Wazee muhimu wasife na kuicha CCM peke yake

Wazee muhimu ninamaanisha wazee wenye akili nyingi, wenye hekima na wanaoifahamu vema Tanzania. Wazee hawa ni wale wote wenye hadhi ya Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee Kikwete, Mzee Warioba, Butiku, Cleopa Msuya, Malecela, Msekwa, Karume, na wengine wa aina hii.

Kule Marekani na Ulaya wazee wazee wao wa aina hii kama vile George Washington na wengine kabla ya kufa walihakikisha kuwa wanaacha checks and balance za kisiasa kwenye mataifa yao kwa kuacha vyama zaidi ya kimoja vyenye nguvu sawa na katiba imara ili viwasaidie wananchi wao baada ya wao watakapokuwa hawapo tena duniani. Waliacha dira za mataifa yao na vyama na taasisi imara zitakazoshindana kwenye kuitekeleza dira yao wakati wao hawapo duniani tena.

Mwalimu Nyerere ilikuwa anaifahamu siri hii ya mataifa ya ulaya na Marekani, lakini alishindwa kuitekeleza yote kwa 100% kutokana na waliokuwa wanamzunguuka kushindwa kumuelewa kabisa, alijaribu lakini hakufua dafu. Mwl. Nyerere alifahamu kuwa baada ya yeye kufariki dunia ile checks and balance aliyokuwa ikiifanya yeye haitakuwepo kabisa kutokana na hurka na ufahamu wa watu waliokuwa wakimzunguuka. Hii ndiyo sababu iliyomsukuma Baba wa Taifa kukubali na kulazimisha Tanzania ikubali mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992 ingawa wenzake walimpinga. Yeye alitaka kuwepo na vyama 2 vya siasa vyenye nguvu sawa ili vikosoane kwenye masuala ya nchi. Yaani vishindane hoja na sera katika kuitawala nchi, chama kimoja kikizembea na kuboronga chama cha pili kinarekebisha kama inavyotokea Marekani, Uingereza na nchi nyingine za ulaya.

Nyerere aliwafahamu sana watu wake na CCM yake, alifajua tu kuwa akiondoka yeye CCM itatunga sheria na kanuni za Kikaburu za kuumiza watu bila kujali, watakuwa madalili wa mali za wananchi, watajilimbikizia mali na madaraka bila kuhojiwa na wataendelea kubaki madarakani kwa nguvu za dola. Na kweli sasa hivi CCM haitegemei kupiga kampeni tu ili kushinda chaguzi, zipo sheria na taratibu kwaajili ya kuibakisha CCM madarakani sio kwa manufaa ya watanzania na wana CCM bali kwaajili ya viongozi na familia zao. Leo hii nafasi zote nzuri za ajira na uongozi zimejaa watoto wa viongozi na jamaa zao zao.

Hata wanaCCM walio wengi wanatoka kapa, wanaambulia t-shirts na kofia na posho wakti wa kampeni baaaasi.

Wazee wetu hawa muhimu kama wataondoka duniani na kuviacha vyama vya upinzani vyootenchini vimekufa au havina nguvu kabisa wajue kuwa wameliacha taifa lisokuwa na matumaini, watakuwa wameiacha Tanzania kwenye njia mbaya kabisa kuwahi kutokea. Wameliacha taifa bila ya mtu wala taasisi yoyote inayoweza kuhoji chochote kizuri au kibaya kama wanavyohoji akina Mzee Butiku na Warioba wakati mwingine. Kila atakayehoji kitu kibaya atatungiwa sheria ya kumthibiti kama walivyokuwa wakifanya makaburu. Taifa litaanza upya kutafuta uhuru na demokrasia kwa njia ngumu sana.

