Wazazi tunaofanya biashara tuwaandae watoto mapema wafike mbali kutuzidi, shule ipewe nafasi lakini iwe kwajili ya maarifa ila sio ndoto za kuajiriwa

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,077
Hata mimi mwenyewe tangu mtoto naaswa, soma sana mwanangu uje upate kazi nzuri, elimu ndio ufunguo wa maisha, n.k. misemo yote hio inapindishwa ili mtoto adhani kwamba njia pekee ya kutoboa ni kuja kuajiriwa wakati kuna alternatives far more better, elimu inatupa maarifa muhimu lakini inapopondishwa ionekane njia pekee ya kutoboa ni kutumia elimu uajiriwe hapo pana utata.

Madaraja ya watu wenye pesa kuna wafanyabiashara na wanasiasa / viongozi, huku ndiko pesa ilipo lakini uhakika zaidi ni biashara maana kwenye mambo ya siasa huko kuna complexities kibao.

Napozungumzia biashara namaanisha biashara zenye lengo la kufaidisha hata vizazi viwili vijavyo, i mean real business.

Hii nadharia ya wazazi kusema ntaanza kumuachia majukumu mtoto wangu akifika miaka 25 ni upumbavu, kwanini usimuanzishe mapema awe anazoea kidogo kidogo hata akifika 16 tu tayari anayajua mambo mengi, hivi kweli samaki kashakua mkavu unategemea atakunjika kirahisi kama yule mbichi ??

Biashara ni rahisi lakini watu wana complicate sana mambo, Biashara hata uwe na elimu ya darasa la 7 kama ukishauzoea wimbo wa biashara unayofanya unasubiri kukinga pesa zako huku watu wakidhani kwamba biashara inahitaji elimu kubwa unabaki kuwashangaza, kumbe walaaa!!

Mtu unaifanya biashara yako mwaka mzima tayari una wateja wako, tayari umeshajuana na watu wanaofanya hio biashara, umepata connections, unayajua machimbo, n.k. ishakua kama wimbo kwako unachofanya ni kutwanga faida tu.
 
Kwakweli mm plan yangu mwanangu lazima aijue biashara niifanyayo...jumamosi naenda nae ofisin kbsaa...mtoto anajengwa udogoni
 
Kwakweli mm plan yangu mwanangu lazima aijue biashara niifanyayo...jumamosi naenda nae ofisin kbsaa...mtoto anajengwa udogoni
Hata watoto wa kiarabu na wahindi hawana maajabu yoyote, ni vile wazazi wao wanaanza kuwazoesha tangu watoto waijue biashara, halafu udogoni ni muda mtu anaelewa vitu ambavyo haji kuvisahau tofauti na huku ukubwani, mtoto anafika miaka 18 tayari biashara kwake ni kama wimbo ulionasa kichwani.
 
sawa,ila kuna kukatia mitaji na madeni huko,umeandika kana kwamba biashara ni rahisi saaaaana
 
Back
Top Bottom