Wasalam,
Jana, juzi na majuzi niliitwa na ndugu huko Mbezi. Japo wao kidogo wapo vizuri yaani ni wa kishua kiufupi.
Kama kawaida mgeni wa kiume basi utakua temporary chumba cha watoto wa kiume.
Wa ndugu nilishangaa sana nikichokutana nacho mule ndani.
Hawa vijana ni wachafu sijapata kuona toka nizaliwe.
Wakitoka nje ni watu watanashati kabisa ila mazingira ya ndani hapana kwa kweli.
Toka juzi nashinda na simu tu mda wote kuchart maana hapalaliki kuna harufu za ajabu ajabu.
Na wazazi wao wenyewe wamekausha tu. Hivi ndugu zangu najua humu kuna wazazi wa namna hiyo.
Jaribuni kulea watoto katika tabia ya usafi wajue personal hygiene.
Leo hii jumba kubwa kila kitu safi alafu unakutana na kesi ya kunguni. Serious kunguni, kitu ambacho nilijua nishamalizana navyo huko boarding school.
Hii imeniuma sana najua kuna mmoja yupo humu soma hii alafu fanya kuwakemea vijana wako najua sio wa kiume tu mpaka wa kike.
Na tabia ipo sana kwa hawa wakishua ambao wanalelewa kimayai unakuto toto la form 2 hata kufua halijui.
Shame on you
Shame upon you