya hawa wazee wa DSM tena wa CCM au namna gani? Si ingekuwa ni vema Rais angeandaa kipindi ambacho watu wengi wangeshiriki tena kwa kuuliza maswali, kuliko kuhutubia hao wazee ambao wengi wao walikuwa wamelala usingizi na kushtuka baadhi yao wakiwa wanapiga makofi!
 
Kwani ni kigezo gani kinachotumikaga kupata wazee wa dar?na wanafanya kazi gani?au wapogo tu kusubiria kuitwa na rais.
 
Mara Nyingi Professor JK amekuwa akinilazimisha kufikiri sana pale anapoamua kutumia hadhira inayoitwa WAZEE WA DAR ES SALAAM.

Tija gani huyu Professor huipata kwa kutumia hadhira ya namna hii?
Mbona Wazee wangu mtaani hawakualikwa kuna Vigezo gani ambavyo wamekosa,

Je anachokifanya kwa Wazee hawa wa dar ni kuwaheshimu au

Hivi Kwanza hawa Wazee wa dar Ndio wale wale aliokuwa akiwatumia mwalimu enzi zile?
tafadhalini wadau hebu nisaidieni kuelewa zaidi....

:confused2:
 
Kwani ni kigezo gani kinachotumikaga kupata wazee wa dar?na wanafanya kazi gani?au wapogo tu kusubiria kuitwa na rais.

Ni heshima tu wanapewa kwani wao ndio watu wa kwanza kumvalisha nyerere suruali. before nyerere alikua anavaa bukta tuu sasa asingeweza kwenda UNO na Bukta! wazee hawa wakamzoesha kuvaa suruali na suti hata alipokwenda UNO akaonekana mtu miongoni mwa watu. wazee hawa wanaihitaji kupewa heshima hii kwa kweli...
 
Leo nimewaona wazee wa Darisalama ,kumbe ni vijana ni tofauti na wazee wenzangu wa vijijini kule Lyamba lya mfipa,aisee kumbe wazee wenzetu wa mujuni hawazeeki leo nimewaona wakimsikiliza Mh raisi nimeona wazee wengine kama wana umri wa miaka 25,ila pia hawa wazee wa Darisalama pamoja na mkuu wa mkoa wote ni wana CCM sasa si wangeitwa tu wazee wa CCM wa mkoa wa Darisalama.
 
Back
Top Bottom