Wazanzibar muungano tutaununua...

Wazanzibar muungano tutaununua...

Status
Not open for further replies.
Usiwe na wasi wasi ndugu yangu, Zanzibar itakuwa Singapore ya Afrika Mashariki ingawa mwanzo wake unaweza kuwa mgumu kidogo lakini baada ya miaka kama hamsini hivi kila mtu ataitamani Zanzibar.


Tena kipindi hicho Sefu atakuwa Rais wa Zanzibar, Jussa atakuwa Waziri anayehusika na masuala ya Dhambi, na Faridi atakuwa Supreme Leader of the People's Republic of Zanzibar.
 
"na iwe hivyo, kwani hayakuwa maisha wakati wa huo wa ukoloni?, ndio wakati huo hata kina Ali Hassan Mwinyi, Aboud Jumbe, Salmin Amour, wazee wangu walisoma, wakitibiwa bure na kijujumla maisha yao yakienda vizuri tu kuliko tulivyo sasa chini ya huu ukoloni wa Tanganyika (mkoloni mwafrika). Na tupo tayari kuanza upya kwa hivyo uonavyo wewe."

Kama yalikuwa maisha ya maana mapinduzi ya nini?
 
Ukiniuliza mimi kwa nini nilitaka serikali ya Tanganyika,sababu kubwa nitakayokwambia ni gubu la wazanzibari!Wanajua kutukana vizuri kwa kiswahili na kiingeeza!Hatimae walipoona matusi kwa wabara hayatoshi,waliamua kuhujumu wakristo wa visiwani na kuchoma maduka ya watu wa bara.Nilijiuliza sana ni kwa nini wabara walio congo,Zambia,Zimbabwe nk wanafanya biashara kwa heshima kuliko wanapokuwa zenji?Hatimaye niliona ni bora waishi peke yao kama watakavyo kuliko kukaa nao huku wakituchagulia aina mpy za matusi kila uchao

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Ingalikuwa maelezo yanayotolewa ni ya namna ya kusema kama unavyosema mtazamo ungekuwa ni tofauti, lakini mnadai kujitenga kwa jeuri sio kama watu mliosaidiwa
Ni kweli, miezi miwili na nusu ya uhuru ilikuwa ngumu sana kwa marehemu Karume kushikilia dola ya visiwa viwili kama nchi moja - alishalemewa sana na hatari ya vita vya wenyewe kwa wenyewe - kama historia inavyoonesha. Lakini kwa sasa mazingira ni tofauti na wakati ule tulipohitaji msaada wa Watanganyika ili kuepuka balaa baada ya Mapinduzi matukufu. Sasa tunaweza kabisa kujisimamia kama nchi. Historia imebadilika, watu wamebadilika, mazingira ya ki-dunia yamebadilika. Tunawashukuru Wabara kwa kupita nasi kipindi kile kigumu, lakini shukrani na heshima hii itapungua na kubadilika iwapo mtaendelea kufikiri mtoto akishakua anahitaji tena kutunzwa na kusimamiwa na mzazi. Mzazi mwenye busara humpa mtoto heshima na uhuru wa kujitawala muda unapofika kufanya hivyo!
 
Sipati picha kama baada ya muungano Zanzibar ndio ingefutwa kama Tanganyika.
yani ingekuwa Serikali ya Muungano na tanganyika tu kama ilivyo sasa Serikali ya Muungano na Zanzibar.
Nadhani wangepiga makelele hadi makoo yangekauka.

wa kulalamikia muungano huu alikuwa ni Tanganyika ambaye nchi yake imefutwa baada ya muungano.
 
