Hammaz
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 7,091
- 15,513
Kwanza mimi ni Mtanganyika, ninachokifahamu ni hiki kupitia historia niliyosoma kwenye makala mbalimbali na kama sipo sahihi tafadhali nirekebishe. Suala lenyewe linahusu uhusiano wa Zanzibar na Tanganyika kwenye suala linalounda dhana nzima ya Muungano wetu. Ningependa tusafiri na historia pengine inaweza ikatupa mwangaza.Tujiulize nini? Wao si wanataka kiti, kwanini wasianzie ndani
Wana VP mzanzibar, wajumbe wa NEC-CCM, Bunge n.k. mbona hawafikishi madai yao
Lini umewasikia wakijadili ndani ya baraza la wawakilishi
Kipindi cha Abdu Jumbe Jaji Bashir Swanzy kupitia serikali ya Jumbe iliandaa hati ya mashtaka kuhoji muundo na uhalali wa Muungano kwenye mahakama maalum ya katiba ya JMT ya 1977. Lakini kwa ghafla hati hiyo ilipotea mezani kwa Abdu Jumbe na kwa kipindi hicho alikuwa ni Rais wa Znz na ilipotea kwa mazingira ya kutatanisha lakini ilionekana mikononi mwa Mwl. Nyerere. Mwalimu aliitisha kikao cha halmashauri kuu ya Taifa Dodoma, 1984 January Jumbe akabanwa kwa madai ya kutaka kuvunja Muungano. Kilichotokea ni kazi ya historia, wote tunafahamu kilichomtokea.
Mara nyingi tunaona masuala ya namna haya yakizungumzwa au kuitishwa mjadala yanayotokea yanakuwa ni historia. Sifahamu mengi ila hayo ndiyo ninayoyafahamu na pengine hiyo ndiyo imekuwa ni sababu kwa Wazanzibari kufanya hivyo, na kwa nini sisi tukose kiti UN kwa sababu Uhuru tumepata 1961 na Muungano ni 1964. Kwa nini? Au kuna kitu nakikosa juu ya hili?
Ndiyo maana swali ulilouliza juu ya Zanzibar nikakukoti na kuandika nasi tujiulize vivyo hivyo, kwa nini wamechupa kote huko na kurukia huko majuu?