Wazazi msio na connection mnaosomesha watoto kwa matumaini makubwa waje kuajiriwa, mmejipangaje kisaikolojia na jinsi ajira zilivyo ngumu ?

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,451
Ajira nyingi zina nafasi zaidi kwa watoto wa maboss, watoto na ndugu wa wanasiasa wakubwa, watoto wa matajiri wanaojuana na watu wakubwa, wazanzibari wanaopewa mgao wa ajira ili kubalance muungano.

Halafu sasa kuna upande wa pili wazazi wanofosi kingi bila kujua hatma ya watoto, mmejipangaje ?

Ajira ni chache sana, vyuo vinazidi kujengwa, wahitimu wanazidi kujaa kila mwaka, division 1 na 2 zipo nyingi kama utitiri

Mmejipanga vp kisaikolojia ?
 
Acheni Fikra Mbovu Jamani hakuna boss au tajiri anae peleka mtoto Polisi, JWTZ, Ualimu, Unesi, Udaktari.

Pia bado kuna Private sector Inahitaji watu daily, Pambaneni kujuana na watu pamoja na kujua vitu. Nafasi zitawakuta tuuu.

OVER
Nani kakudanganya ?

Huko Polisi na Jeshi kuna nafasi zina power kubwa sana na mianya ya pesa ndefu, usiwachukulie poa kupitiliza !!

Kwenye ualimu na unesi ajira zao nyingi zinasimamiwa na Tamisemi, maboss wa huko hata kama watoto wao hawajasomea kada hizo wana nguvu kubwa ya kuingiza ndugu zao na watu wanaojuana.
 
Wanangu wawili wa mwisho wanaosoma, wa advance anasoma PCM ili nimpeleke ufundi. Akimaliza ajiajiri. Wa kidato cha tatu tayari anajifunza umeme wa magari kitaa wakati wa likizo. Lengo aje awe fundi pia.

Nina uhakika wataishi tu.
 
Huyo wa form 6 ungepeleka diploma baada ya kumaliza form 4, siku hizi diploma ina dili sana kuzidi form 6, huyo wa form 3 akimaliza 4 akitaka kuendelea na shule na uwezo upo peleka Diploma asomee eletrical engineering.
 
Nani kakudanganya ?

Huko Polisi na Jeshi kuna nafasi zina power kubwa sana na mianya ya pesa ndefu, usiwachukulie poa kupitiliza !!

Kwenye ualimu na unesi ajira zao nyingi zinasimamiwa na Tamisemi, maboss wa huko hata kama watoto wao hawajasomea kada hizo wana nguvu kubwa ya kuingiza ndugu zao na watu wanaojuana.

Mkuu Ushawai Fanya Usali Utumishi? Au unahisi tu.

Hao maboss wana ndugu kiasi gani waingize watu kwenye ajira zaidi ya 200 zinazotangazwa na serikali?

Nawajua watu wengi hoe hae waliopata kazi serikalini bila kujuana na mtu yeyote.

Acha imani potofu, Just GO for it with positive mindset.
 
Acheni Fikra Mbovu Jamani hakuna boss au tajiri anae peleka mtoto Polisi, JWTZ, Ualimu, Unesi, Udaktari.

Pia bado kuna Private sector Inahitaji watu daily, Pambaneni kujuana na watu pamoja na kujua vitu. Nafasi zitawakuta tuuu.

OVER
Mark my words ,miaka 10 ijayo ni hatari ,bora usizae kabisa ...AI inaenda kuchukua ajira za watu zaidi ya milion.
 
Wanangu wawili wa mwisho wanaosoma, wa advance anasoma PCM ili nimpeleke ufundi. Akimaliza ajiajiri. Wa kidato cha tatu tayari anajifunza umeme wa magari kitaa wakati wa likizo. Lengo aje awe fundi pia.

Nina uhakika wataishi tu.

Wape elimu zote mkuu, Za ufundi na zile Academics ambazo wao wanazipenda, Huwezi jua ndoto zao ni zipi
 
Ajira nyingi zina nafasi zaidi kwa watoto wa maboss, watoto na ndugu wa wanasiasa wakubwa, watoto wa matajiri wanaojuana na watu wakubwa, wazanzibari wanaopewa mgao wa ajira ili kubalance muungano.

Halafu sasa kuna upande wa pili wazazi wanofosi kingi bila kujua hatma ya watoto, mmejipangaje ?

Ajira ni chache sana, vyuo vinazidi kujengwa, wahitimu wanazidi kujaa kila mwaka, division 1 na 2 zipo nyingi kama utitiri

Mmejipanga vp kisaikolojia ?