Sipati picha kama baada ya muungano Zanzibar ndio ingefutwa kama Tanganyika.
yani ingekuwa Serikali ya Muungano na tanganyika tu kama ilivyo sasa Serikali ya Muungano na Zanzibar.
Nadhani wangepiga makelele hadi makoo yangekauka.

wa kulalamikia muungano huu alikuwa ni Tanganyika ambaye nchi yake imefutwa baada ya muungano.

chukua "like"
 
Sipati picha kama baada ya muungano Zanzibar ndio ingefutwa kama Tanganyika.
yani ingekuwa Serikali ya Muungano na tanganyika tu kama ilivyo sasa Serikali ya Muungano na Zanzibar.
Nadhani wangepiga makelele hadi makoo yangekauka.

wa kulalamikia muungano huu alikuwa ni Tanganyika ambaye nchi yake imefutwa baada ya muungano.

Kwa nini Tanganyika hakulalamika kwa muda wote huo japo angalau kwa sasa kelele zimeanza kusikika? Lakini pia kwanini pamoja na yote hayo CCM hasikii wala haambiwi kuhusu muungano hususan muundo wake?
 
Fursa niliyochukua hapa ni kuwaeleza ndugu zangu wazanzibar siasa za kufuata mkumbo hazifai.
1.Kwanini sisi ndo tuonekane walalamishi kwa kila jambo?

2.Kwanini tujifanye Zanzibar inatuuma sana kuliko watanganyika inavyowauma Tanganyika yao?.

3.Tuache hisia za umimi na usisi, Tumefikia mahali tumewafundisha watanganyika kutuchukia ijapokua hilo limenogeshwa na kutojitambua kwetu Wazanzibar.

3.
 
Kwa nini Tanganyika hakulalamika kwa muda wote huo japo angalau kwa sasa kelele zimeanza kusikika? Lakini pia kwanini pamoja na yote hayo CCM hasikii wala haambiwi kuhusu muungano hususan muundo wake?

Baada ya muungano kuvunjika, Pemba nao watataka kuwa nchi ili kujitenga na Unguja.
Hapo sisi watanganyika yetu macho.
Pili ni vyema ndugu zetu wa unguja na pamba wakaanza kuhamisha mali zao kwenda kwao. Ardhi mliyonunua anzeni kuiuza wakati huu mtapata bei nzuri
Mkija kuondoka kwa mtindo wa operation kimbunga, watanganyika waichukua bure
 
Fursa niliyochukua hapa ni kuwaeleza ndugu zangu wazanzibar siasa za kufuata mkumbo hazifai.
1.Kwanini sisi ndo tuonekane walalamishi kwa kila jambo?

2.Kwanini tujifanye Zanzibar inatuuma sana kuliko watanganyika inavyowauma Tanganyika yao?.

3.Tuache hisia za umimi na usisi, Tumefikia mahali tumewafundisha watanganyika kutuchukia ijapokua hilo limenogeshwa na kutojitambua kwetu Wazanzibar.

3.
Umenena mkuu kula like.!
 
Naanza kuona wazanzibar kuogopa kitu mlichokidai miongo kadhaa,ila kusema labda mpewe mda mwingine mjiandae hilo siwashauri make ni lazima mkubali kuanza na mda ndo huu,yasafisheni mapito ya bwana ili mfike kanaani salama.
 
Kama yalikuwa maisha ya maana mapinduzi ya nini?

"kwani siri hasa ya mapinduzi huijui wewe? tafuta kitabu kimoja kinaitwa "kwaheri uhuru,kwaheri ukoloni" cha Harith Ghassani unaweza kupata mwangaza. Hapa ndio tatizo lenu kubwa mapinduzi hasa hamyajui wengi wa watu wa Tanganyika"
 
Hapo kwenye bluu; let's be serious, Muungano ulizaliwa not more than three months baada ya Mapinduzi. Hii inamaanisha kwamba Zanzibar iliwahi kusimama yenyewe kama taifa huru (nje ya Muungano) kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu tu! Kabla ya hapo Mamlaka ya Zanzibar yalikuwa chini ya Mkoloni (mwarabu) tangu 1840 - 12th Jan. 1964 yaani kwa miaka 124.

