Angalizo muhimu sana kwa CCM, mwenye sikio atege

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Nachelea kuita ONYO kwa CCM.

Angalizo hili linaweza likawa la mwisho yaani msipoangalia kuna dalili mbaya sana ambayo itawagharimu na kutikisa Afrika.

Kuendelea kukumbatia Katiba inayopigiwa kelele na wananchi kuwa haifai kwa mfumo wa siasa za vyama vingi, ni sawa na kulalia kitanda cha misumari huku godoro liliwa ni kipande cha gunia.

Nimeona, yes nimesikia masikioni kwangu. Inawezekana sauti hii ilikuwa kutoka upande wa pili wa ukuta ambapo sijaweza asilani kufahamu nani alikuwa mzungumzaji. Lakini sauti inasema kuwa KIPIMO KILE MLICHOWAPIMIA WENGINE NDICHO MTAKACHOPIMIWA NA KUJAZWA KWA KUFURIKA.

Katiba hii tuliyonayo sasa ambayo mnaamini ndiyo ulinzi wa Taifa letu ni Katiba inayotoa maelekezo na maagizo muhimu (japo kwa uchache) ya maongozi ya nchi hususani kwenye Haki na Wajibu. Bahati mbaya sana mmeweka pamba masikioni na kujiweka kwenye daraja la kuwa wenye akili na ufahamu kuliko raia wote wa nchi hii. Maamuzi mengi mnayoyafanya (CCM) ni kwa maslahi mapana ya chama na walioshika madaraka.

Siku hazigandi, kwa sababu baada ya kiangazi huja mvua, mvua inaweza kugharikisha na kuporomosha milima kwa nguvu itokanayo na matone ya maji yaliyojikusana sehemu moja na kusaka njia ya kupita.

Haya fanyeni jambo la akili sasa. Mchakato wa kupata Katiba Mpya uanze mapema kabla ya uchaguzi ujao 2025 ili kuepusha yanayoepukika. Angalizo kwenu ni kwamba Katiba hii itakapokuja kutumia dhidi yenu hakika hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe kwenye ghorofa la barafu mlilolijenga tangu uhuru hadi sasa.

Sauti ya tindo za wajenzi imezidi sauti za waombolezao. Fahamuni kwamba waliao na kusugua maogti kwa nchi hii siyo wale mnaowapandisha kwenye majukwaa yenu ya kisiasa na kiserikali wakiwaombea kwa mbwembwe na ufahari wa kufaidi juisi ya watawala.

Ni mtu wa kawaida sana tena mdogo.
Sina jipya zaidi ya kufikisha ujumbe niliousikia kwa masikio yangu mawili bila kumuona mnenaji

CC Mshana Jr
 
Katiba mpya siyo kipaombele cha watanzania. Ndio maana hakuna bibi yeyote wa kijijini anayeweza kukwambia kuwa kero yako ni katiba mpya.
Je sisi tunaoidai Katiba mpya hadharani siyo Watanzania?

Mungu alimuambia Musa kuwa ataufanya mgumu moyo wa Farao ili apokee yale mapigo aliyopangiwa kupewa...

Yule kiumbe Umsolopagaaz alisema
Pigo la mwisho
pigo lililonyooka

Hoja yako haina tofauti na watesi wa Taifa hili
 
Nachelea kuita ONYO kwa CCM.

Angalizo hili linaweza likawa la mwisho yaani msipoangalia kuna dalili mbaya sana ambayo itawagharimu na kutikisa Afrika.

Kuendelea kukumbatia Katiba inayopigiwa kelele na wananchi kuwa haifai kwa mfumo wa siasa za vyama vingi, ni sawa na kulalia kitanda cha misumari huku godoro liliwa ni kipande cha gunia.

Nimeona, yes nimesikia masikioni kwangu. Inawezekana sauti hii ilikuwa kutoka upande wa pili wa ukuta ambapo sijaweza asilani kufahamu nani alikuwa mzungumzaji. Lakini sauti inasema kuwa KIPIMO KILE MLICHOWAPIMIA WENGINE NDICHO MTAKACHOPIMIWA NA KUJAZWA KWA KUFURIKA.

Katiba hii tuliyonayo sasa ambayo mnaamini ndiyo ulinzi wa Taifa letu ni Katiba inayotoa maelekezo na maagizo muhimu (japo kwa uchache) ya maongozi ya nchi hususani kwenye Haki na Wajibu. Bahati mbaya sana mmeweka pamba masikioni na kujiweka kwenye daraja la kuwa wenye akili na ufahamu kuliko raia wote wa nchi hii. Maamuzi mengi mnayoyafanya (CCM) ni kwa maslahi mapana ya chama na walioshika madaraka.

Siku hazigandi, kwa sababu baada ya kiangazi huja mvua, mvua inaweza kugharikisha na kuporomosha milima kwa nguvu itokanayo na matone ya maji yaliyojikusana sehemu moja na kusaka njia ya kupita.

Haya fanyeni jambo la akili sasa. Mchakato wa kupata Katiba Mpya uanze mapema kabla ya uchaguzi ujao 2025 ili kuepusha yanayoepukika. Angalizo kwenu ni kwamba Katiba hii itakapokuja kutumia dhidi yenu hakika hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe kwenye ghorofa la barafu mlilolijenga tangu uhuru hadi sasa.

Sauti ya tindo za wajenzi imezidi sauti za waombolezao. Fahamuni kwamba waliao na kusugua maogti kwa nchi hii siyo wale mnaowapandisha kwenye majukwaa yenu ya kisiasa na kiserikali wakiwaombea kwa mbwembwe na ufahari wa kufaidi juisi ya watawala.

Ni mtu wa kawaida sana tena mdogo.
Sina jipya zaidi ya kufikisha ujumbe niliousikia kwa masikio yangu mawili bila kumuona mnenaji

CC Mshana Jr
Ukweli mchungu..
Wakumbuke tu, hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho
 
Umenena vema mtu wa Mungu.
 
Katiba mpya siyo kipaombele cha watanzania. Ndio maana hakuna bibi yeyote wa kijijini anayeweza kukwambia kuwa kero yako ni katiba mpya.
Katiba mpya ni kilio na kipaumbele cha wanasiasa walafi na wenye uchu wa madaraka hasa chadema, wananchi kilio Chao na kipaumbele ni umeme wa uhakika, maji, na huduma nzuri za afya na elimu
 
Katiba mpya siyo kipaombele cha watanzania. Ndio maana hakuna bibi yeyote wa kijijini anayeweza kukwambia kuwa kero yako ni katiba mpya.
Dah!

Nimeandika mara nyingi sana na kufuta! Itoshe kusema, wewe ni miongoni mwa watu wachache wasiolipenda Taifa letu

Ni wale wenye kusema, nchi hata ikiibiwa hovyhovyo, haibiwi baba yako!

Wewe ni mtu wa hovyo kuwahi kutokea
 
Nachelea kuita ONYO kwa CCM.

Angalizo hili linaweza likawa la mwisho yaani msipoangalia kuna dalili mbaya sana ambayo itawagharimu na kutikisa Afrika.

Kuendelea kukumbatia Katiba inayopigiwa kelele na wananchi kuwa haifai kwa mfumo wa siasa za vyama vingi, ni sawa na kulalia kitanda cha misumari huku godoro liliwa ni kipande cha gunia.

Nimeona, yes nimesikia masikioni kwangu. Inawezekana sauti hii ilikuwa kutoka upande wa pili wa ukuta ambapo sijaweza asilani kufahamu nani alikuwa mzungumzaji. Lakini sauti inasema kuwa KIPIMO KILE MLICHOWAPIMIA WENGINE NDICHO MTAKACHOPIMIWA NA KUJAZWA KWA KUFURIKA.

Katiba hii tuliyonayo sasa ambayo mnaamini ndiyo ulinzi wa Taifa letu ni Katiba inayotoa maelekezo na maagizo muhimu (japo kwa uchache) ya maongozi ya nchi hususani kwenye Haki na Wajibu. Bahati mbaya sana mmeweka pamba masikioni na kujiweka kwenye daraja la kuwa wenye akili na ufahamu kuliko raia wote wa nchi hii. Maamuzi mengi mnayoyafanya (CCM) ni kwa maslahi mapana ya chama na walioshika madaraka.

Siku hazigandi, kwa sababu baada ya kiangazi huja mvua, mvua inaweza kugharikisha na kuporomosha milima kwa nguvu itokanayo na matone ya maji yaliyojikusana sehemu moja na kusaka njia ya kupita.

Haya fanyeni jambo la akili sasa. Mchakato wa kupata Katiba Mpya uanze mapema kabla ya uchaguzi ujao 2025 ili kuepusha yanayoepukika. Angalizo kwenu ni kwamba Katiba hii itakapokuja kutumia dhidi yenu hakika hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe kwenye ghorofa la barafu mlilolijenga tangu uhuru hadi sasa.

Sauti ya tindo za wajenzi imezidi sauti za waombolezao. Fahamuni kwamba waliao na kusugua maogti kwa nchi hii siyo wale mnaowapandisha kwenye majukwaa yenu ya kisiasa na kiserikali wakiwaombea kwa mbwembwe na ufahari wa kufaidi juisi ya watawala.

Ni mtu wa kawaida sana tena mdogo.
Sina jipya zaidi ya kufikisha ujumbe niliousikia kwa masikio yangu mawili bila kumuona mnenaji

CC Mshana Jr
Uzuri ni kwamba umeme ukikatika hauchagui nyumba ya ccm wala kiongozi
 
Katiba iliyopo inatosha.
 
Back
Top Bottom