Nitoe wito kwa hawa wazee waone mbele kama wezao akina washington na Nyerere kuhusu mataifa yao. Wasiangalie matumbo yao ya kizee eti kwasababu watoto wao pia wamejumuishwa kwenye ulaji. Ulaji wa aina hii haudumu na sisalama kwa taifa, sio kwamba watu wote (raia na askari) wataendelea kuangalia hali hii iendelee milele.
Uwepo wao unamsaada Gani kwa Nchi sindio hao wanataka Katiba ibadilike ili watoto wao waendelee kugawana mamlaka hao wazee wako ni Hasara kwa Nchi

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Wazee hawa wanafahamu sana kuwa baada ya wao kuondoka duniani hakutakuwa na atakaehishimiwa, aminiwa, kuthaminiwa wala kusikilizwa sio tu na wanchi bali hata ndani ya wanaCCM wenyewe. Ikifikia hapo taharuki ya kutunga sheria kandamizi na matumizi mabaya ya vyombo vya dola vitaongezeka nchini. Hii itawaunganisha watanzania wengi dhidi ya kitabaka hiki nufaika cha kinasaba.

Ni heri wazee hawa sasa, leoleo wasaidie kuimarisha demokrasia nchini ili watu wasiopenda sera za chama kinachotawala watumie vyama vilivyoratibiwa kupinga badala ya kutumia vikundi na njia ambazo sio rasmi. Hivi ndivyo wanavyofanya Democrats na Republican, Labour Party na Conservative, etc. Na Mwl. Nyerere alikusudia hivyo yatokee Tanzania baada ya yeye mkosoaji mkuu atakapokuwa hayupo duniani lakini Wenzake hawakumuelewa kabisa. Nyerere alikerwa na utitiri wa vyama bali alitaka vyama vikubwa 2 tu vikosoane vinapofanya uzembe kwa wananchi. CCM haikubali kukosolewa na haina mkosoaji kwasasa, wazee wote muhimu wana conflict of interests na serikali maana watoto wao wamepewa ulaji na watawala ili kuwanyamazisha. Vyama vya upinzani navyo vimekabwa kooni ile mbaya kwa sheria za kikaburu na matumizi mambaya ya vyombo vya dola dhidi yao.

Mwl. Nyerere aliwahi kusema kaburu ni kaburu tu bila kujali ngozi yake. Kuhahakikisha kuwa vyama vya siasa na viongozi wake hawafurukuti hakuna tofauti na yale yaliyotokea kwa ANC dhidi ya National Party cha makaburu, tofauti ni kwamba wale walikuwa weupe na hawa ni weusi.
Umeeleza vizuri, hawa wazee ni matapeli tu bora wafe wote tuanze upya
 
Wazee muhimu ninamaanisha wazee wenye akili nyingi, wenye hekima na wanaoifahamu vema Tanzania. Wazee hawa ni wale wote wenye hadhi ya Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee Kikwete, Mzee Warioba, Butiku, Cleopa Msuya, Malecela, Msekwa, Karume, na wengine wa aina hii.

Kule Marekani na Ulaya wazee wazee wao wa aina hii kama vile George Washington na wengine kabla ya kufa walihakikisha kuwa wanaacha checks and balance za kisiasa kwenye mataifa yao kwa kuacha vyama zaidi ya kimoja vyenye nguvu sawa na katiba imara ili viwasaidie wananchi wao baada ya wao watakapokuwa hawapo tena duniani. Waliacha dira za mataifa yao na vyama na taasisi imara zitakazoshindana kwenye kuitekeleza dira yao wakati wao hawapo duniani tena.

Mwalimu Nyerere ilikuwa anaifahamu siri hii ya mataifa ya ulaya na Marekani, lakini alishindwa kuitekeleza yote kwa 100% kutokana na waliokuwa wanamzunguuka kushindwa kumuelewa kabisa, alijaribu lakini hakufua dafu. Mwl. Nyerere alifahamu kuwa baada ya yeye kufariki dunia ile checks and balance aliyokuwa ikiifanya yeye haitakuwepo kabisa kutokana na hurka na ufahamu wa watu waliokuwa wakimzunguuka. Hii ndiyo sababu iliyomsukuma Baba wa Taifa kukubali na kulazimisha Tanzania ikubali mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992 ingawa wenzake walimpinga. Yeye alitaka kuwepo na vyama 2 vya siasa vyenye nguvu sawa ili vikosoane kwenye masuala ya nchi. Yaani vishindane hoja na sera katika kuitawala nchi, chama kimoja kikizembea na kuboronga chama cha pili kinarekebisha kama inavyotokea Marekani, Uingereza na nchi nyingine za ulaya.