Hivyo, kusema kwamba "kabla ya muungano" Zanzibar iliishije; jibu ni rahisi; YALIKUWA MAISHA YA UKOLONI WA KIARABU, labda ndio aina ya maisha wengine mnayotamani kuishi. Vinginevyo nakubaliana na mleta mada kwamba nje ya Muungano Zanzibar inatakiwa "kuanza upya" kwani kabla ya hapo Zanzibar kama taifa huru "haikuwahi kuwa na chochote" na sio kutuletea majibu mepesi na ya kijinga eti "kabla ya muungano ilikuwaje" kana kwamba Muungano ulikuja muda mrefu baada ya Zanzibar kuwa taifa huru!

MKOLONI MWARABU? Mulipokwisha kupindua mkauza nchi kwa Tanganyika na bado mpaka leo mnalalamika na Mwarabu ukiwacha Mzee Karume kwani hao viongozi wa SMZ walisoma katika serikali ya nani hata wakafika Makerere na Oxford? Je kwanini baada ya hapo for the last 50 years wameshindwa kubadilisha maisha ya mwananchi wa kawaida yakawa bora kuliko yalivyokuwa wakati wa 'Mkoloni Mwarabu'

Huko Ngambo mpaka ukifika mashamba majumba ya watu binafsi ni yale yale tokea kabla ya mapinduzi ukiona majumba mapya ya kisasa basi ama ni ya wafanya biashara au mafisa wa ngazi za juu serikalini au ya Wazanzibari walioko nje.

Na hao wafanya Biashara ni wachache nao watu aina tatu mostly Wenye asili ya Kihindi, Waarabu au Wapemba na siku hizi Wazungu. Biashara kubwa kubwa zina wapemba, waarabu na wageni.

Na kwanini Serikali zote mbili zinategemea mikopo na misaada kutoka nje na hali zimerithi utajiri wa mali za asilia na akiba kubwa ya fedha za nje.

Kwani basi Serikali zote mbili zinaenda Arabuni kuomba misaada. Au Baniani mbaya Kiatu Chake Dawa?

Hivi karibuni Oman imewapa scholarship wanafunzi wengi wa Zanzibar nafasi za kusoma nje. Imeahidi kujenga Bandari ya Mtwara kwa kukidhi mahitaji ya kuendeleza biashara ya gesi asilia amabayo itawafaa wananchi wa Tanganyika zaidi. Juzi tu serikali ya Oman imetoa Dola za Marekani milioni 700 kujenga Chuo na Msikiti mkubwa kabisa katika EA.

Serikali ya Oman imetoa misaada mingi tu kusaidia Zanzibar.

Kwanini mwaka 2005 wagombea 11wa Urais wa SMZ walienda Oman kuomba msaada wa fedha za Kampeni?

Muingereza kwenu si Mkoloni au ndio Bwana mnaempenda?

Watoto wengi wa the so called wana mapinduzi wako nje hasa UK, Canada, Scandinavia na US wamejiripuwa as wasomali na sasa wamepata uraia wa nchi hizo na wamepata kusoma mpaka elimu ya juu kwanini SMZ imeshindwa kuwatunza baada ya vifo vya wazee wao?

KWANINI MAJUMBA YA MICHENZANI SASA YANAKALIWA NA MATAJIRI BADILI YA WALE WALALAHOI WALIOLENGWA NA.SERIKAL BAADA YA MAPINDUZI?
 
Ndugu zangu wazanzibar,Ni muda mrefu sasa tumekua ktk manung'uniko kwamba serikali ya Muungano(Tanganyika) wanatunyonya.

Kumekua na rai nyingi sana za kutaka mamlaka kamili ya nchi Zanzibar ili tujiendeshe kama nchi nje ya Jamhuri ya Muungano.

Wapo wazanzibar walofika mbali zaidi na kusema sasa Muungano basi.