Kwani Futungo wataendelea kutamalaki siku zote?
 
Wanangu wawili wa mwisho wanaosoma, wa advance anasoma PCM ili nimpeleke ufundi. Akimaliza ajiajiri. Wa kidato cha tatu tayari anajifunza umeme wa magari kitaa wakati wa likizo. Lengo aje awe fundi pia.

Nina uhakika wataishi tu.
Hapa kitaa hao madogo waliojifunza mambo ya Garage ,wanaringa sana yaani hawakosi pesa .

Pikipiki ufundi wake kwa mkoani unalipa ,ila ufundi wa magari katika mji kama Dar ni kazi nzuri sana na atafika mbali inshallah.
 
Ajira nyingi zina nafasi zaidi kwa watoto wa maboss, watoto na ndugu wa wanasiasa wakubwa, watoto wa matajiri wanaojuana na watu wakubwa, wazanzibari wanaopewa mgao wa ajira ili kubalance muungano.

Halafu sasa kuna upande wa pili wazazi wanofosi kingi bila kujua hatma ya watoto, mmejipangaje ?

Ajira ni chache sana, vyuo vinazidi kujengwa, wahitimu wanazidi kujaa kila mwaka, division 1 na 2 zipo nyingi kama utitiri

Mmejipanga vp kisaikolojia ?
Sasa hivi robots wanashindania Ajira na watu 😁😁
 
Ajira nyingi zina nafasi zaidi kwa watoto wa maboss, watoto na ndugu wa wanasiasa wakubwa, watoto wa matajiri wanaojuana na watu wakubwa, wazanzibari wanaopewa mgao wa ajira ili kubalance muungano.

Halafu sasa kuna upande wa pili wazazi wanofosi kingi bila kujua hatma ya watoto, mmejipangaje ?

Ajira ni chache sana, vyuo vinazidi kujengwa, wahitimu wanazidi kujaa kila mwaka, division 1 na 2 zipo nyingi kama utitiri

Mmejipanga vp kisaikolojia ?

Kwani Futungo wataendelea kutamalaki siku zote?
 
Mark my words ,miaka 10 ijayo ni hatari ,bora usizae kabisa ...AI inaenda kuchukua ajira za watu zaidi ya milion.

AI haichukui ajira za watu, Ila ina zi transform tu, Watoto wanao soma Secondary saivi watakuja kutumia A.I kama tools ya kutafuta pesa.

Mfano: Ujio wa Self Driving Tax. Tafsiri yake hatuitaji dereva Tax Tena, Mtu unaweza nunua Self driving Tax ukaiweka barabarani ikawa inakuingizia pesa.
 
Hapa kitaa hao madogo waliojifunza mambo ya Garage ,wanaringa sana yaani hawakosi pesa .

Pikipiki ufundi wake kwa mkoani unalipa ,ila ufundi wa magari katika mji kama Dar ni kazi nzuri sana na atafika mbali inshallah.
Ebwana ee !! juzi gari limeharibika nikaenda kufanyamatengenezo, fundi alipomaliza nikamwambia aandike bili nikagundua fasta atakuwa ameishia form 2, lakini ufundi nilimlipa elf 80, ana maisha mazuri kuzidi vijana wengi wenye degree zao mtaani

Nje ya ajira hizi za serikali inayolipa mishahara kama zawadi huku mtaani tunamlipa anaeweza kazi, hatujali vyeti
 
Ebwana ee !! juzi gari limeharibika nikaenda kufanyamatengenezo, fundi alipomaliza nikamwambia aandike bili nikagundua fasta atakuwa ameishia form 2, lakini ufundi nilimlipa elf 80, ana maisha mazuri kuzidi vijana wengi wenye degree zao mtaani
Wajanja sana hao ,huku Tanga madogo hawa mafundi pikipiki wanaringa sana ,hawakosi pesa ..Tatizo ni malaya sana ,wengi wanakufa kwa sifa za kuendesha pikipiki hovyo.
 
AI ni tishio kwa ajira.
Miaka mitatu ijayo ambapo watu wengi watakua na uelewa wa AI ndio mtajua hamjui
AI sio tishio kwa ajira hasa kwenye taasisi na idara za serikali za Afrika zisizojali utendaji wa kazi, kuna mashirika mengi yanapata hasara miaka nenda rudi na watu wanalipwa mpaka wanastaafu na pensheni juu yake.

AI itapunguza ajira kwenye sekta binafsi, mtu umejifungulia kabiashara kako ukiona AI inaweza unamtoa mtu unaemlipa mshahara ili kupunguza gharama uongeze faida.
 
Back
Top Bottom