Nyerere aliwafahamu sana watu wake na CCM yake, alifajua tu kuwa akiondoka yeye CCM itatunga sheria na kanuni za Kikaburu za kuumiza watu bila kujali, watakuwa madalili wa mali za wananchi, watajilimbikizia mali na madaraka bila kuhojiwa na wataendelea kubaki madarakani kwa nguvu za dola. Na kweli sasa hivi CCM haitegemei kupiga kampeni tu ili kushinda chaguzi, zipo sheria na taratibu kwaajili ya kuibakisha CCM madarakani sio kwa manufaa ya watanzania na wana CCM bali kwaajili ya viongozi na familia zao. Leo hii nafasi zote nzuri za ajira na uongozi zimejaa watoto wa viongozi na jamaa zao zao.

Hata wanaCCM walio wengi wanatoka kapa, wanaambulia t-shirts na kofia na posho wakti wa kampeni baaaasi.

Wazee wetu hawa muhimu kama wataondoka duniani na kuviacha vyama vya upinzani vyootenchini vimekufa au havina nguvu kabisa wajue kuwa wameliacha taifa lisokuwa na matumaini, watakuwa wameiacha Tanzania kwenye njia mbaya kabisa kuwahi kutokea. Wameliacha taifa bila ya mtu wala taasisi yoyote inayoweza kuhoji chochote kizuri au kibaya kama wanavyohoji akina Mzee Butiku na Warioba wakati mwingine. Kila atakayehoji kitu kibaya atatungiwa sheria ya kumthibiti kama walivyokuwa wakifanya makaburu. Taifa litaanza upya kutafuta uhuru na demokrasia kwa njia ngumu sana.

Nitoe wito kwa hawa wazee waone mbele kama wezao akina washington na Nyerere kuhusu mataifa yao. Wasiangalie matumbo yao ya kizee eti kwasababu watoto wao pia wamejumuishwa kwenye ulaji. Ulaji wa aina hii haudumu na sisalama kwa taifa, sio kwamba watu wote (raia na askari) wataendelea kuangalia hali hii iendelee milele.
Jibu ni kupanua wigo wa siasa katika nchi. Akili nzuri sana zipo hata nje ya CCM, ukizifunga pingu nchi itadidimia. Na hili ndilo hao unaowaita wazee wa CCM wamekuwa wakijaribu kulifanya katika uhai wao wote. Sishabikii kufa kwao, lakini Mwenyeezi Mungu ndio mjuzi katika kuiletea nuru Tanzania au na Wazee hao au bila wazee hao.

Kimsingi tunatakiwa tufikirie nje ya box, kwani pale walipotufikisha hatutatoboa kama hatutalitoboa box.
 
Hakuna watu wa ajabu kama hao wazee walio wahi kushika madaraka nchi hii,wanajiona mungu mtu, kwamba wao na family zao ndio wanauwezo wakuongoza nchi,ndo sababu wakifa watu wanashangiria na kubeza
 
Wazee hawa hawana haya hata kidogo. Kwanza wanashangaa kuona eti vyama vilivyoleta uhuru kule Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia, nk vyote havipo madarakani leo hii, Wanaviona wajinga kushindwa na wapinzani. Miundombinu ileile tuliyoitumia kupambana na makaburu na wareno kuzisaidia nchi za kusini mwa Afrika kudai uhuru wao sasa hivi ndio inatumika kuvikandamiza vyama vya upinzani visinyanyue shingo.

Hata hivyo, Nadhani hata sisi wananchi ni majuha sana, unyumbu wetu wanautumia kikamilifu.
 