1.Napenda niwaulize ndugu zangu wazanzibar kabla hatujapaza yowe la kuukataa muungano huu je tumejiandaaje kujiendesha kama nchi kamili nje ya Muungano.
Una umri gani ndugu yangu? Kabla 1977 ulikuwa hujawa mwenye kuiona dunia? Kwa ufupi Zanzibar ilijiendesha wenyewe. Halafu Makamee wewe ni mwanamume? Iwapo ni mwanamme hujui kuwa binaadamu anahitaji kujitegemea? Aibu ilioje kutaka kufanyiwa mambo kwa maisha yako!

2.Niwajuze wazanzibar wenzangu kelele na manung'uniko yetu yamewaamsha watanganyika sasa wako mbioni kupata nchi yao nje ya muungano.wao wamejipanga tayari kwa hilo.
Unashangaza sana! Hivyo wewe ulitaka iweje, walale tu kwa chao? kama uliamuwa kukimbia kwenu kwa kutegemea kwa wenzako hilo ni shauri yako. Kwetu tulio wengi tunataka nao waendeshe nchi yao wajuwe utamu wa kuendesha nchi kama tunavyofanya sisi. Tanganyika ni nchi yao na wana uhuru wa kuifanya watakavyo!

3.Ndugu zangu wazanzibar kama tulikua tunafanya utani wenzetu wapo serious,kiuchumi,kisiasa.
Wamejiimarisha ktk nyanja nyingi muhimu kama nchi.JE sisi tumejiandaaje!
Jee mwenzetu unategemea wao walifika walipo kwa kufanyiwa? Aibu iliyoje , sasa tulifanya mapinduzi ya nini, si tungebaki kungojea huo utayari unaotaka wewe?

Rai yangu kwenu mdundo huu wa kuvunja muungano usituleweshe naona mwisho wake tutakuja kuwapigia magoti watanganyika turudiane kuungana.
Tafadhali tena tafadhali elewa sisi sote sio kama wewe. Kama unapenda dezo basi hamia huko na hapo tutakapokuja kuangukia wewe uwe wa mwanzo kutukatalia.

Upepo wa mabadiko
Upepo wa kisiasa
Lazima tuangalie tuna vyuo vikuu,vyanzo vya mapato zanzibar,ajira,n.k
Malalamiko na manung'uniko yasio na tija hayafai.

Hivyo Wazanzibari tulio wengi hatuna akili isipokuwa wewe? mwisho wa yote naamini wewe si Mzanzibari lakini ujumbe ndio huo hapo juu. Tulishaeleza mara nyingi kuwa tunataka muungano wa faida na makubaliano kwa pande zote.​Iwapo kudai huo usawa kuna maanisha kutaleta kuvunjika kwa muungano na iwe hivyo!
 
baada ya kuvunja muungano na bara kitakachofata ni kuvunja muungano wa zanzibar...pemba watataka nchi yao na Unguja watataka nchi yao
 
Teh teh, mkoa unatamani kuwa nchi, wacha zanzibar iende salama! Tanganyika kwanza!
 
Fursa niliyochukua hapa ni kuwaeleza ndugu zangu wazanzibar siasa za kufuata mkumbo hazifai.
1.Kwanini sisi ndo tuonekane walalamishi kwa kila jambo?

2.Kwanini tujifanye Zanzibar inatuuma sana kuliko watanganyika inavyowauma Tanganyika yao?.

3.Tuache hisia za umimi na usisi, Tumefikia mahali tumewafundisha watanganyika kutuchukia ijapokua hilo limenogeshwa na kutojitambua kwetu Wazanzibar.

3.

Na kwa kweli umimi na usisi ndio utakaowamaliza na kuwasambaratisha. Yetu macho ila twawatakia maisha mema baada ya Muungano huu ambao pamoja na ukarimu wa Tanganyika tumeishia kuambulia matusi na kila aina ya dharau kutoka kwa waZanzibari. Nendeni salama.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom