Wazee Kumi na Saba (17) Waliodai Uhuru wa Tanganyika

Wazee Kumi na Saba (17) Waliodai Uhuru wa Tanganyika

hawa kumi na wasaba mbona wanajulikana tokea kale. au lilozidi ni lipi ?

Mkuu usemavyo ni sahihi sana! Nakumbuka hawa watu tumewasoma sana kwenye historia na siasa enzi hizo za sekondari. Tatizo kuu ni kwamba kuna genge fulani limeibuka hivi karibuni kwa malengo wanayoyajua wao wanataka kubadili au kupindisha historia yetu iliyotukuka.

Sasa, la msingi na muhimu hapa ni kuweka historia vizuri kungali mapema ili kukiponya kizazi hiki na kijacho na hila za magaidi hawa. Binafsi namshukuru sana Mh. Rais kwa majina haya.
 
kwani wewe ulilishwaje!? Kwa hiyo kumbe wewe ulimuona!!? Hebu wewe Tufafanulie!
Mbona unadandia treni kwa mbele? Mimi ndiye niliyesema kuhusu biashara ya Sykes? Acha hizo. Kama unafahamu majibu tujuze la kama hujui ni bora zaidi ukakaa kimya. Waache kina Jasusi watujibu.
 
Aliwasahau kivipi? huna jipya wewe, umemwona Ally tu mbona huzungumzi kuwahusu akina Kaselabantu, Kunambi, Rupia, Bogohe n.k?
 
walopigania uhuru wengi,huwezi toa vyeo kama zawadi hutawamaliza.watu wenyewe ndo hao wanaosema tumemvalisha suruali atawafokea vipi,au kuwawajibisha wakivurunda.yanayomsibu jk ndo hayo ya ushkaji kwenye vyeo na kulipa fadhila hua haulipi badae
 
Uliza mambo yaliyopo achana na ya Marehemu, taka kujua kwanini EL kafanya mikakat yotei ya kumwingiza Kikwete madarakani lakini Kikwete akaamua kumsaliti baada ya kujiuzulu ili kuilinda serikali na yeye mwenyewe Kikwete asiporomoke madarakani!
Usituletee porojo za vigengeni.
 
Nyerere kichwa jamani, kama angewajaza hao "wapigania uhuru" wenu wote serikalini mnafikiri tungefika hapa tulipo? Hivi hamuoni hii awamu tuliyonayo, mkulu alivyofanya kama hivyo mtakavyo. Mnaona kinachompata? Tatizo lenu mna macho ya kuona lakini hamuoni! Nyie mnafikiri waliopigania uhuru ni hao tu 17? wangeweza wapi! wapo kibao na harakati zilianza zamani mno, wengine hawakuwa hata na shule lakini walipigana kwa viwango vyao.
 
Chuma Chakavu,
Mkuu kwanza msome mtu alikotokea kisha ndio unakuja na hoja kinyume cha hapo utakuwa unarukia treni kwa mbele.. Kwanza nimesema kwamba ni nyie mnaosema JK ni mdini! kweli sii kweli... Sasa kama JK ni mdini iweje leo kasema tu habari hii unamwamini mtu ambaye ni mdini maana nijuavyo mimi mtu mdini asingeweza kusema hayo...Na nimetoa mfano wa Mohammed Said, nina hakika asingeweza kuisoma list hiyo kwa sababu haamini na hapendi isomeke hivyo... Kwa maana hiyo basi, kama unamwamini mtu ambaye unaamini ni mdini (JK) kwa sababu kasema ulotaka kusikia inakuweka wewe ktk nafasi mbaya zaidi ya Udini vile vile simply because the said what you wanted to hear!..lakini humwamini...hilo moja.

Pili. Kambona na Kawawa hata kama wameingia baadaye, swala ni watu waliotuletea Uhuru na hawa waliifanya azi kubwa kuupata Uhuru huo. Na kama swala ni kuanza harakati basi wapo watu walianzisha chama hiki na wakaishia katikati kama huyo Cecil Matola lakini naye hakutajwa. Mtu kama Mwapachu alokuwepo wakati wote, ndiye mwanzilishi wa TAA (Kisiasa) yeye na na AbdulWahid Sykes (walipompindua Kreist), ndiye aliyemgundua Nyerere na kumtambulisha kwa wanaTAA wakiwa wamekutana masomoni Uingereza... Leo mbona hayupo? nikatoa na majina mengine kina Denis Phombea, Kambona, Steven Mhando na huwezi kunambia ati hawa wamekuja baadaye wakati chama TANU kinaanzishwa walikuwa wanachama na viongozi wa juu wa chama...

Udini unakuja pale nyote hapa mnasodoana tosi kwa kuridhika na hotuba ya JK ambayo kusema kweli haikutaja wahusika wakuu wote na pengine kwa sababu maalum, lakini hakuna ukweli wowote kwamba hawa 17 pekee ndio waliotuletea Uhuru wetu... TANU ilijengwa na vyama vya kijamii 24 na kabla ya hapo TAA ya kisiasa ilikuwa na viongozi ambao hawakutajwa ktk list hiyo..Haya ndio maelezo yangu na unaponitazama mimi kwa jicho la Udini hutaweza kunielewa lakini ukiyasoma maandishi yangu vizuri utanielewa..

Kwako ndugu Mkandara,
1. Sijawahi kusema jk ni mdini na sina ushahidi wowote kuthibitisha udini wake, je wewe una ushahidi wa mimi kusema jk ni mdini? pitia post zangu ili uone! kwa nini unakuwa mzushi kwa kuniwekea maneno mdomioni!?
2. Bado sijakuelewa kabisa jinsi unavyohusisha list aliyosoma jk na mimi kuwa mdini! unaweza kufafanua vizuri kwa nini unahusisha udini na list aliyosoma jk?
3. Unasema hiyo list ndo niliyotaka kusikia; mimi sikujua jk atasema nini kwenye hotuba yake na pia hiyo list nilikuwa siijui kama ipo kwa hiyo nimeisikia jana.
4.Sina budi kuamini list aliyosoma jk kwa kuwa yeye ni kiongozi wa taifa hili,yupo karibu zaidi na vielelezo na makabrasha ya historia, na pia sioni hana haja ya kudanganya umma katika suala hili kwa sababu sioni manufaa gani atakayopata kisiasa au katika nyanja nyingine yoyote ile kwa kusema uongo kuhusu historia hiyo.
5.Kutokana na point ya 4 hapo juu,siwezi kuamini makala ya mohamed said kwa kuwa kwa kiasi kikubwa naona ni ya upotoshaji ukilinganisha na official history, yeye ni nani mpaka tuamini makala yake, kila mtu anaweza kuandika historia kutokana na mtazamo wake, sasa tumuamini nani? nadhani makala yake ingebeba maana zaidi kama ingebakia kuelezea historia ya kariakoo,mitaa yake,wakazi wake n.k kama ambavyo alivyojitahidi kuipamba makala yake.
6.Kama wewe hukubaliani na orodha aliyosoma jk badala ya kulalama tunaomba utuwekee orodha yako ambayo unadhani ni authentic na ujenge hoja za msingi ili tuweze kukubaliana nawe.
 
Hapa ndio Mwl. Nyerere anapowaacha kwa mbali viongozi wengine wa Tanzania, hasa Kikwete. Huwezi kuendesha nchi kwa urafiki-rafiki. Na naweza kumuelewa Mwl. Nyerere pale aliposema 'unaweza kuwa mtu mzuri sana, tukakaa na kunywa chai, au brandy or cherry lakini lakini kama kiongozi -hufai'. Kikwete anasumbuliwa sana na hili la kuchanganya urafiki na uongozi wa nchi. Na wakati mwingine mambo yanakwenda mrama kwa sababu anakosa ujasiri wa kuwaadhibu 'marafiki' zake pale wanapokosea. Mwishowe anaonekana hajafanya lolote la maana. Kwa mfano kwa nini bado hajatekeleza azimio la Bunge la kumuondoa Luhanjo?

Wengi wa wanaolalamika kuhusu Mwl. Nyerere na harakati za Uhuru wanaonekana kuegemea kwenye hoja ya 'personal' reward. Sijui ni nini hasa wanaona Mwl Nyerere alipata na wao wakakosa? Tena wengine kama Sykes walikuwa na uwezo wa kusomesha watoto wao nje ya nchi, wana biashara nyingi kwa kifupi wana hela. Nyerere kasomesha watoto wake hapa hapa, familia yake haiko that well off kulinganisha na viongozi wengi Tanzania.

Hivi watu kama Walter Sisulu wa South Africa walipata cheo gani baada ya Mandela kuwa rais? Mbona watu wengi waliofungwa na Mzee Mandela hawakupata vyeo serikalini lakini hawanung'uniki? Mimi nilifikiri nia ilikuwa kupata uhuru na kurudusha utu wa mtanzania na sio vyeo. Na hilo lilifanikiwa 9/12/1961 maana baada ya hapo hakuna aliyepanda basi akaambiwa hili ni watu weupe na hili ni la watu weusi. Malalamiko nje ya dhana ya uhuru naweza kusema ni 'ubinafsi'. Sorry.
 