Hakuna watu wa ajabu kama hao wazee walio wahi kushika madaraka nchi hii,wanajiona mungu mtu, kwamba wao na family zao ndio wanauwezo wakuongoza nchi,ndo sababu wakifa watu wanashangiria na kubeza
Iko siku kama sio wao wenyewe basi watoto au wajukuu zao hawataamini kile watakachokiona, itawatokea kama ndoto usingizini. Watakujakuambiwa kila kitu wanachokijua leo kuwa ni chakwao na kumiliki kumbe sio chao ni cha serikali. Wananchi watagawana hata suti na bakuli zao. Historia na ukweli havina tabia ya kupotea. Kuna mtu anateuliwa kuwa DC na mbunge mpaka askari wanajisikia kichefuchefu kumpigia salute. Iko siku udhalilishaji huu pia utawachosha,
 
Ubinadamu wetu unatutaka kufa. Ipo siku watakufa. Matumaini ya Taifa letu hayako mikononi mwa wanadamu tuache kuchuliana. Na wala sio lazima kila mzee anabeba vision ya umoja na ustawi wa Taifa hili. Wengine wako kimaslahi zaidi
 
La Kikwete naye yumo?
Nimeishiwa hata nguvu za kusoma mpaka mwisho.
Mzee kikwete ni miongoni mwa wazee wanaokwenda sana mataifa ya wengine kama Ulaya na Marekani ambako vyama vya upinzani ndio kimbilio la wananchi na taifa. Mfano, bila kuweko kwa democrat imara wamarekani ingewawia vigumu kuondokana na Trump. Wanafahamu uzuri wa kuwa na vyama vingi vikubwa lakini wamekaa kimya wakati vyama vya upinzani vinanyamazishwa kwa hila.
 
Huyuhuyu aliyeuza dhahabu yetu tukipewa vyandarua? Aliuza gesi yetu.
Kina Bush, Obama, Clinton,walikuwa wanapishana Dar utafikiri ni Texas.
 
Haha, alitaka kuwauzia Kigamboni yooooote. Eti mji wa kisasa.
 
Watu wazima wote hata watoto wanaojielewa wapiganie nchi yao iwe salama kwa wote kuishi.
Hizi fikra tegemezi ni hatari kwa mustakabali wa taifa.
 
Sio fikra tegemezi ila ni namna bora ya ku manage planed change. Vijana wao waliowaachia wamepoteza uwezo wa kushawishi badala yake wanatumia nguvu kufanikisha kila kitu
 
Hao wazee tuwaache wapumzike na washauri wakiweza.
Watu wenye nguvu ya kimwili na kiakili wawajibike kulinda taifa.
We must have a competent succession plan.
 
Mwalimu alifanya kosa kubwa kutubadilishia kipande tu cha Katiba ili kuruhusu siasa ya vyama vingi... Kwa kweli mabadiliko haya yameghalimu maisha ya watanzania wengi mno hadi muda huu - mfumo huu umefanya watu kufa, kufilisiwa, kufungwa, kunyanyashwa nk

Mwalimu angetupatia katiba mpya kabla ya kughatuka, kwa kweli katuachia mzigo mkubwa mno kiasi cha kuligawa Taifa letu makundi mawili - wanaotaka mfumo wa mwaka 1977 ambao chama tawala ndicho kinachoshika hatamu ya uongozi mia kwa mia na wale wanaotaka mfumo wa kidemokrasia, taasisi za kutoa haki kuwa huru bila kuingiliwa na watawala.

Bado tupo katika giza nene, Mwalimu umetuachia mzigo mzito mno.
 
Ukikumbuka yaliyotokea Zanzibar katika uchaguzi wa Mwaka 1995, namna ambavyo CUF wali-perform, nashindwa kukubaliana na wewe juu ya Nyerere na dhamira ya dhati ya mfumo wa vyama vingi.

Kaunda aliyekubali kushindwa, waiona nchi yake ikibadilisha vyama bila bughudha!
 
Back
Top Bottom