kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,313
- 12,613
- Thread starter
- #41
Hao wazee tuwaache wapumzike na washauri wakiweza.
Watu wenye nguvu ya kimwili na kiakili wawajibike kulinda taifa.
We must have a competent succession plan. ni msur
Wazee hawa ni msululu wa wa watanzania wenzetu ambao walihakikisha kuwa CCM haitoki madarakani litoke jua inyeshe mvua. Wanafanya hivyo huku wakifahamu kuwa sera za CCM kwa miaka zaidi ya 60 ya uhuru zimeshindwa:Hao wazee tuwaache wapumzike na washauri wakiweza.
Watu wenye nguvu ya kimwili na kiakili wawajibike kulinda taifa.
We must have a competent succession plan.
1. kuwapatia maji wananchi, hadi leo watu na wanyama wanakunywa pamoja.
2. Kuwapatia matibabu watanzania wote
3. Kuinua Kilimo
4. Zimeua Elimu yetu, watu wanahangaika kupeleka watoto wao Kenya na Uganda
5. Zimeshindwa kupanga miji
6. Zimeshindwa kusafisha miji
7. zimeshindwa kulipa mishahara kwa watumishi. Kima cha chini hakizidi dola 120 kwa mwezi miaka 60 ya uhuru.
8. Hakuna hata soko la mahindi
Mwl. Nyerere hata yeye alilijutia kosa hili. Alidhani baada ya kung'utuka angemuamrisha chakufunga na lakufanya yule aliyemuachia kijiti, lakini looo, haikuwa hivyo, ikamlazimu ashinde nyuma ya vipaza sauti akimkosoa mteule wake hadi akamuandikia kitabu cha kukosoa siasa na uongozi wake. Kabla hajageuka wenzake wakalifuta Azimio lake la Arusha na kuja na la Zanzibar. Wenzake wakawa matajiri wa kupindukia ghafla wakayauza mashirika yote na kuyabinafsisha mengine huku akiangalia kwa macho yake bila kuwa na la kufanya kwa mujibu wa katiba yake yeye mwenyewe. Twiga wakawa wanapanda ndege wazimawazima.Mwalimu alifanya kosa kubwa kutubadilishia kipande tu cha Katiba ili kuruhusu siasa ya vyama vingi... Kwa kweli mabadiliko haya yameghalimu maisha ya watanzania wengi mno hadi muda huu - mfumo huu umefanya watu kufa, kufilisiwa, kufungwa, kunyanyashwa nk
Mwalimu angetupatia katiba mpya kabla ya kughatuka, kwa kweli katuachia mzigo mkubwa mno kiasi cha kuligawa Taifa letu makundi mawili - wanaotaka mfumo wa mwaka 1977 ambao chama tawala ndicho kinachoshika hatamu ya uongozi mia kwa mia na wale wanaotaka mfumo wa kidemokrasia, taasisi za kutoa haki kuwa huru bila kuingiliwa na watawala.
Bado tupo katika giza nene, Mwalimu umetuachia mzigo mzito mno.
Wanakula bila kunawa na kila anaewakosoa Wana wivu wa kike.