Nadhani wengi waliomsaidia walikuwa tayari na umri mkubwa na hivyo walimshauri kuwapa nafasi vijana wenzake akina Kambona, Kawawa n.k na wao wakabakia kuwa washauri tu wa Serikali. Ndiyo maana likawepo Baraza la Wazee wa TANU na Nyerere alikuwa akiwafuata kuomba ushauri mara kwa mara, utamaduni ambao umeendelezwa hadi sasa kwenye zama za Kikwete kwa kuongea na wazee..
 
Ukweli ni kwamba huyu mzee alikuwa mbinafsi. Alikuwa ni dikteta so alijitahidi kuwapoteza wale wote aliofikiri hataweza kuwasukuma kibabe.
 
1955 wakati Nyerere anahamia Dar na kupokelewa na kuishi kwa Abdul Wahid Sykes, Dar Es Salaam haikuwa Mkoa, ulikuwa ni Jiji na Pugu ilikuwa ni kijiji nje ya Dar Es Salaam. Kwa wakati ule Pugu sio Dar Es Salaam, hata kwa sasa Mkoa wa Dar Es Salaam una jiji la Dar Es Salaam na kuna kitongoji cha Pugu. Kuwa makini, ustake nkucheke.

Bila shaka wewe utakuwa na mtindio wa uelewa wa jiografia ya nchi yetu.
Sijui hapa ndio umeandika nini pamoja na kwenda kula twisheni kwa mwalimu wako mtetezi wa wamanyema!
 
lkn jamani tuseme ukweli hii mada inarudiwa si mnakumbuka ule hot mjadala kuhusu Mwl. JKN na uhuru
 
haya mambo ya kumchimba nyerere naona yanachukua sura ya udini sa sio kufunndisha watu jinsi ya kutorudia makosa ya kuporomosha uchumi. Kama tunakerwa na uozo na maudhi ya maraisi waliopita , inatubidi kumchambua na mwinyi pia.

Si unajua katika utawala wa mwinyi, yeye ali hassan alikaa kimyaa miaka kumi yote ya uongozi wake , huku waislamu wakitukana wakristo hadharani miskitini? Sasa haya nayo lazika yajadiliwe ili raisi ajaye akiwa mzanzibari, asithubutu kufanya kama vile alivyofanya ali hassan.. ni lazima makosa ya mwinyi yaanikwe hadharani, kwa sababu katika utawala wake yeye nusura wakristo na waislamu wapigane wenyewe kwa wenyewe.

Mwinyi aliwaingiza wairani wengi sana katika vijiji vya wakristo ili wasilimishwe kinguvu. Ilifikia mpaka wairani kujiingiza sehemu ziitwazo, malonji, na Igamba, wilayani mbozi na kuwajengea miskiti mikubwa ingawa ilikuwa haina watu. Ni raisi aliyechukia wakristo vibaya sana kuliko raisi yeyote Tanganyika. sasa naye achambuliwe maudhi yake na sio kila siku tumchambue nyerere tuu,. Tusiwe wabaguzi ila tuwe wakweri daima.

Hili swala la nyerer na skye na wenzake wazamani ni la kitoto na halina siagi. Hebu tuanze kufikiria juu ya watu wsio nakzi, jinsi ya kumbana raisi awatafutie ajira.
 
Bila shaka wewe utakuwa na mtindio wa uelewa wa jiografia ya nchi yetu.
Sijui hapa ndio umeandika nini pamoja na kwenda kula twisheni kwa mwalimu wako mtetezi wa wamanyema!

Ha ha ha ha ha ha! Hakuna cha mtindio wala nini. Tatizo amejivika mawani fulani inayomwelekeza k*bla hata kwa mambo yasiyohusika. Mtu wa aina hiyo ni lazima ataona wengine ni manyang'au tu ila yeye na genge lao ndio wako sahihi.
 
The common problem shared by Tanzanians and their political leaders is the fact that both sides have a powerful predisposition in discussing trivial matters while ignoring things of national interests. Everyone may be left disappointed to see that after all the tremendous and sacrificial job executed by Nyerere in a process of seeking autonomity one may still come out and question his credibility. These calories might worth a multi-million dollar if they were dedicated to much grave discussions that will in turn help to disentangle our state from devastating penury.
 
Nahis Mwalimu alitaka watu ambao wangefanya utendaji wa serikali usonge mbele. Pia kwa nguvu walizokua nao hawa jamaa, kwa asilimia kubwa wangetaka kumcontrol mwalimu kitu ambacho kingeathiri maamuzi na utendaji wake serikalini.

Hata hivyo, sioni tija ya hii mada yako
 
kwahiyo Sisi wote tunaoshirikiana na viongozi wa chadema kwenye maandamano na mambo mbalimbali ya kudai ukombozi tk kwa wakoloni weusi ccm siku tukilikomboa taifa lzma tupewe vyeo serikalini??
 
Back
Top Bottom