John John Msakuzi
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 279
- 99
Katika hotuba yake kwa wanahabari anasema Chini ya uongozi wa Rais Samia utoaji wa huduma za elimu mkoani umeimarika kwa kiasi kikubwa kupitia ujenzi na ukarabati wa miundombinu pamoja na ongezeko la walimu.
Serikali imetoa jumla ya TZS 146.69 bilioni kuanzia mwaka 2021 hadi mwaka 2025 kwa sekta ya elimu. Fedha za Elimu Bila Malipo zimeongezeka kwa TZS 9.84 bilioni, kutoka TZS 12.84 bilioni mwaka 2020 hadi TZS22.68 bilioni mwaka 2025.
Shule za msingi zimeongezeka kwa shule 171, kutoka 819 mwaka 2020 hadi 990 mwaka 2025, na shule za sekondari zimeongezeka kwa shule 67, kutoka 197 mwaka 2020 hadi 264 mwaka 2025.
Vyumba vya madarasa ya shule za msingi vimeongezeka kwa 2,026, kutoka 6,074 mwaka 2020 hadi 8,100 mwaka 2025, na vya Sekondari vimeongezeka kwa 1,796, kutoka 2,251 mwaka 2020 hadi 4,047 mwaka 2025. Nyumba za walimu zimeongezeka kwa 258, kutoka 2,076 mwaka 2020 hadi 2,334 mwaka 2025.
Ufaulu wa darasa la saba umeongezeka kwa asilimia 1.0, kutoka 69.8 mwaka 2021 hadi 70.8 mwaka 2025; kidato cha nne kwa asilimia 6.6, kutoka 88.4 mwaka 2020 hadi 95 mwaka 2025; na kidato cha sita kwa asilimia 0.04, kutoka 99.96 mwaka 2020 hadi 100 mwaka 2025.
Walimu wa msingi na sekondari wameongezeka kwa 1,635, kutoka 10,719 mwaka 2020 hadi 12,354 mwaka 2025. Vyuo vya VETA vimeongezeka kwa vyuo 3, kutoka 3 mwaka 2020 hadi 6 mwaka 2025 katika wilaya za Igunga, Uyui, Tabora, Nzega, Kaliua na Urambo. Hivyo Rais Samia ameongeza TZS10bn kwenye Elimu bure Tabora.