Naomba kuuliza;
- Hivi hawa wanaoitwa wazee wa Daressalaam ni akina nani?
- Wana umri gani, maana huwa naona mchanganyiko wa watoto, vijana na watu wa makamo katika kinachoitwa wazee wa Dar-Es-Salaam.
- Lakini pia je, Wazee hawa ni wa Chama gani, Maana kama wana chama, basi wangeitwa wazee wa CCM au CUF au CDM mkoa wa Dar-es-Salaam.
- Na pia Je, Matumizi ya "FORUM" hii inayoitwa "WAZEE WA DARESALAAM" yanaendana na kuasisiwa kwake au yalivyokuwa yakitumika kipindi cha Hayati baba wa Taifa?